Ni uhaini - as simple as that!

Ni uhaini - as simple as that!

....bali kuna mgogoro mkubwa wa kikatiba hapo.

Kwa ujumla katiba zote mbili zina matatizo makubwa tu na kuna vipengee kadhaa ambavyo havipo harmonised. Kinachotokea Zanzibar sasa hivi ni matokeo ya udhaifu katika katiba zetu. Mahakama ya rufani mara kadhaa imekuwa ikizionya serikali zetu kutatua matatizo haya lakini hawasikii.

The Court was faced with a similar situation in Seif Sharif Hamad v. SMZ, Criminal Appeal No. 171 of 1992 (unreported). Two of us dealing with this appeal were also in the panel for that appeal. We mused over a number of incongruent provisions of the two constitutions and after that we had this to say on page 18 of the type-written judgment:

Tunapendekeza kuwa mamlaka zinazohusika katika pande zote mbili za Muungano zichukue hatua zipasazo kusawazisha vifungu hivi na vingine nyenye utata ama uwezekano wa kuleta utata baina ya hizi Katiba mbili.
A free translation would be: “We recommend to the relevant authorities on both sides of the Union, to take necessary steps to harmonize these conflicting sections and other sections of the two constitutions which are potentially irreconcilable”.

It burdens our hearts that such a solemn appeal went unheeded and failed to find purchase like the warning of the Soothsayer to Julius Caesar: “Beware the ides of March”.

Tizama pia madudu mengine haya yaliyowahi kutokea!
Again, to digress a bit, the earlier version of the 1977 Union Constitution was silent as to which government had authority over Mainland Tanzania for the non-Union Matters. The categorization that such authority was vested in the Union Government existed in the Interim Constitution of the United Republic, 1965, but it was not reproduced in 1977. Professor B.P. Srivastava in his Professorial Inaugural Lecture, “The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 – Some Salient Features – Some Riddles”, delivered on 6th March, 1982, pointed out that omission. He argued that it was unconstitutional for the Government of the United Republic to deal with non-Union Matters for the Mainland Tanzania. Probably that criticism prompted the reinstatement of the 1965 position. We make this observation to underscore the need to be painstaking in writing our Constitution.
 
yaani hata hii kauli ya kipuuzi iliyotolewa na Kikwete mwanzoni (na niliipinga wakati ule vile vile) watu hawafikirii wanachosema: "NDANI YA TANZANIA ZANZIBAR NI NCHI". Really?

Hivi hili suala si lilishamalizwa na Mtukufu Rais bungeni na kukubali kuwa Zanzibar ni nchi katika masuala yasiyo ya muungano? Je haya mabadiliko yanakingana vipi na mtizamo ule wa serikali ya Tanzania? Ukweli ni kuwa hatua hii haikupaswa kufanywa sasa kwa manufaa ya Wazanzibari wenyewe lakini pia kwa maslahi ya Tanzania. Wazanzibari walipaswa kufocus katika kufanikisha serikali ya pamoja na kuhakikisha kuwa yaliyokusudiwa kama vile kuleta kuaminiana na kushrikiana kati yao kunafanikiwa na sio kuchokonoa kina Mwanakijiji na wazee wa mjini (Mkandara).

Lakini ukiangalia kwa undani wake kilichofanyika hakina athari na muungano labda tu kwa wale ambao tayari wanamitizamo yao kuhusu Zanzibar na wanachongoja ni kupata cha kuhalalisha mitazamo hiyo, na hapa wamepata. Tupunguze munkari nyamani hizi ni nyakati za busara sio kukimbilia conclusions zisizo na mishiko. Huu ni wakati wa uchaguzi tutasikia mengi, sasa kama tutakurupuka kukaa mikao ya kivita kwa kila kinachoibuka ama kinachotengenezwa basi soon tutajikuta kubaya...

omarilyas
 
Mkuu Mwanakijiji

Hakuna atakayekusikiliza hapa tumeweka Jambazi sugu pale magogoni unategemea nini? Ameweka group la banyamelenge, Iranians, hata nyang'au naambiwa wameingia kwa mlango wa uani usitegemee kitu kwenye hiki Chama Cha Majambazi.


