Wakuu sasa hapana tunamlaumu Sitta as a person au systme inayomruhusu Spika hata ukiwa wewe au mimi kukaa kwenye nyumba ya gharama hiyo. Kuna institutional corruption lazima tuikemee pia. Tatizo hakuna mwenye uwezo na hakuna mechanism ya kupambana na bunge as institution.
Habari wanabodi,
Ni muda sijaingia humu sababu ya majukumu makubwa niliyokabidhiwa miezi mitatu iliyopita,Muda wa kupitia humu unakuwa mdogo sana.
Hii ya spiika kutumia zaidi ya milion 700 kwa muda wa miaka matano kwa malazi tu ni jambo la kupigwa vita.
Nchi ya mandondocha..sijui tumerogwa!
Mwanakijiji fuatilia hili,hiyo nyumba inamilikiwa na nani na je tender ilitangazwa kupata mzabuni.Unawez akuta hiyo ni nyumba ya kigogo wa serikali..tayari dar sasa hivi kuna nyumba za dola 8000??aisee..
Karibu mkuu Gembe. Kweli tumeku-miss. Mkuu hii ni episode nyingine ya Bongo Darisalam!!
8000 x 12 x 5 = usd 480,000 in five years only housing; kweli masikini hajijui kuwa ni masikini; hata akili haifanyi kazi. Hata Raisi hana akili!
viongozi wa hovyo huwekwa na wananchi wa hovyo
Nyumba za serikali si wameshajiuzia sasa wanabaki kupangisha.. hii akili ya viongozi wetu sijui imekaaje. chunguzeni vizuri utakuta hiyo nyumbani aliyopangishiwa ni ya hao hao tu hakuna kitu hapo ni mchezo tu wanatuchezea watanzania.
Inamaana hiyo hadhi anayotaka spika kwa kuhamishiwa nyumba ambayo alikuwa anakaa tayari na kupangishiwa nyingine hiyo ya mamilioni ni hadhi gani huyu jamaa ataitaka.
Waafrika kweli akili hatuna.. mbona mtoni kiongizo wa juu tu anakaa kwenye nyumba kama raia tu mwingine. Hiyo ni "game" tu wamecheza.. hizo hela wanajilipa wenyewe hakuna kitu hapo.. no body can agree kulipa mtu kiasi chote hicho kwa pango.. imekuwa ikulu hiyo..????
Kweli hawa viongozi wetu hawana uchungu na kodi zetu, hiyo nyumba ina nini hasa? Na kama unaworthy 10ml kwa nini wanunue na thamani tena za ml 200!?
Namna hii hatuendi popote

Hiki ni kiasi kikubwa sana kwa pango hakikubaliki,hivi wakati wanaidhinisha matumizi haya je hawakumbuki kuwa kuna watanzania ambao hawahimili milo miwili kwa siku tena makao makuu ya Serikali Dar let alone mikoani.

Huu ni ubinafsi wa hali ya juu,mimi nafikiri wameshachoka kuongoza na inabidi wapumzishwe haya matumizi hayakubaliki kabisa kwenye nchi kama ya kwetu.

Hadhi ya Spika kwani akikaa kwenye nyumba ya gharama ndiko kunakomuongezea hadhi au ni utendaji uliotukuka kwa kuthamini hali halisi na kulinda utu wa watanzania ndiko kunakomuongezea hadhi.Kwa kweki wamekengeuka na ni vipofu ambao hawastahili kutuongoza,.Hali hii haikubaliki kabisa.