Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Kuna haka kamsemo " ni Tanzania Pekee a.k.a Only in Tanzania" nimekuwa nikikutana nako kwenye nyuzi mbalimbali humu JF. Nimetumia muda mrefu kutafakari haka kamsemo na nimegundua kweli ni only in Tanzania kuna mambo mengi yanatokea yakushangaza kama si kutuaibisha watanzania.

Ifuatayo ni sehemu ambazo nimekuta huu msemo ukitumika.

Ni Tanzania pekee Tanzanite inachimbwa lakini soko kuu la Tanzanite ni Kenya na India.

Ni Tanzania pekee mwizi wa mali ya uma anajulikana lakini hachukuliwi hatua yeyote.
b4b3d1b37e190d66c0fad46d3c95f223.jpg

Ni Tanzania pekee mtu ana PHD lakini hawezi ongea kingereza.

Ni Tanzania pekee Mwenyekiti anajiuzuru tena kwa barua na mbwembwe tele kwenye media ila baada ya mwaka anarudi kwa ubabe nakudai na yeye ndiye Mwenyekiti halali.

Ni Tanzania pekee pesa za maafa/rambirambi zinageuka kuwa za lambalamba.

Ni Tanzania pekee Waziri Mkuu anaulizwa swali anajibu Naibu Spika.

Ngoja niishie hapo mengine mtaongeza wenyewe, maana ni Tanzania pekee ukiongea ukweli unaitwa mchochezi.
Duuh,ndo maana jf inawaumiza kichwa balaa.
 
Aisee wewe ni kichwa panzi ,kwani hujui katibu mkuu ndiye mtendaji katika taasisi nyingi kama vyama na mwenyekiti ni kiongozi tu? Sasa ajabu iko wapi mwenyekiti kutokuwa na elimu kubwa kuliko katibu wake. Halafu mtu asiye na elimu hawezi kuendesha biashara na kuwa na mafaniko mithili ya mwenyekiti unayemsema, mtu asiye na elimu hawezi kusimamia chama kwa imara kama huyo unayemlenga. KUNA UTOFAUTI KATI YA KUMALIZA MADARASA MENGI NA ELIMU NDIYO MAANA WEWE NA ELIMU YAKO HAUNA CHOCHOTE CHA MAANA TUKIKULINGANISHA NA HUYO FORM SIX DIV 0. MWISHO WA SIKU ISSUE SI VIDATO BALI PRODUCT YA VIDATO HIVYO KATIKA MAISHA YAKO NA JAMII.
Ni TZ pekee mtu akiambiwa ukweli hutoa povu[emoji23]
 
Hiyo ya PHD kutoweza kuongea kiingereza si Tanzania pekee..

Maprof wa urusi na china sio wote wanajua english, na hawaoni kama ni shida
Kama mtu alisoma hiyo Phd kwa lugha isiyo ya kiingereza hata asipojua kiingereza hatushangai.

Tatizo linakuja pale hiyo Phd ilisomwa kwa kutumia kiingereza alafu muhitimu wa hiyo Phd hajui kiingereza.no offense intended[emoji35] [emoji35]
 
Ni tanzania pekee ambapo watu wanaohoji elimu ya mkuu wanaitwa wahaini.
 
Ni Tanzania pekee kwenye hifadhi za wanyama kuna makaburi ya kuzika wanyama pori
 
Ni Tanzania pekee wanasiasa wakiwa vijana wanakitumikia chama cha kijani,
Wakizeeka na kuchoka wanahamia buluu nyekundu na nyeupe.
 
Ni tanzania pekee watu wanachangiana harusi mamilioni ya shilingi kwenye swala la elimu awachangiani
 
Utakuwa huna gari we!!!
Btw hapa sio mahara pa kutolea ya moyoni. Anyway!! Ni Tanzania pekee
UTAKUWA HUNA NYUMBA WEWE! maajabu wa waswahili wa tanzania anauza nyumba ya urithi kununua gari!
 
Ni Tanzania pekee ambapo, Kiongozi naye anahitaji Muongozo !
 
Kwani walisoma PHD zao kwa kiingereza?
Maprof. wa China na Urusi hata wasipojua kuongea Kiingereza kumbuka hiyo siyo lugha yao rasmi kama ilivyo kwa Tanzania, Kiingereza ni lugha rasmi hivyo tunatarajia yule anayeitwa msomi hasa kwa viwango vya PHD lazima ajue kuandika na kuzungumza kwa ufasaha Kiingereza
 
Ni Nchi yenye kila kitu cha kuleta utajiri wa Nchi hivyo vitu havizungumziwi kutwa utasikia ushuru wa boda boda ili kuongeza mapato madini,gesi,makaa ya mawe hutokuja kusikia wala kujua vinaliingizia Taifa pato la kiasi gani...
NI TANZANIA PEKEE MWEKEZAJI ANAPEWA MADINI ACHIMBE YAWE YAKE LAKINI NCHI INAOMBA KODI TU KUTOKANA NA MADINI HAYO.
 
Ni tanzania pekee nchi ina ukame lakini haina njaa
 
haaahahahahahahahahahahaha
Kama mtu alisoma hiyo Phd kwa lugha isiyo ya kiingereza hata asipojua kiingereza hatushangai.

Tatizo linakuja pale hiyo Phd ilisomwa kwa kutumia kiingereza alafu muhitimu wa hiyo Phd hajui kiingereza.no offense intended[emoji35] [emoji35]
hahahahahahahahahahah
 
  • Thanks
Reactions: Lee
NI TANZANIA PEKEE NDIYO NCHI YANGU BABA NA MAMA YANGU. .NITAKULINDA TANZANIA YANGU ...MPENZI WANGU. ..NAKUOMBEA BARAKA ZOTE ZA MAULANA NCHI YANGU . ....ENDELEA KUSHINE KAMA JUA MILELE YOTE. ...
 
Back
Top Bottom