Angalia mambo haya.....
 
Hivi hili suala si lilishamalizwa na Mtukufu Rais bungeni

Acha kukufuru asiee.. ana "utukufu" gani?

Na pili, Rais hakumaliza suala hilo Bungeni kwani hana uwezo wa kufanya hivyo. Haya mambo ya "Rais kasema and that settles it" hayako kwenye jamhuri yako kwenye wafalme ambao wana kauli za mwisho. Alichosema siku ile ni mawazo tu potofu ambayo hayana nguvu ya kisheria.

na kukubali kuwa Zanzibar ni nchi katika masuala yasiyo ya muungano?

Haina mantiki, ni nchi au siyo nchi maana ukikubali dhana hiyo inawezekana kabisa kuongeza na nchi nyingine ndani ya Zanzibar inaitwa "Pemba" ambayo nayo katika mambo yasiyo ya "Zanzibar" itakuwa nchi!

Je haya mabadiliko yanakingana vipi na mtizamo ule wa serikali ya Tanzania? Ukweli ni kuwa hatua hii haikupaswa kufanywa sasa kwa manufaa ya Wazanzibari wenyewe lakini pia kwa maslahi ya Tanzania. Wazanzibari walipaswa kufocus katika kufanikisha serikali ya pamoja na kuhakikisha kuwa yaliyokusudiwa kama vile kuleta kuaminiana na kushrikiana kati yao kunafanikiwa na sio kuchokonoa kina Mwanakijiji na wazee wa mjini (Mkandara).

Kwa wengine ni sawa kwa sababu inaonekana inachokonoa kina mwanakijiji na mkandara badala ya kuona tatizo la kikatiba ambalo wahuni wa Zanzibari wanalilazimisha huku viongozi waoga na wazembe wakikaa na kukodolea macho.

Lakini ukiangalia kwa undani wake kilichofanyika hakina athari na muungano labda tu kwa wale ambao tayari wanamitizamo yao kuhusu Zanzibar na wanachongoja ni kupata cha kuhalalisha mitazamo hiyo, na hapa wamepata. [quote[]

Kama wewe huoni haina wengine wote hawaoni; huwezi kuwa na nchi ndani ya nchi nyingine halafu mkabakia kuwa na nchi moja (Ibara ya 1 na ya 2 ya Katiba ya Muungano). Hivi hili linahitaji microscope kuweza kuliona?

Tupunguze munkari nyamani hizi ni nyakati za busara sio kukimbilia conclusions zisizo na mishiko. Huu ni wakati wa uchaguzi tutasikia mengi, sasa kama tutakurupuka kukaa mikao ya kivita kwa kila kinachoibuka ama kinachotengenezwa basi soon tutajikuta kubaya...

omarilyas

sasa ningekuwa mimi wewe ningesema wenye munkari ni hawa jamaa wanaojaribu kulazimisha vitu ambavyo vinatokana na jazba na munkari.. but I guess huwezi kuwakemea hao au kutaka wapunguze munkari.
 
Kaka muungano hautalindwa kwa kuitana wahuni.....

omarilyas

Forest Gump alisema "stupid is as stupid does".. guess what..mhuni anajulikana kwa uhuni anaofanya. Na hili si tusi naelezea tu kile ninachokiona. Ila waweza kunisahihisha kabisa kwa kuniambia kinachofanyika si uhuni ukinishawishi nitabadili msimamo.
 
huo ni mwanzo tuu.by 2011 tutakuwa na serikali 3 .kwanini mnafikiri karume kakubali kuungana na cuf ili kuleta mseto .sababu ni kwamba alijua akianza kuchokonoa katiba na kuanza kuitetea znz ,yangelimkuta yalomfika JUMBE kufukuzwa katika chama.hata salmini alijaribu lakini kashindwa pia .so karume he decided to get cuf involved because sera ya cuf ni serikali 3 .na wanaweza kuzungumza masuala ya muungano watakavyo.wakati ccm wao lazima ulinde muungano japokuwa una kasoro kibao.that was a clever move by karume because he is using third party to fight for zanzibaris .and you know why?cause ccm znz katiba yao ya chama inawafunga kudai serikali 3 .kumbuka kwamba katiba ya ccm inasema serikali 2 kuelekea moja.
 
