Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

huwezi kujustify ufisadi mmoja kwa kulinganisha na ufisadi mwingine na kudai kila mtu anafanya kwahiyo ni sawa, unafanya tena kosa lingine kusema kuwa sitta ni spika mstaafu siyo kweli sitta alianguka kwenye primary za ccm kwenda kugombea uspika kwa kukosa sifa zilizoitajika ingawa binafsi sikubaliani nazo lakini ndio ulikuwa uamuzi wao so basically sitta was kicked out of the office hawezi kuendelea kupokea marurupu ya spika mstaafu kwani hakustafu kumbuka alitaka kugombea mtu anayestaafu hawezi kugombea cheo anachotaka kustaafu. naodha naye pia ni fisadi mwingine kama alivyo sitta kwa kutaka kujitwalia malipo hasiyostaili.

Msekwa naye alistaafu kabla au aliishachukua form na kurudisha na akaja kuangushwa na Sitta?...
 
Tanzania bila mageuzi hatutafika, tunawasomi wazuri sana lakini wanashindwa kutetea mabadiliko ya katiba badala yake wanakaa kimya eti kulinda nafasi zao au kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya. Tuamke tukatae ujinga, baba wa Taifa hayati mwl Julius Nyerere alipiga vita maadui wakuu wa tatu wa taifa ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Kukaa kimya ni ujinga, watu kama kina Sitta wanakula jasho letu bila haya alafu tunakaa tunawasifia kuwa wanatutetea. Huo ni ujinga, bado hatujaweza kupambana na adui ujinga, wana CCM wanasema Nape Nauye anajitaidi kweli, siyo kweli ni hela za allowance anazopewa kila siku na magari anayosafiria yanamfanya kubwabwaja hovyo ili waliomtuma wamwone anafaa na kumuongezea safari.
Waziri Sitta amezeeka, hatufai tena, angehama kwenye nyumba ya spika akaishi kwake ili kuokoa gharama. Hizo milioni kumi na mbili kwa mwezi mara miaka mitano ni milioni 600 tungejenga hospital ata ya watoto kwenye kata mbili.
 
Jamani hamkumbuki alivyo ifilisi CDA (Capital Develpment Authority) alikuwa anajijingea majumba yake mwenyewe kama alivyofanya alipokuwa Speaker na Kujijengea hilo JENGO la MBUNGE SPEAKER wilayani kwake wakati hakuna Lami kuelekea huko.

Alizuiwa hata kugombea Ubunge... lakini akarudi baada ya Nyerere kung'atuka

Tunamkumbatia sababu watanzania rahisi kweli kusahau ufisadi wa enzi hizo
 
Wasio mfahamu 6 ndo hao wanao msifia, na hata wabongo hawajui lengo la spika kuwa tofauti na bib kiroboto ni nin. 6 ni silent killer, nakubali wakina lowasa ni mafisadi but hata sita ni fisadi mkubwa sana,

ipo siku watanzania watajua ukweli wa huyu mnafiki 6 na ndo hapo watakapo acha kumsifia
 
Halafu huyu jamaa na roho ya kwa nini? Anapenda madaraka kuliko maelezo. Na kelele zote anazo piga ni kuutaka uraisi na ccm wasilogwe wakampitisha watakuja juta
 
mbali na kung'ang'ania kwenye nyumba ya spika pia ni mmoja wa watu lile zari la kuuziwa numba za serikali liliinufaisga sana familia yake imagine yeye na mkewe wote walinunua nyumba za serikali na nyingine wameamua kuifanya night club wakati mawaziri wetu wanalala mahotelini kwa gharama zetu. SNITCH MKUBWA.
 
mbali na kung'ang'ania kwenye nyumba ya spika pia ni mmoja wa watu lile zari la kuuziwa numba za serikali liliinufaisga sana familia yake imagine yeye na mkewe wote walinunua nyumba za serikali na nyingine wameamua kuifanya night club wakati mawaziri wetu wanalala mahotelini kwa gharama zetu. SNITCH MKUBWA.

