Sheillah Sheillah
JF-Expert Member
- Jun 17, 2020
- 695
- 1,803
- Thread starter
- #21
Comments mpaka hapa, nimeshaona hili ndilo la msingi.Wee jifanye tyuuh " ndio mzee" ili yey ajisikie faraja na mahusiano yenu yadumu.
Comments mpaka hapa, nimeshaona hili ndilo la msingi.Wee jifanye tyuuh " ndio mzee" ili yey ajisikie faraja na mahusiano yenu yadumu.
😂😂😂kama ninyi wote ni waswahili kuna haja gani ya kutumia kiingereza mpaka mkosoane, si mtumie tu kiswahili, hayo ya kukosolewa ataenda kukosolewa huko mbele kwa mbele.Na hapo kwenye lugha? Nitumie njia gani kumrekebisha asione kama namletea dharau na kujiona ni msomi kuliko yeye?
Kuna mdada wa Tangazo la Tigo , unajua kwann Amekua Gumzo kwa wanaume Tanzania nzima kiasi kwamba hata mimi nmejikuta nasajili Tigo? ....Hofu ya kimakosa ilisahihishwa kwa lugha na mbembelezo wa kimataifa.Asante, kwenye hiyo mifano miwili hapo kwenye mada ukielekezwa umekosea kwa staili gani ndio utaona haujadharauliwa?
mfano, mtu anakwambia Biden ameshinda uraisi wa marekani ameona facebook. Namrekebisha vipi asione kama namkashifu au kumkosea adabu?
nitaacha mara moja.Hayo ni mambo ya kitoto ndani ya mahusiano/ndoa! Achana nayo mara moja. Wanaume tulio wengi huwa hatupendi aina hiyo ya masihara/utani. Kama ujumbe umeuelewa, unakosoa ili iweje?
Natamani watu wote wangeamini kukosolewa ni njia ya kujifunza. Inasaidia kutokurudia makosa ukihisi upo sahihi.Mimi naona ni sawa kabisa,kuna watu wanatabia ya kujifanya wanajua kitu kumbe hawajui.
Mfano:
Mimi kipindi Niko chuo nilikuwa sijui kutamka neno Monkey nilitamka (monkei) na donkey nilitamka (donkei) hii yote ilitokana na athari za walimu wangu wa shule za msingi enzi hizo,so kuna siku Niko class chuoni nikatamka hivyo infront of the class ,jamaa ambaye ni swahiba wangu wa damu alinirekebisha na wala sikujisikia vibaya,kwakuwa najua Learning is an endless process.
Nikiwa kazini nilipita karibu na shule ya msingi nikakuta mwalimu anawakalilisha wanafunzi neno monkey linatamkwa kama monkei ,uvumilivu ulinishinda.Nikapita pale nikamwita mwalimu na kumwambia abadilishe neno hili halitamkwi hivyo Bali linatamkwa /ˈmʌŋki/,sasa sijui kama alijisikia vibaya au lah.
Pili hata mke wangu huwa ananikosoa pale ninapokosea katika nyanja yoyote ile,inategemea na life style yenu,bati Mimi huwa nakosolewa nawala siwezi kukasilika
Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Asante kwa ushauri.😂😂😂kama ninyi wote ni waswahili kuna haja gani ya kutumia kiingereza mpaka mkosoane, si mtumie tu kiswahili, hayo ya kukosolewa ataenda kukosolewa huko mbele kwa mbele.
NB; jifunze tu kuishi na hao viumbe maana wanajifanyaga wao ni vichwa na kamwe hawawezi kua mkia, ukiona umejaribu kumkosoa hataki wewe achana nae kama jambo halina madhara kwako kama linamadhara na anang'ang'ania na hataki kukosolewa muache aende zake 😎
Nilimwambia "babe lini hiyo, sio kwamba uchaguzi bado?"Kuna mdada wa Tangazo la Tigo , unajua kwann Amekua Gumzo kwa wanaume Tanzania nzima kiasi kwamba hata mimi nmejikuta nasajili Tigo? ....Hofu ya kimakosa ilisahihishwa kwa lugha na mbembelezo wa kimataifa.
