Turudi kwenye hoja, malipo ya nyumba ile yanaendana na soko? Taratibu zilifuatwa? Lakini kama lengo lenu ni kumsulubu Sitta, mnaweza kuendelea na wala hamtapata suluhisho maana kesho akiwa Spika Slaa au Hamad Rashid au Marmo nk, atalipiwa nyumba hivyo hivyo kama hatutamaliza tatizo la Nyumba kwa viongozi wa Kikatiba.QUOTE]
this is materially FACT!and indeed we need to go through this plan
Duh! sasa kama hujui tofauti kati ya Spika na Naibu Waziri.. tutakuwa na mjadala mrefu kweli.
NO it does not! He is not the King of the Parliament!
Nashukuru sana kwa majibu yako , ambayo kiasi fulani yamenihuzunisha sana ! Kwa hiyo kamati ya bunge iliona ni kuzalilishwa kwa Spika kupangiwa nyumba hapo Kijitonyama ! Hivi watu wakifika hapo Bungeni mbona wanajichukulia too serious, Spika ana tofauti gani na naibu waziri. Na bunge litadhalilishwa vipi kwa yeye kuishi kwenye hizo nyumba. Mimi naona tatizo ni low self esteem !
Tunamlaumu Spika kwa sababu when it comes to our parliament issues, THE BUCK STOPS WITH HIM. Mwanasiasa yoyote makini angependa kujua ni kiasi gani kimetumika katika kulipia gharama mbali mbali zinazomhusu yeye.
sorry.. mapendekezo yako yote yanamfanya asifanane na Mtanzania wa kawaida. Mtu mwingine ataona ni kumtengenezea maisha ya anasa. Labda umodify ili yote utakayoyapendekeza yasimfanye aonekane ana maisha ya kifahari. Kutumia dola 10,000 kwa safari watu wachache sana wanaweza kutumia hizo.
Halafu dola 120 kwa mwezi ni chini ya kiwango anacholipwa Polisi, daktari, n.k sasa siyo tu umemfananisha na watu wa kawaida, bali umemshusha mno. Na kama ana watoto wadogo au walio shule atamudu kweli hata kama ana wito? Siyo kwamba tutamtengenezea mazingira ya kutafuta "fedha ya ziada pembeni"..
Nashukuru mheshmiwa Kabwe na MKJJ kwa kuwafunua watu kutoka ndani ya telescopic vision. Maana mjadala huu umekua mrefu hivi kwa watu kuangalia mtu badala ya mfumo.
Mara spika aache kupambana na ufisadi, mara msaliti,...kaazi kwelikweli.
Usihuzunike kwani hapa tunajadiliana na mjadala hata siku moja usi assume kuwa kila mtu atakuwa anakubaliana na hoja zako. Huzunika na hoja ninazotoa na usihuzunike na mimi kama Zitto.
Spika ni mhimili wa Dola. Kuna mihimili mitatu. Spika anafanya maamuzi mazito sana Bungeni na wakati mwingine maamuzi yaliyo kinyume na mhimili mmoja, hasa ule wa Utendaji ambao unaundwa na Waziri Mkuu na Mawaziri na Manaibu wao.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kukaa na Manaibu Mawaziri. Spika wa Bunge anapaswa kukaa katika makazi rasmi yaa Spika. Nimesema, makazi hayo rasmi yaliuzwa na hivyo ikabidi apangiwe nyumba kwa muda mpaka hapo makazi mapya yatakapopatikana ambayo Spika yeyote atakayekuja atakaa (yasiuzwe tena).
Hayo makazi ndiyo kodi yake hiyo. Je kodi hiyo inaendana na bei za soko?
Hakuna mahusiano kati ya makazi ya Spika na Mikopo ya wanafunzi kwani kwa vyovyote vile ni lazima mikopo ilipwe na ni lazima Spika akae katika makazi rasmi kwa mujibu wa dhamana aliyonayo.
Hili ndio tatizo letu kubwa sana. Tunahukumu haraka sana! Haki (justice) inataka tuhukumu baada ya kuwa na taarifa zote muhimu. JF haipaswi kuonea wala kupendelea, bali kusimamia ukweli na ukweli mtupu!
Hata hivyo hukumu hizi zinatokana na hasira ambazo watu wanazo kuhusu hali ya nchi yetu na ufisadi uliokithiri. Ni mchakato muhimu kupitia (yaani kuwa na hasira). Ninaamini baadae tutakuwa tunahukumu kwa haki.
