Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,692
Kuna haka kamsemo " ni Tanzania Pekee a.k.a Only in Tanzania" nimekuwa nikikutana nako kwenye nyuzi mbalimbali humu JF. Nimetumia muda mrefu kutafakari haka kamsemo na nimegundua kweli ni only in Tanzania kuna mambo mengi yanatokea yakushangaza kama si kutuaibisha watanzania.

Ifuatayo ni sehemu ambazo nimekuta huu msemo ukitumika.

Ni Tanzania pekee Tanzanite inachimbwa lakini soko kuu la Tanzanite ni Kenya na India.

Ni Tanzania pekee mwizi wa mali ya uma anajulikana lakini hachukuliwi hatua yeyote.
b4b3d1b37e190d66c0fad46d3c95f223.jpg

Ni Tanzania pekee mtu ana PHD lakini hawezi ongea kingereza.

Ni Tanzania pekee Mwenyekiti anajiuzuru tena kwa barua na mbwembwe tele kwenye media ila baada ya mwaka anarudi kwa ubabe nakudai na yeye ndiye Mwenyekiti halali.

Ni Tanzania pekee pesa za maafa/rambirambi zinageuka kuwa za lambalamba.

Ni Tanzania pekee Waziri Mkuu anaulizwa swali anajibu Naibu Spika.

Ngoja niishie hapo mengine mtaongeza wenyewe, maana ni Tanzania pekee ukiongea ukweli unaitwa mchochezi.
 
Ni Tanzania pekee ambapo wasomi wengi wanaaminiwa kuongoza taasisi nyeti kama mifuko ya kijamii etc...lakn ubunifu ni zero...wanaongoza kwa kusema Ulaya wanafanya hivi (copy & paste )...na wanalipwa hela mingi kwa hizo copy and paste zao....eg..FAO la kujitoa
 
Ni Nchi yenye kila kitu cha kuleta utajiri wa Nchi hivyo vitu havizungumziwi kutwa utasikia ushuru wa boda boda ili kuongeza mapato madini,gesi,makaa ya mawe hutokuja kusikia wala kujua vinaliingizia Taifa pato la kiasi gani...
 
Back
Top Bottom