Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Na bado anadai wabunge wa Tanzania wanalipwa kidogo kulinganisha na wabunge wa Kenya na hata South africa! anacheza huyu mbona halinganishi kima cha chini cha watanzania na hizo nchi?
Huyu ananuka ufisadi its time to go....

Yego Masatu

Naona leo umeamua kumkoma nyani kwetu....ni muda mrefu nilikuwa sijasoma point toka kwako...safi sana mazee welcome to the club...!
 
Wapambe wa mafisadi wanapomtuhumu mwenzao aliyehasi yetu macho mtatafunana sana mwaka huu
 
Hakuna jipya hii mada imewahi kujadiliwa mwaka jana, GT ulikuwa wapi wakati hii mada inajadiliwa ?
 
Jamani hii sasa ni nafasi nzuri kwetu hasa wana JF pamoja na vyombo vya habari kumshinikiza SPIKA wetu aachie ngazi.
No. Kabla hatuaanzisha shinikizo hilo ni vema kwanza tuhuma hizi zikathibitishwa. Itakuwa ni uonevu kuanza kushinikiza mtu ajiuzulu kwa tuhuma tu, tukianza mchezo huo, hakuna atakayebakia kwenye nafasi yake
 


Hahahaha kuna watu wengine wanachekesha duh,, kwa kweli kwa hili leo ndo nimeamini kuwa wewe ni Comrade Mpayukaji original, yaani we si wa kucopy na kupaste duh....
 
Hizi tuhuma za matumizi mabaya kwenye ofisi ya sitta, CAG ameshaisemea na kuclear hii issue kwa kusema vitabu vya mahesabu ya ofisi ya spika ni safi. Fuatilieni ripoti ya Utouh.

Hizi tuhuma zimepitwa na wakati, labda hicho kipengele cha kuongeza mishahara ya wabunge.
 



Wazazi wangu waliponambia kuwa uyaone nilifikiri Maghorofa kumbe ni haya ninayoyaona sasa, Watu kuuza utu wao kununuliwa na watu wenye nia mbaya na nchi hii na kuamua kuchafua wale ambao wanaonekana ni mwiba kwa mafisadi dah, ni aibu sana kuja hapa JF na kuanza kutoa maneno ambayo ukiambiwa utoe ushahidi wake unakaa kimya pasipo na sababu za msingi, hebu kuweni na huruma kidogo jamani na mkumbuke kuna watanzania wanaohitaji msaada wa hali na mali kutoka kwenu ambao angalau mnaweza mkashika keyboard na kutoa hoja kuliko kukubali kununuliwa ili kusafisha watu fulani fulani pasipo na sababu za msingi,, hamkawii kuipeleka hii hoja kwenye udini maana mtasema mbona anayesemwa ni muislam tumemsema mkristo wanalalamika la hasha, hapa tungependa kuona hoja zenye ukweli si hoja ambazo hazina uthibitisho. Awe mkristo awe muislamu kama kuna ushahidi basi atakemewa kwa nguvu zote.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WANYONGE WAKE WOTE AMBAO WANASHINDIA MLO MMOJA WHILE MAFISADI WANAKIMBIZA PESA NJE YA NCHI. AMEN
 
Huyu GT bila shaka bado anasumbuliwa kwa kufanya vibaya kwa Arsenal -- mwaka wa nne bila taji lolote.

Kwa vile Spika wa Uingereza kajiuzulu kwa kashfa ya kuapprove malipo ya claim hewa za wabunge ndiyo kapatia kauhalali na hivyo kijisababu cha kuchomeka kithread chake hapa -- mada ambayo ilishajadiliwa kwa kina.

Alete ushahidi wa tuhuma zote alizotaja ama sivyo aache kupayuka ovyo kwa niaba ya wezi wakuu wa taifa hili.
 
..lakini Spika Samuel Sitta ni fisadi tangu alipokuwa waziri wa ujenzi miaka ya 80 na 90. baadaye akahamishiwa wizara ya ustawishaji makao makuu Dodoma na kuendeleza ufisadi wake.

..katika masuala ya ngono ndiyo usiseme kabisa.
 
..lakini Spika Samuel Sitta ni fisadi tangu alipokuwa waziri wa ujenzi miaka ya 80 na 90. baadaye akahamishiwa wizara ya ustawishaji makao makuu Dodoma na kuendeleza ufisadi wake.

..katika masuala ya ngono ndiyo usiseme kabisa.


Na we nawe ndo wale wale.... Leteni ushahidi hapa sio bla bla tu ilimradi muongeze idadi ya post
 
Rostam anajitahidi... hadi kurecycle pseudo news... ujumbe ni kuwa Sitta anawasubiri Bungeni..!!!
 
inaelekea huyu Sitta naye ni mtazamaji sana wa hii forum

kuandikwa jana leo kajibu

sasa hii ndio tunavyotaka
 
mwenzie keshajiuzulu

Kwa bongo ndugu yangu hata akutwe na gunia la mali ya wizi bado inakuwa ngumu... Tatizo ni culture ya good goernance and accountability bado tunajikongoja

Tukienda kwa staili hiyo nadhani itabidi tupitie na matumizi ya wabunge (if are serious on accountability) wote na liquidations/claims zao... utaona wote wanajipanga nyuma ya spika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…