Ni sahihi mwanamke kumkosoa mume wake/boyfriend?

Sheillah, wee kwenu ni wangapi kuzaliwa? Na umezaliwa mwezi gan??
Si unaona wenyewe wanasema hawapendi.
Usikute nawewe ni wale watu ambao, anaweza kukukuta umekaa kwenye kiti.

Kwa heshima ukaamua kumpisha yeye akae.

Maajabu, akatoa kwanza kitambaa, akafuta kile kiti weeee..kisha ndo akakaa.

Ukiwa wa ivo, basi utaumizwa na vingi sana , vingine fanyaga kuvimezea tu.
 
Nmekuelewa Mama, changamoto ulonayo niiyo,mwenzako ni mjuaji .

Kwan wee huwezi mbebea aibu zake?

Endelea kumkosoa kwa uzuri,.ukimpa uthibitisho ,kuna wakati atafikia atajishtukia.

Sema pole sana.

Una umri gan?? Nayeye anaumri gan??
Nina 24 na yeye ana 31.
 
Sheillah Pole sana.
Kwenye mahusiano ukitaka kujua haujapata mtu sahihi utagundua kwamba inakulazimu kuvumilia vitu vingi ili maisha yasonge.

Baadhi ya wanaume wana dhana ya kwamba hao ni kichwa na kichwa hakikosei.

Mimi wakwangu anaiamini akili yangu kuliko anavyoiamini yakwakwe. Nilisoma nae chuo, mimi ndio nilikuwa namfundisha na kwenye mitihani ananitegemea kwa kiasi kikubwa.

Kazini tangu kwenye interview alikuwa ananitegemea mimi yaani nianze kumhoji mimi nimwelekeze na namna ya kujibu. Maana yake mimi nifuatilie kuhusu kazi anayoiomba na aina ya maswali ambayo huwa yanaulizwa na namna ya kuyajibu.

Anafanya kazi sehemu tofauti na mimi, ila kazi zake na utendaji wake naujua mimi zaidi ya yeye anavyozijua. Kiasi kwamba kazi zake anakuja nazo nyumbani na yupo tayari kuandaa dinner mimi nimfanyie kazi zake.

Akiandaa reports mpaka anipe mimi nizihakiki ndipo azipeleke sehemu husika. Hadi sasa anatamani nifanye kazi kama secretary wake kazini kwake. Maana kila kitu lazima aanze kwangu kuhusu ushauri.

Hivyo basi namkosoa vizuri sana, na anapenda sana. Anakubali kwamba kwenye nimemzidi uwezo kwenye mambo hayo, na hilo haoni tabu.

Kwahiyo ni vyema kujua mwanaume unayetaka kuingia naye kwenye mahusiano ni wa namna gani ili isije kukulazimu kuvumilia mambo ambayo yanapaswa kurekebishika. Hapo hajakuoa lakini umeshaona unaingia kwenye ndoa na maumivu au majuto moyoni. Haifai.
 
Mwenzangu wewe mshukuru Mungu.
Huyu wangu hataki kusikia umemzidi kitu. Na ikitokea akakuuliza kitu anajidai amesahau umkumbushe. Yeye anajua kila kitu.
 
Kumkosoa mtu kwasabu kaongea Kingereza kibovu kwa bongo unaonekana umemdharau na kum-prove kua hana akili.

Wengi wanafanya kosa hilo wanakushusha vyeo unaonekana huna akili so Don't cover the book by its judge
Hahahahaha hapo yenyewe umeyumba ili kuonesha msisitizo ama nini?
"Don't cover a book by its judge"
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hakuna mtu ambaye anajua kila kitu duniani. Kumkosoa ni muhimu lakini unamkosoa kistaarabu. Leo kakosea kwako kesho atakosea kwa watu wengine. Ni vizuri kumkosoa kama ni muelewa haitakuwa issue ila kama si muelewa anaweza KUNUNA.

Lakini unakuta kakosea kabisa.
 
Sheillah Pole sana.
Kwenye mahusiano ukitaka kujua haujapata mtu sahihi utagundua kwamba inakulazimu kuvumilia vitu vingi ili maisha yasonge.

Baadhi ya wanaume wana dhana ya kwamba hao ni kichwa na kichwa hakikosei.

Mimi wakwangu anaiamini akili yangu kuliko anavyoiamini yakwakwe. Nilisoma nae chuo, mimi ndio nilikuwa namfundisha na kwenye mitihani ananitegemea kwa kiasi kikubwa.

Kazini tangu kwenye interview alikuwa ananitegemea mimi yaani nianze kumhoji mimi nimwelekeze na namna ya kujibu. Maana yake mimi nifuatilie kuhusu kazi anayoiomba na aina ya maswali ambayo huwa yanaulizwa na namna ya kuyajibu.

Anafanya kazi sehemu tofauti na mimi, ila kazi zake na utendaji wake naujua mimi zaidi ya yeye anavyozijua. Kiasi kwamba kazi zake anakuja nazo nyumbani na yupo tayari kuandaa dinner mimi nimfanyie kazi zake.

Akiandaa reports mpaka anipe mimi nizihakiki ndipo azipeleke sehemu husika. Hadi sasa anatamani nifanye kazi kama secretary wake kazini kwake. Maana kila kitu lazima aanze kwangu kuhusu ushauri.

Hivyo basi namkosoa vizuri sana, na anapenda sana. Anakubali kwamba kwenye nimemzidi uwezo kwenye mambo hayo, na hilo haoni tabu.

Kwahiyo ni vyema kujua mwanaume unayetaka kuingia naye kwenye mahusiano ni wa namna gani ili isije kukulazimu kuvumilia mambo ambayo yanapaswa kurekebishika. Hapo hajakuoa lakini umeshaona unaingia kwenye ndoa na maumivu au majuto moyoni. Haifai.
Wanawake kama wewe ndio mna sehemu yenu spesho mbinguni yenye free wifi na wall socket huku mkiandaliwa kiepe yai na kuku choma na malaika kila mkisikia njaa. Napenda sana mwanamke ambaye sio mbinafsi...you prove to be one straightaway kupitia hili bandiko.
 
Habari.

Moja ka moja kwenye maada, Ni sahihi mwanamke/mke/girlfriend kumkosoa mume wake/boyfriend anapokosea?.

Mfano, mwanaume kamtumia mwanamke/mke wake text kwa lugha ya English. Hiyo text ikawa na makosa, sio ya bahati mbaya bali ni kwamba mwanaume hajui hiyo lugha vizuri. Mwanamke akichukua hatua ya kumrekebisha ni kuonesha dharau?

Mfano mwingine, mwanaume anamwelezea kitu mke wake, na anavyomwelezea sio sahihi, na mwanamke anajua usahihi wa hilo jambo. Akimkosoa atakuwa ameonesha dharau? Au mwanamke anapaswa asikilize tuu hata kama anapigwa fix?.

Wanaume na wanawake naombeni maoni yenu.
Nakushauri usijaribu kuoa siku za karibuni
 
Back
Top Bottom