Forest Gump alisema "stupid is as stupid does".. guess what..mhuni anajulikana kwa uhuni anaofanya. Na hili si tusi naelezea tu kile ninachokiona. Ila waweza kunisahihisha kabisa kwa kuniambia kinachofanyika si uhuni ukinishawishi nitabadili msimamo.
mzee mwanakijiji
naona unapiga kelele lazima znz iwe kwenye muungano ,hebu nipe faida 3 ambazo tanganyika inapata kwenye huu muungano.vile vile naomba unipe hasara 3 ambazo tanganyika itapata ikiwa znz itajitenga .
ikiwa kweli tanganyika ina hamu na muungano why not unite with kenya ,uganda or whatever they speak swahili as well.ikiwa ndoa yako ina matatizo you always have to move on to find another wife or husband .you dont have to force it.
 
QUOTE=Richard;1019916]Mimi naamini kuwa ikiwa itakuwa hivyo basi yule alietiwa kizuizini na wengine ambao wanaona wako huru kutimiza ndoto zao kwa kuwa mwenyewe hayupo tena na wanaweza kumwambia huyu kijana nae akaitikia tu, huo ni uhaini wa "first degree".[/QUOTE]

:confused2:
 
Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.

Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.

Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".

Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:



Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):


na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?

Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?


Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:

(

Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!



I couldn't be more blunt than that.

Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):

Ooh how prophetic!!!

I'm standing on guard, by CHOICE!
Sasa mmeanza kubweka ee yamekushindeni ya Mafisadi mlibweka hapa wee leo wao ndio wanaokufanyeni Gari la ngombe sukani puwa, nafikiri mwanakijiji unajifanya hayawani kwa makusudi na kujisahaulisha matokeo muhimu ulisahau wakati ule mwakiyembe aliposema ndani ya Bunge eti viongozi wa Zanzibar hawana Adabu na watiwe adabu nafikiri kauli tosha ya Mr Ali juma shamhuna ilitosha kumnyamazisha yeye na wenziwe kama alivyosema Mr shamhuna ni nani mwenye uwezo wa kulitia adabu viongozi wa zanzibar?na kama wewe unahisi Hao wawakilishi watiwe pingu basi na watumwe wakuwatia pingu wafanye hivyo halafu utaona nini kitakuwa kwa tarifa yako wazanzibari hawapo Desperate na pia mabadiliko yamekuja wakati mzuri tunaanza saumu
 
mzee mwanakijiji
naona unapiga kelele lazima znz iwe kwenye muungano ,hebu nipe faida 3 ambazo tanganyika inapata kwenye huu muungano.vile vile naomba unipe hasara 3 ambazo tanganyika itapata ikiwa znz itajitenga .
ikiwa kweli tanganyika ina hamu na muungano why not unite with kenya ,uganda or whatever they speak swahili as well.ikiwa ndoa yako ina matatizo you always have to move on to find another wife or husband .you dont have to force it.

Hivi umesoma wapi nimesema kuwa ni lazima Zanzibar iwe kwenye Muungano? Nimesema, Katiba ya Muungano inasema kuna nchi moja nayo ni "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" na eneo lake ni eneo 'LOTE' la Bara na eneo lote la Zanzibar. Hili siyo gumu kulielewa siyo maneno yangu ni maneno kina Kikwete, Karume, wabunge, n.k waliapa kuyalinda.

Sasa leo kuna wahuni wa natangaza "nchi" ndani ya "nchi" wanaachiwa.

