Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Ni kwel ila mkuu ukiulizwa swali sio la kawaida la kitaalamu ulitolee maelezo kwa lever ya elimu fulani kwa lugha fulani ukatoa vizur kabs alafu ata kingeleza cha kuombea maji ujui ni kutoka speed wakati huna break what do u expect ahahahaha only tz
*Level
*Kiingereza

Sasa wewe lugha unayoiweza ni ipi?
 
Kuna haka kamsemo " ni Tanzania Pekee a.k.a Only in Tanzania" nimekuwa nikikutana nako kwenye nyuzi mbalimbali humu JF. Nimetumia muda mrefu kutafakari haka kamsemo na nimegundua kweli ni only in Tanzania kuna mambo mengi yanatokea yakushangaza kama si kutuaibisha watanzania.

Ifuatayo ni sehemu ambazo nimekuta huu msemo ukitumika.

Ni Tanzania pekee Tanzanite inachimbwa lakini soko kuu la Tanzanite ni Kenya na India.

Ni Tanzania pekee mwizi wa mali ya uma anajulikana lakini hachukuliwi hatua yeyote.
b4b3d1b37e190d66c0fad46d3c95f223.jpg

Ni Tanzania pekee mtu ana PHD lakini hawezi ongea kingereza.

Ni Tanzania pekee Mwenyekiti anajiuzuru tena kwa barua na mbwembwe tele kwenye media ila baada ya mwaka anarudi kwa ubabe nakudai na yeye ndiye Mwenyekiti halali.

Ni Tanzania pekee pesa za maafa/rambirambi zinageuka kuwa za lambalamba.

Ni Tanzania pekee Waziri Mkuu anaulizwa swali anajibu Naibu Spika.

Ngoja niishie hapo mengine mtaongeza wenyewe, maana ni Tanzania pekee ukiongea ukweli unaitwa mchochezi.
 
Hiyo ya PHD kutoweza kuongea kiingereza si Tanzania pekee..

Maprof wa urusi na china sio wote wanajua english, na hawaoni kama ni shida
Urusi na China kutoweza ongea kiingereza siyo tatizo. Tanzania tunaanza kujifunza kiingereza darasa la 3. Sekondari hadi chuo kikuu tunafundishwa kwa kiingereza. Kutoweza ongea kiingereza vizuri ni tatizo kubwa.
Kwetu sisi Kiswahili na Kiingereza ni official languages. Ndiyo maana kwa madiwani na wabunge moja ya sifa katika kugombea ni kujua kuandika na kusoma kiswahili au kiingereza.
 
Ni Tanzania pekeee Vijana wanagawiwa Smartphone na Mafisadi ili washinde kwenye Mitandao ya Kijamii Kutukana Serikali na Viongozi wake na Kueneza Uongo.
 
Gari linaheshimika kuliko nyumba. Mwenye gari anaishi nyumba ya kupanga anaonekana wa maana kuliko anaeishi kwake na hana gari.
 
Ni tanzania pekee mtu anaandika post pumba kama hii [emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
 
Hiyo ya PHD kutoweza kuongea kiingereza si Tanzania pekee..

Maprof wa urusi na china sio wote wanajua english, na hawaoni kama ni shida
Ila maprof wa Urusi na China wasiojua kiingereza wana faida, faida yao wanaitumia elimu yao kivitendo. Maprof wa Tanzania wasiojua kiingereza hawana faida, hawaitumii elimu yao kwa vitendo wala kuitajirisha nchi.
 
Tambua katiba inatambua rasmi lugha mbili kiswahil Na kingereza so inakuwaje MTU ana PhD hajui hata kurepresent?aibu kweli hii ni Tanzania pekeee!urusi sio hapa fuatilia katiba yao inatambua nn!ondoeni UNYUMBU
 
Hiyo ya PHD kutoweza kuongea kiingereza si Tanzania pekee..

Maprof wa urusi na china sio wote wanajua english, na hawaoni kama ni shida
Kwani walisoma PHD zao kwa kiingereza?
 
1) Hata almasi zote zinazochimbwa duniani soko kuu ni Ujerumani. Kahawa ya duniani soko kuu ni Uingereza.

Hilo la kwanza, ni ujinga tu kudhani kuwa kwa kuwa unachimba madini basi soko kuu litakuwa kwako.

Ndizi hazilimwi Dar. Lakini mahakama ya ndizi (soko kuu la ndizi) lipo Dar.

Ni ujinga tu umetujaa Watanzania mpaka tunafikia kuwa na fikra za kijinga.
Hiyo kesi naona ni yofauti na ya Tanzanite, mchimbaji mkuu anaweza kuwa mzaaji mkuu since kenya wameweza kuwa wauzaji wakuu!!
 
Gari linaheshimika kuliko nyumba. Mwenye gari anaishi nyumba ya kupanga anaonekana wa maana kuliko anaeishi kwake na hana gari.
Utakuwa huna gari we!!!
Btw hapa sio mahara pa kutolea ya moyoni. Anyway!! Ni Tanzania pekee
 
Hiyo kesi naona ni yofauti na ya Tanzanite, mchimbaji mkuu anaweza kuwa mzaaji mkuu since kenya wameweza kuwa wauzaji wakuu!!
Ilo ni tatizo ndlo tunaloongelea. Ni ujinga unazalisha wewe lakini anatajirika meingine. Mfano mzuri ni wakulima wengi tz ni masikini lakni unakuta wale madalali wa mali zao ndio matajiri.
 
Hiyo kesi naona ni yofauti na ya Tanzanite, mchimbaji mkuu anaweza kuwa mzaaji mkuu since kenya wameweza kuwa wauzaji wakuu!!

Haya anzisha basi soko la Tanzanite popote ulipo Tanzania na ulifanye soko kuu.

Unangoja nini, unafikiri Kenya kuwa na soko kubwa la Tanzanite walianzishiwa na serikali yao?
 
Ilo ni tatizo ndlo tunaloongelea. Ni ujinga unazalisha wewe lakini anatajirika meingine. Mfano mzuri ni wakulima wengi tz ni masikini lakni unakuta wale madalali wa mali zao ndio matajiri.

Anzisha soko. Unangoja nini?
 
Ni tanzani pekee viongoz na huvunja sheria za barabaran kwa kutanua pemben
 
Back
Top Bottom