Duu.. I was lacking this info.
 
kwa kweli inashangaza sana na inatia masikitiko kuona mtu ambaye tulidhani ni patriotic kufanya haya anayofanya sita. amegeuka sasa kuwa marketer sasa wa kile alichokuwa anapinga kwanza. inawezekanaje mtu aliyekataliwa na chama chake kugombea uspika awe spika msitaafu? angekuwa mkweli angejua kwamba hicho ni kilemba cha ukoka. au hajui kwamba hilo ndo jaribio la kupima uadilifu aliokuwa anadai kuutetea? nionavyo mimi ni kwamba sitta amepewa mtihani wa uadilifu wake na kweli ameshindwa. yale matarajio tuliyokuwa nayo kwake tuyaondoe kabisa maana ameshindwa. na kama hajui ni kwamba hata hao ccm hawapi shida kabisa. wamemjaribu na wameona alitaka nini sasa asubiri tu anguko lake la kisiasa. inaonekana ameikana itikadi yake ya kwanza ya uadilifu na uwajibikaji.
 
Lilishatolewa ufafanuzi hilo,wanasema ni kila spika mstaafu anastahili hayo,nchi yetu ina hela za kumwaga!
 
Kwa mengine yote kuhusu Sitta semeni, lakini la nyumba, msimlaumu. Nyumba ya spika inalipiwa na serikali, nyumba za mawaziri pia zinalipiwa na serikali. It was logical kwa Sitta kuendelea kuishi nyumba ile ile kwa hadhi yake ya uwaziri hivyo serikali imesave a lot kuliko angehamishwa na kuishi hotelini mpaka nyumba yenye hadhi ya spika mstaafu ipatikane. Wale viongozi wakuu watano wanastaafu na marupurupu yao yote 100%.
 
Politik is the best investment i've ever seen! Try it at your homeland!!
 
Ngoja niwamwagie dondoo kidogo za sita

Mimi binafsi nimewahi kukutana na Samwel Sitta hapa Texas miaka mingi kidogo iliyopita. Sitta alikuja na waziri mkuu wa wakati huo Sumay, Kienja na wengineo. Sitta alikuwa mkuu wa Tanzania Investent Cnt kama sikosei na walikuja hapa Houston kuongea na Watanzania vilevile Mtoto wa sumay alikuwa anaishi hapa hivyo naona ilikuwa kama shinikizo kuja Houston, TX
Baada ya Mkutano kuisha nikaona Watu wamebakia na ku chat na Sitta na Sumay, Sumay alioondoka kwenda kwenye Hotel hulala lakini sitta nikaona ameenda na jamaa mmoja na wahindi wawili kwenye chumba kidogo. Mimi nilikuwa nataka kuongea na sitta pia hivyo nikataka kuingia kwenye hicho chumba lakini yule Mtanzania mweusi akanizuia ambaye vilevile alikuwa mwenyekiti wa jumuia ya watanzania Houston. Basi mimi nikasubiri kama lisaa lizima baada ya hao wahindi wawili na huyo mwenyekiti kutoka nikamsalimia sitta na akanipa card yake.
Nikaja baadae kugundua wale wahindi wawili ni Gire na Mdogo nikauliza je huyu Gire anafanya nini mbona anaongea kichinichini na sitta?? nikaambiwa ni mfanya biashara mkubwa wa printing na anasambaza printing za City of Houston. Basi kwa ufipi ni kwamba baada ya mazungumzo ya Sitta na Gire basi Gire miezi michache akafungua kampuni ambayo ndiyo mnaijua kwa jina la Richmond ambayo ameipa jina la barabara kubwa inayopita karibu na hiyo sehemu yake ya printing pale Richmond na Fountview.
Hivyo Sitta inawezekana kabisa alimshauri Gire afungue kampuni ya Richmond na si kweli kwamba hajui hii deal kwani anajua wahusika vizuri na waliongea nae chemba kabla kampuni haijafunguliwa. Sitaki kwenda mbali sana lakini ukweli ni kwamba huyu ni mnafiki mkubwa labda Gire alimnyima pesa.
 