Sasa kama wanachotaka ni Zanzibar iwe nje ya Muungano, wawe tayari kutuambia tu na waweke utaratibu wa Zanzibar kutoka. Kama kinachoendelea sasa kuanzia madai ya bendera, wimbo wa taifa, serikali ya UK n.k ni hatua ya kutoka kwenye Muungano waseme tu ili tusiburuzwe kama hatuna akili.

Nani amesema ni lazima kuwe na faida 1, 2, 3, 4 ili muungano uwepo?
 
MKKJ,
Nina wasi wasi kuna mtu kavamia ID ya Mwanakijiji, na anaongea kama mlevi, anapayukwa payukwa tu, hatujuwi hasa anasimama na hoja ipi na ipi ana kataa. Tunaomba kama kuna mtu kaivamia ID ya Mwanakijiji atupe nafasi...asimtie aibu...mwenyewe kwa maongezi yasiyoeleweka eleweka.

Hapo juu kwenye post 113 unakataa kuwa hujawahi kusema Zanzibar lazima iwe kwenye muungano...wakati thread yako inakusuta kwa kauli za "tutaulinda kwa gharama yoyote", "jeshi lichukuwe hatua" n.k...na jazba,chuki na nongwa kwa Wazanzibar unaiyonesha wazi wazi kwa sababu tu kwa umoja wao wamekubali mabadiliko ya muundo wa serikali yao na hadhi yake katika muungano.

Mkuu unayejiita Mwanakijiji(siye yule ninayemfahamu kuwa mtu muelewa wa mambo), inaonyesha neno "jamhuri ya muungano" kwa kiswahili cha kusini ya Tanzania linamaanisha siku zote "nchi moja", unasahau neno kama 'muungano' linaashiria kitu zaidi ya kimoja, kwa muktadha wetu ni nchi/jamhuri mbili ambazo ni Tanganyika na Zanziabar.

Mabadiliko tuliyoyafanya wazanzibar wengi wetu (wahuni, maadui kama ulivyotuita) ni kuainisha tafsiri sahihi ya neno "jamhuri ya muungano" ambao ni wa nchi mbili ambazo kabla ya 1964 kila moja ilikuwa na "jamhuri" yake.

Kinachokufanya uwashwe sijuwi nini tena. Acha jazba na chuki zako kwa wazanzibar, sisi si mazuzu kama nyinyi sisi tuna njaa ya mabadiliko ya kweli si ya vitabuni, nyinyi endeleeni kuabudu CCM na mizimu ya muasisi wake,sisi tushatoka huko,hatutaki kurudi tena...mnaibiwa rasilimali zenu, mnanyanyaswa na kudharauliwa na watawala halafu hao hao mnawachaguwa kwa kishindo.

Sisi hatuyataki hayo na hatua za kuyaondoa ndiyo hizo tushaanza kuzichukuwa...CUF ipo ikulu...we do'nt have to wait for another saviour...he has already come. Mda huu tunahisabu tarehe tu kuifutilia mbali CCM Zanzibar, inayolea muungano wa kidhalimu...ambao hatuutaki.
 
Mbona viongozi wa Zanzibar hawathubutu kutamka wazi wazi kuwa hawautaki huu muungano... wanacho kiogopa kitu gani...!?
 
Hivi katika Uongozi wa chama cha CUF ni nani alishiriki ktk baraza la Mapinduzi - AfroShiraz Party?
 
Mwawado, bara wala hatuhitajiki kuulizwa; hili ni suala la Zanzibar..sisi tumelalamika lini kuidai Tanganyika? Kumbuka hata hoja ya G55 ilitokana na Zanzibar na OIC (rejea kitabu cha Mwalimu). Hilii ni suala la Zanzibar TU.

Siyo lazima usema uwongo kufanya watu wakuamini...ukiwa mkweli utaongezeka zaidi ya heshima. Nitajie huyo Mzanzibar aliyekuwa behind ya G55 au angalau wazanzibari 10 halisi walioshiriki humo...usidanganye watu hapa!

