Kwa ujumla, ofisi nyingi za serikali hukutwa na mapungufu makubwa tu ya hapa na pale. Lakini hili la Ofisi ya Bunge kuandikwa na Tanzania Daima ni mfululizo tu wa vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na akina RA na EL kutaka kulipa kisasi kwa Spika baada ya suala la Richmond. Hawa mafisadi wamegundua udhaifu wa wahariri wa Tanzania Daima hivyo wanawatumia ipasavyo! Jaribuni kufuatilia makala na maoni yao kuhusu Spika Sitta. Zinachefua, kwani unaona kabisa hawa watu wanatumiwa. Shame on you guys!-
Nyumba za serikali si wameshajiuzia sasa wanabaki kupangisha.. hii akili ya viongozi wetu sijui imekaaje. chunguzeni vizuri utakuta hiyo nyumbani aliyopangishiwa ni ya hao hao tu hakuna kitu hapo ni mchezo tu wanatuchezea watanzania.
Inamaana hiyo hadhi anayotaka spika kwa kuhamishiwa nyumba ambayo alikuwa anakaa tayari na kupangishiwa nyingine hiyo ya mamilioni ni hadhi gani huyu jamaa ataitaka.
Waafrika kweli akili hatuna.. mbona mtoni kiongizo wa juu tu anakaa kwenye nyumba kama raia tu mwingine. Hiyo ni "game" tu wamecheza.. hizo hela wanajilipa wenyewe hakuna kitu hapo.. no body can agree kulipa mtu kiasi chote hicho kwa pango.. imekuwa ikulu hiyo..????