Nashindwa kushangaa kuona celebrity wa JF kama MKKJ unaongea pumba kama hizi kama Yussuf Makamba vile! MKKJ wakati unafikiria (endelea kufikiria maana Nyerere hafufuki tena) kuwa jeshi lilinde katiba, you sound like Hitler...Mussolin...Idd Amin and the likes.
Ujuwe hilo jeshi unalosema ni la wananchi wa Tanzania-Zanzibar, limeundwa kwa katiba ya Tanzania ambayo wawakilishi wa zanzibar inadaiwa wameshiriki. Uelewe kuwa BLW lipo kwa mujibu wa katiba na maamuzi yake yananguvu ya katiba zote mbili...chombo kingine chochote kitakachoingilia maamuzi yake kitakuwa kinavunja katiba...nakushangaa uonavyo wewe jeshi litakuwa linalinda katiba badala ya kuwa linavunja kwa fikra zako.
Kama katiba inavunjwa...Mkuu remedy yake ndiyo nguvu za kijeshi?
MKkJ, unamkumbuka mwalimu Paul Mhozya..na kesi ya OIC? kenda kumshitaki rais Mwinyi mahakamani na mahakama ikamsikiliza...MKKJ, you are suggesting military intervention for your alleged treason?
Unashindwa kujenga hoja ya maana hata kwenye jambo jepesi kama hili..unakuwa kama mtu wa maskani vile!! Post hii ikiendelea kuwapo hapa utaendelea kujishushia hadhi na heshima yako uliyojijengea kwenye mitandao...you can't talk pumbaz and nonsense like these MkkJ...you are not of such type!
Leo kama wazanzibar wataandika petition kupeleka bungeni au BLW kuwa hawataki tena muungano...katika akili yako unadhani ndiyo JWTZ litaweza kuondoa matakwa ya Wazanzibar kwenye nyoyo zao kwa nguvu za kijeshi...? Angalia tu wakati tunapiga kura ya maoni macho ya ulimwengu mzima yalihamia Zanzibar, leo unavyofikira huo 'uvamizi wa kijeshi' Zanzibar dunia itafunga mikono kukutazameni tu...?
Unadhani iwapo jeshi linavamia Zanzibar, wazanzibar tutafunga mikono tukutazameni mnfavyofanya uhuni wenu...kama mlivyowafanyia Uganda...unajidanganya? au unadhani hilo jeshi lenyewe litabaki kama lilivyo baada ya kitendo hicho...kumbuka vijana wetu wazalendo, wapenda na wenye uchungu wa nchi yao ya Zanzibar pia wamo humo humo JWTZ, so unazungumzia CIVIL WAR THEN not military intervention any more...?
Mkkj, kama bado unafikiria hivyo basi ujuwe unaishi na mzimu wa Nyerere "zidumu fikra zake" kwa kuwa kama hivyo ingekuwa ndivyo leo kusingekuwa na nchi kama Eritrea, Bosnia-Hetzegovina, East Timor na karibuni tu Cosovo...and I strongly believe that Zanzibar will, one day, not be the exception..whatever comes may.
Sitaki kusema MKKJ, unakosa heshima, adabu na busara ya kiutu uzima unapoashiria kuwaita Wazanzibar "maaduwi wa ndani", sijuwi ndani ipi! uaduwi upi! wakati walioamua mabadiliko hayo kwa mustakbali wa nchi yao ni wananchi wenyewe wa Zanzibar tena kwa wingi tu na kwa njia halali ya kidemokrasia...nakushangaa unawatangazia uaduwi...sitaki kuanzia leo nikuone kama aduwi wa Zanzibar...unless unafafanuwa ulikusudia nini unaposema "maaduwi wa ndani?"
So mabadiliko ya 10 ya katiba are there to stay...whether you like it or not...ZANZIBAR NI NCHI...tunasubiri jeshi lije...maana wanaoshindwa kwa hoja hutumia nguvu...na hii ndiyo sifa ya tawala za kidhalimu...mfano wa CCM.