Kumrejea Nyerere kama shikilio la hoja yako ni kichekesho, hasa kama kuna Mzanzibar anasoma uwongo wako. Kwa wananchi wa Zanzibari wa kawaida, wanamuona Nyerere kama enemy rather than hero...ni bilisi zaidi kuliko mtakatifu, ndiyo maana hata alipokufa TVZ walipiga tarabu baada ya nyimbo za msiba,kwa maana walifurahia.

Hivyo, kama Nyerere kaandika, kasema lolote kuhusu Zanzibar hatushangai likiwa in negative. Nyerere aliichukia Zanzibar binafsi na hakuficha hata mara moja chuki zake.

Wala Nyerere hakuwahi kuficha unafiki wake kwa Wazanzibar...nilimsikia kwa masikio yangu akisema kuwa "kama wazanzibar watakataa muungano...siwalazimishi" (nashangaa wewe Mwanakijiji unaona lazima wakati Mwalimu wako haoni hivyo) na akaonyesha kuwa alikuwa anadanganya tu kusema vile (kama unavyodanganya wewe Mwanakijiji kuhusu G55 na Zanzibar).

Maana Wazanzibar waliposimama kudai makubaliano ya muungano halisi yatekelezwe, Nyerere alitumia nguvu za vitisho na kidikteta kuwafukuza viongozi wa Zanzibar madarakani...na awali alishasema kama hawataki basi hawalazimishi, hapa wamehoji tu kaja juu (kama ulivyokuja juu Mwanakijiji kwa mabadiliko ya katiba ya zanzibar), kama kizee kile hakikuwa kinafiki kilikuwa nani???

Inaonyesha kuna watu wanachuki tu na wazanzibar zisizo na sababu yoyote. kuna mfanyabiashara mmoja maarufu wa kichaga DSM, anayemiliki vyombo vingi vya habari, magazeti yake yakiandika habari za Zanzibar, mbaya mbaya kwa chuki...tu. Kitambo tulishtuka kuona vichwa vya habari kama "Mpemba akamatwa kwa Ugaidi", " Mpemba kusimama Mahakamani Leo"n.k

Kuna wakati Dr.Mwakyembe, alisimama bungeni, akitoa maneno yake ya utovu wa adabu(kama kakosa malezi vile) zidi ya viongozi na wawakilishi wa Zanzibar, na kuwaita majina mabaya mabaya (kama wewe Mwanakijiji unavyotwita wahuni, wahaini, maaduwi), jibu alilolipata kutoka kwa Ali Juma shamhuna ni "...zamani tulikufichieni maovu yenu kama taka zinavyowekwa chini ya kapeti...sasa taka hizo zinatoa harufu...hatuwezi kuziweka tena chini ya kapeti..." kama Dr.Mwakyembe angekuwa mswahili wa kweli, jibu hili lingemsononesha, maana ni tusi kwa mtu asiye na malezi kama yeye, mana yake mwanakharamu.

Kwahiyo endeleeni kutuzulia uwongo wenu kwasababu hamtaficha chuki zenu kama mwalimu wenu Nyerere alivyofanya...nayeye akazirithisha kwa waliomfuatia...hata hatukushangaa mwaka 2001, aliyekuwa amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi Tanzania, Ben mkapa(L.L), alipoleta askari na kuhujumu roho za Wazanzibari wasiokuwa na hatia yoyote, sababu tu hawaitaki CCM...dhulama ile..kuna jicho lisilolengalenga machozi kwa dhulma kama ile ya watawala dhalimu wa CCM kwa Wazanzibar...halafu bado tupende CCM tu!!!
 
Complicated idiocy.

Sijawahi kusikia wabongo wanagombania patent ya ugunduzi wa kitu hata siku moja.

Nyerere mut be rolling over in his grave.
 
Mimi bado npitia huu ukurasa nione kama kulikuwa na logic? na kama ilikuwepo je ilikuwa valid? na kama ni valid Je ni applicable? na kama ni applicable je ipo up to date? na kama ipo up todate what went wrong? na kama kuna something went wrong swali ni where did something went wrong? how? when? can it be fixed? how? by who? ...........