Paka pakawa basi kama waswahili wasemavyo.
Ukiwa mdogo unaambiwa nenda kalale mapema wakubwa wabaki macho wakiongea. Basi hii ni aina za stori wakubwa huwa tunaongea wengine wakienda kulala.

Katika hali inayoonekana kama kuangaliana kwa jicho la husudu basi CCJ wamefikia hapo katika harakati zao za kuwania madaraka ndani ya CCM. Katika kikao chao kulitokea tafrani kubwa hasa pale ilipogunduliwa kuwa Sitta ana mpango wa kuwania uraisi. Lakini wajumbe wengine wakaamua kumtolea uvivu kabisa kwa kumweleza kuwa kama ingekuwa sio unafiki basi fisadi namba moja nchini angekuwa yeye SITTA.

Tuhuma zenyewe ni hizi hapa:
<ANGALIZO: MOD ukiitoa hii naomba unifungie na account yangu kwa kuwa sipo tayari kudhalilishwa hapa JF kwa kuibua ufisadi wa mnafiki 6>

1. Inaamika ile nyumba yaani ofisi ya Spika iliyojengwa kule TABORA ilijengwa kwa fedha nyingi tena zenye utata hasa katika malipo na thamani halisi.
Katika jambo la kustajaabisha eti wakahoji ni nani alimpa ruhusa Sitta akajenge ofisi ya Spika Tabora ili hali ofisi za Bunge ziko Mjini Dodoma.

2. Inaaminika kuwa kila mwaka samani za nyumba ya Sitta pale Dodoma ilikuwa zikibadilidhwa kwa gharama ya kutisha na ambayo haikuwahi kukaguliwa na CAG. Watu wengi wamekuwa wakistaajabu haya.. Lakini ukweli huu utajulikana tuu endapo CAG ataruhusiwa kwenda kukagua.

3. Watu wamehoji hasa kuhusu yule mke wa nje wa Sitta pale Sinza. Lakini kuhusu wake za nyngeza za watu si hoja muhimu kwa hiyo sitaweza kujadili umbeya huu badala yake nitajikita zaidi kwenye hoja itakayofuata.

4. Inaaminika kuwa Sitta ana account ya mamilioni ya shilingi nje ya nchi(nchi inajulikana lakini kwenye swala la Benki bado kapuni kwa kuwa data zenyewe hazikuwa wazi). Hii ni hoja mpya kumkuta kiongozi wa tangu za enzi za mwalimu kuweza kuthibitika kuwa na uwizi wa hali ya juu.

5. Tuhuma nyingine nzito na ambao wengine waliita ufisadi ni tabia ya Sitta ya kupenda unafiki. wlimuhoji kwa nini akubali kuwa kiongozi wa serikali wakati Waziri mkuu hayupo na hapohapo aendelee kuiponda serikali. Ufisadi huu kwa mujibu wao ndio unaowaogopesha ukizingatia Sitta has NO any integrity.

6.
7.
8.

nitakuja kuzimalizi umeme ukirudi maana naona kama nimehujumiwa tayari na serikali ya kina Sitta na wasanii wengine.
 
hiyo number 3 mkuu una uhakika? maana 6 ni mzee wa kanisa letu -- futa kauli tafadhali.
 
Toa detail zaidi mkuu!! Ila hilo la nyumba ya speaker Tabora, tulishalijadili sana hapa jukwaani.
 
La nyumba ya spika tabora sio sahihi limeposhosho hizo ni ofisi za wabunge zita jengwa kila kijiomba ila
hayo mengine yanaweza kuwa sahihi hasa kuficha hela nje ya nchi kwa viongozi wetu ni kawaida sana.
SITTA anaingiza karibu milioni ishirini kwa mwezi kutokana na posho mafao
vyeo alivyowai kushika huko nyuma vyausika
 
Back
Top Bottom