Usihuzunike kwani hapa tunajadiliana na mjadala hata siku moja usi assume kuwa kila mtu atakuwa anakubaliana na hoja zako. Huzunika na hoja ninazotoa na usihuzunike na mimi kama Zitto.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kukaa na Manaibu Mawaziri. Spika wa Bunge anapaswa kukaa katika makazi rasmi yaa Spika. Nimesema, makazi hayo rasmi yaliuzwa na hivyo ikabidi apangiwe nyumba kwa muda mpaka hapo makazi mapya yatakapopatikana ambayo Spika yeyote atakayekuja atakaa (yasiuzwe tena).
mwanakijiji,naona sina hela tena kwenye internet yangu,naomba ufungue email yangu ........ paswd ni ..........angalia kwenye sentitems utazikuta ujiforwadie mara moja.
Sijasema ya kuwa nimehuzunika na wewe kama Zitto, bali nimehuzunika na hoja ulizozitoa zaidi nikizingatia ya kuwa wewe ni Mbunge wa jamhuri wa muungano. Umesema ya kuwa kununua fenicha za hizo gharama ni part ya commonwealth tradition , kwa hiyo inaonekana tunafanya vitu kwa sababu ni part ya tradition bila ya kujali uwezo wetu. Kwa hiyo inaonyesha hatuna maamuzi yetu wenyewe , ni kama mchezo wa monkey see monkey do.
Ni lazima nyie wabunge pamoja na Spika mtambue ya kuwa cheo mlichopewa ni dhamana , na Tanzania (Tanganyika, zanzibar) ilikuwepo kabla yenu na itakuwepo even after y'all have long gone! Nyerere, alitumikia taifa kwa miaka zaidi ya ishirini lakini alipostaafu serikali ilibidi imjengee nyumba . Nadhani kwa standard za bunge letu la leo hakuilinda hadhi yake vizuri ! The whole thing is ridiculous , watumishi wa serikali ni lazima mjifunze kuishi katika hali ya umaskini wetu.
Zitto umesema ya kuwa maamuzi ya kuuzwa nyumba hayakupitishwa na bunge, na kwa kuwa ile nyumba ya kwanza ya Spika aliyepewa Msekwa bado ipo , kwa nini hiyo nyumba isirudishwe baada ya kutumia milioni 200 kwa ajili ya nyumba nyingine. Mbona serikali ilirudisha nyumba zilizouzwa kwenye makazi ya polisi , kwa nini tusirudishe nyumba hiyo ; after all, Msekwa ana nyumba nyingine aliyopata thru Mke wake.
Swali langu la mwisho kwako , jee unadhani ni sahihi kwa Spika kutembelea gari lenye thamani ya shilingi milioni 300 ?
. Hao walionunua, wajue wanakaa kwa muda tu kwani ni LAZIMA hizo nyumba zitarudi tu na zile ambazo hazina sababu ya kuwapo ziuzwe kwa utaratibu wa sheria na sio kupeana peana tu!Sera nzima ya kuuza nyumba za serikali na namna zilivyouzwa mimi ninapinga
Sera nzima ya kuuza nyumba za serikali na namna zilivyouzwa mimi ninapinga. Hao walionunua, wajue wanakaa kwa muda tu kwani ni LAZIMA hizo nyumba zitarudi tu na zile ambazo hazina sababu ya kuwapo ziuzwe kwa utaratibu wa sheria na sio kupeana peana tu!
Pili, 200m sio za nyumba ni za fenicha za nyumbani...............! Hata kama ingekuwa ni nyumba ile ile, fenicha zingine zingetakiwa tu. Sasa kwamba ni fenicha za bei hiyo, hilii nalo ni la kuangalia kwa mapana na bei za fenicha zenyewe.
Tatu, Gari ya 300m! Ni gari aina gani inayozungumzwa hapa. Ni rahisi kujua bei ya gari kupitia mtandao baada ya kupata aina ya gari. Serikali hainunui magari yaliyotumika, hununua magari mapya. Hivyo kama ni mercedes au nyingine yeyote mpya tutajua bei yake sokoni. Hii gari sio ya Sitta, ni gari ya Bunge anayotumia Spika na inaweza kukaa miaka mingi sana.
Nikijua ni gari gani inayosemwa, nitasema kama naubaliana au hapana.
Naomba kuuliza; Ni nini hasa kilichopeleka serikali kuuza nyumba?
Ni nani alinufaika? "Hao" kina nani?
Mbona Adam Sapi Mkwawa alikuwa anakaa nyumba ya kawaida tu relatively speaking pale nyuma ya ubalozi wa Marekani wa zamani (Laibon) na alikuwa Spika mzuri tu?
Spika Sapi alikuwa wa zama gani na huyu ni wa zama gani? Hapo utapata jibu zuri zaidi.