I
SURA YA KWANZA
MAPENDEKEZO YA NYALALI HAYAKUTOKANA NA WANANCHI​
Jambo la kwanza ambalo lilimsumbua Mwalimu ni jinsi gani hoja ya Tanganyika ilivyoletwa na kufikia
ilipofikia. Mwalimu aliona hoja hii wala isingekuwa na nafasi kama viongozi wangeweza
kuishughulikia mara moja kwa kutoa majibu ambayo ni ya kihistoria na ya kimantiki. Aliweza
kuthibitisha kwa vielelezo kuwa hoja ya Tanganyika haikutokana na mapendekezo ya wananchi bali
tume ya Jaji Nyalali ilionelea ni bora kutoa pendekezo hilo. Kwa Mwalimu, CCM tayari ilikuwa na
majibu yake kuhusu suala la serikali tatu, kwamba sera ya CCM ni serikali mbili na sababu zake
zilikuwa zinajulikana. Kitendo cha uongozi wa Chama na serikali kuliendeleza suala hili hadi kufikia
Bunge kutoa Azimio la kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ndani ya "Muungano" kilikuwa ni kitendo
kilichoonesha uwezo mdogo wa kuhimili vishindo, uongozi duni, na utetezi dhaifu kabisa wa sera za
chama. Nyerere alijikuta ni mtu pekee ambaye yuko tayari kusimamia kanuni bila ya kujali gharama
au kuangalia sura za watu​
. Alinyosha mkono juu tayari kuhesabiwa – M. M.

1. RIPOTI YA JAJI NYALALI:​
Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza mambo mengi, lakini yanayotuhusu hapa ni mawili:
(i) Pendekezo la kugeuza mfumo wa Chama Kimoja cha Siasa, na kuleta mfumo wa vyama vingi; na
(ii) Pendekezo la kugeuza mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili, na kuleta mfumo wa Shirikisho la
Serikali Tatu.
La kwanza lilikubaliwa na Chama na Serikali, na la pili likakatiliwa. Linalohitaji maelezo ni hilo la pili
Waingereza wana msemo: 'Ignorance is bliss; ujinga ni baraka.'
Wako watu wanaodhani kuwa pendekezo la Tume ya Nyalali la kutaka Shirikisho la Serikali Tatu,
linatokana na maoni au matakwa ya watu. Hiyo si kweli hata kidogo. Lakini watu wanaotaka tuamini
kwamba wasemavyo ni kweli si watu waongo, ni wajinga tu, maana nadhani hawajasoma Ripoti ya
Tume ya Nyalali. Hotuba ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, ya tarehe 30 Aprili, 1992,
katika Bunge Ia Muungano inaeleza vizuri sana ukweli ulivyo.​
Mheshimiwa Spika, mojawapo ya mapendekezo makubwa yaliyotolewa na Tume ya Nyalali lilihusu
mfumo wa Muungano na Ushirikiano kati ya Tanzania, Visiwani. Tume ya Nyalali ilipendekeza
kuubadili mfumo wa Muungano ili kuanzisha mfumo mpya ya Shirikisho lenye Serikali Tatu. Yaani,
Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar. .​
8​
Mheshimiwa Spika, hili ni pendekezo kubwa na la msingi ambavyo kama ilivyofanya Tume, Chama
Cha Mapinduzi na Serikali zimelitafakari kwa undani zaidi. Katika kufanya hivyo, historia ya
Muungano tangu tarehe 26 Aprili, 1964 hadi sasa imezingatiwa. Muungano kama mnavyofahamu
Waheshimiwa wabunge chimbuko lake ni mapatano ya "Articles of the Union yaliyotiwa sahihi na
waasisi wa Muungano; Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid
Amani Karume, Mungu aiweke roho yake pema.
Mapatano hayo yalifanywa kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania. Hilo halina ubishi.
Miungano mingi ya aina hii duniani, imefanywa na viongozi kwa njia hii au nyingine kwa niaba ya
wananchi, bila kuhojiwa na hapana sababu ya kuhojiwa kitendo hicho.​
Kwa msingi huo wale
wachache wanaohoji na kutaka kura ya maoni juu ya suala hili, hawaitakii mema nchi hii. Hoja
hiyo haikubaliwi na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tangu
kuanzishwa kwa Muungano wa nchi zilizokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa
Tanganyika, ziliungana na kuwa nchi maja na Taifa moja. Narudia tena, ziliungana kuwa nchi moja na
Taifa moja. Kwa lugha ya kigeni, 'One Sovereign State'. Hivyo imejenga msingi imara wa umoja kati
ya wananchi wa Tanzania. Tanzania Bara na Visiwani, zimekuwa zikifaidika kisiasa, kiuchumi na
kiulinzi chini ya mfumo uliopo waMuungano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakubaliana na baadhi ya sababu zilizotolewa na Tume ya Nyalali kuwa ndizo
ambazo mara nyingine zimesababisha hali ya kutoridhika na mfumo wa Muungano. Matatizo yapo,
mengi ya matatizo hayo ni ya utekelezaji yaliyojitokeza wakati wa kushughulikia mambo ya
Muungano. Na bila ya kuyaficha baadhi ya matatizo hayo ni mambo yanayohusu suala la uraia, milki
ya fedha za kigeni, ukusanyaji na mgawanyo wa maapato kurokana na kodi na ushuru wa forodha,
tatizo la formula ya kuchangia gharama za Muungano n.k. Hakuna shaka kwamba haya ni matatizo na
mara nyingine yanakera.
Hata hivyo, kwa heshima zote kwa Tume Waheshimiwa Wabunge watakubaliana nami kuwa utatuzi au
ufumbuzi wa matatizohayo, hautapatikana kwa kuanzishwa Shirikisho la Serikali tatu. Kinyume chake
hiyo itakuwa ni chanzo cha kufifia umoja na mshikamano wa Tanzania uliojengeka tangu mwaka 1964.
Inatoa mwanya kwa wasiopenda umoja huo hatimaye kuuvunja. Hiyo siyo kwa manufaa ya wananchi
wa Tanzania nzima. (Makofi) Mheshimiwa Spika, matatizo ni lazima yatatuliwe. Hivyo ni azma ya
Chama Cha Mapinduzi na Serikali kuelekeza nguvu zake zote katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo

9​
bayo. Serikali na Chama zitaendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo bayo halisi na kuyaondoa kwa
manufaa ya wananchi wote wa Tanzania chini ya mfumo wa sasa. Hivyo kwa sasa Serikali inaifanyia
kazi maeneo yanayohusika. Uhusiano wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
hasa katika maeneo yanayohusu matatizo niliyoyaainisha.
Kwa mtazamno huo, ndiyo maana katika marekebisho ya Katiba wakati huo, eneo linalohusu Rais wa
Jamhuri ya Muungano pamoja na uchaguzi wake na wa Makamu wake ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar linawekwa kando, likisubiri mapendekezo mapya ya Serikali kwa Bunge lako Tukufu kwa
kutungiwa muswada utakaowasilishwa hapo baadaye katika Bunge lako Tukufu.
Kwa wakati huu sehemu hii ya katiba itatoshelezwa kwa muda na ibara ya 37 ya katiba ya Jamhuri.
Rekebisho hili limefanywa katika Muswada na kubadili katika katiba.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia ukweli kwamba tangu mwanzo ulipoanzishwa Muungano Waasisi
kwa​
makusudi kabisa hawakutuachia muundo wa Shirikisho la Serikali tatu au Serikali moja, ni
dhahiri muundo unaopendekezwa unatutoa kutoka msingi huo wa awali. Ni mfumo ambao
unadhoofisha nchi nzima ya Tanzania. Kwani Shirikisho ambalo lingeweza kuundwa na nchi mbili
huru zenyewe zikibakia kuwa ni Jamhuri na hivyo kuwa na Serikali tatu. Halitasaidia lolole katika
kudumisha hali ya utulivu na usalama ya wananchi wetu. (Makofi)
Hapatakuwa na. mshikamano madhubuti katika masuala ya uchumi na maendeleo ya jamii na
gharama ya kuziendesha Serikali tatu, ingekuwa kubwa sana na isiyo ya lazima.
Kwa sababu hizi,
ndiyo maana Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake hazikubali pendekezo la Tume ya Nyalali la
kuanzisha mfumo mwingine wa Muungano wa Serikali tatu. (Makofi).

Isitoshe Mheshimiwa Spika, hata pendekezo hili silo la wananchi wengi. Kwani taarifa ya Tume
inasema, na naomba ni nukuu. "Zaidi ya hayo wengi wa wananchi waliotoa maoni yao kwa Tume
hawakuelezea chochote juu ya mfumo wa Serikali ambao Muungano uwe nao.
Kati ya wananchi elfu tatu (3,000) waliojitokeza kwenye Tume huko Zanzibar ni wanne (4) tu
waliozungumzia jambo hilo ambayo ni asilimia (0.13) ndio waliopendekeza kuwepo kwa mfumo wa
Serikali tatu. Na kati ya wananchi 32,275 waliotoa maoni yao kwa Tume ndio waliopendekeza mfumo​
10​
wa Serikali tatu. Wana-Tume ambao hawakubaliani na pendekezo hilo la kuwa na Serikali tatu,
walisisitiza kwamba na ningewanukuu; "Pamoja na kuelewa kuwa baadhi ya mambo mengine siyo
lazima uamuzi wake; kutegemea wingi wa watoa maoni lakini pia tunaona kuwa siyo busara
kupendekeza mabadiliko makubwa kama haya ya mfumo wa Muungano wetu kwa kutegemea maoni ya
Watanzania 49 kati ya Watanzania 36,299 walioshiriki katika mjadala wote, ulioendeshwa na Tume ya
Rais. Idadi hii ni ndogo isiyo na uzito kitakwimu."
Sisi hatuoni kuwa kuna hoja ya kisheria na ya kisiasa ya kubadili mfumo wa sasa wa Serikali mbili na
kuanzisha mfumo wa Serikali tatu.​
Tunaamini kuwa mfumo wa Serikali tatu, utadhoofisha
Muungano wetu kisiasa na kiuchumi".
(Makofi)

Hivyo ndivyo Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania aJivyosema Bungeni tarehe
30, Aprili, 1992; akashangiliwa na kupigiwa makofi na wabunge wa Tanzania. Baadaye, kama
tunavyojua, Waziri Mkuu aliisahau hotuba hii; na wabunge waheshimiwa walisahau shangwe zao na
makofi yao. Wakapitisha Bungeni, "kwa kauli moja", Azimio la kutaka Serikali ya Tanzania ilete
muswada wa kubadili Katiba ya Nchi yetu ili kuwa na Serikali ya Tanganyika "ndani ya Muungano",
kwa madai ya kwamba hayo ndiyo " matakwa ya wananchi wa Tanzania.
Lakini ukweli wa suala hili unabaki pale pale: Wananchi wa Tanzania hawadai Serikali ya Tanganyika;
na mimi nasema, u​
kifufua Tanganyika, utaua Tanzania. Fahari wawili hawakai zizi moja: "Yeltsin"
wa Tanganyika' ataua Muungano.
Lakini pia sababu zile zile za ukabiIa na udini na tamaa za
uongozi zitakazoua Tanzania hatimaye zitaiua Tanganyika nayo.

11
 
bosi junius
umesema Mda huu tunahisabu tarehe tu kuifutilia mbali CCM Zanzibar,
vipi unataka uturudishe utawala wa chama kimoja?enzi zile zishapitwa na wakati bosi,upinzani lazima uwepo in order challenge the ruling party
 
Back
Top Bottom