Ipo ivi, Siumekaa muda mrefu na mtu wako? Unamjua sana hata uwezo wake wa utambuzi wa mambo mbalimbali ?... Basi kwenye kukosoa hakikisha huvuki uwezo wa kichwa chake, kiasi cha kumfanya ajihisi unamuona Kilazaaaaa.
Kwa mfano.. ilo la Biden..... unaweza mwmbia '(Cheko la mahaba linaloambatana na kumgusa kifuani) Hahaha baby bwanaa izo habari za Facebook usipende kuziamin sanaa , mi mbona nmesikiliza taarifa ya Habari ni kwamba Biden kashinda tiketi yakupeperusha chama chake kwenye uchaguzi mkuu wa Urais nchin mwao ... unaona inavyosound??????
Sio mambo ya "hahahahahahhaa hahahahah umeshinichekesha mweeee aiseee Biden kafanyaje ? Hahahahah Biden ashinde Urais wakati bado hata uchaguzi bado?"..au
Uongo mtupu , Biden ashinde kwa uchaguzi ulofanyika lini???
.na ukute ni mwanamke wa kizaramo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sisi wanaume, Tunatafasiri HESHIMA kama UPENDO .
Hatuna utoto wowote, watu wazima kabisa.kumkosoa mwanaume sio dhambi bwana, ila inaonyesha nyote bado watoto, mkikuwa mtaelewana tu
Hofu yako wewe ni aibu itakayoletwa nayeye??.Nilimwambia "babe lini hiyo, sio kwamba uchaguzi bado?"
akaniambia "upo dunia gani wewe, ameshatangazwa kuwa Rais kabisa".
nikamuuliza "mbona hata BBC Swahili hawajatangaza beb.
Akaniambia '' niamini mimi, hao bbc walikuwa vibaraka wa Trump hawawezi kutangaza."
Nikamwambia "sawa baby wewe umeona wapi"
Akanitumia screenshot ya facebook, ni kweli imeandikwa hivyo lakini na page za uongo.
Akaniuliza "umeamini sasa ?'
Nikamjibu "ndio hongera yake"
Sasa roho inaniuma kiasi kwamba naona ataenda kuongea mbele ya watu kwa ujasiri aonekane kichekesho. Na ningemthibitishia kwa kumwonesha source sahihi angeona namwona kilaza. Na kwa maoni niliyoyapata hapa naona nilifanya uamuzi sahihi wa kuacha aamini hivyo.
Siyo kwamba mimi ni mjuaji .Aahhh , ulishawah kua namtu mjuaji wakila kitu ,mbishi lkn kiuhalisia hajui kitu? Sasa ndio Jamaa wako.Hofu yako wewe ni aibu itakayoletwa nayeye??.
Fanya ivo, yenye umuhimu endelea kua unamrekebisha ila kwa uzuri maana mtu waaina hiyo ukimkosoa kwa kejel atahisi unamwona pumbavu na usisahau ile sense ya "Uanaume" yeye lazima ailinde.
Kwa mambo yasokua na maana kama hayo ya Trump, sijui Biden, mkubaliegee tu ila baadae ndo unamsaidia kwa kumpa vyanzo vya uhakika toka kwengine.
Mwisho.... Usiwe mjuaji sanaaaaaa ukaishia kuboa.
Si unaona wenyewe wanasema hawapendi.Dada hiyo sasa siyo heshima bali ni uoga, anakosolewa Mungu na anatuelewa sembuse mume.
Siyo kwamba mimi ni mjuaji .
Huyu ndugu ana ile kutaka kuonekana tofauti mbele za watu.
Akiwa na mimi haongei kingereza, ila akinikuta na ndugu zangu au wafanyakazi wenzangu yeye ni kingereza mwanzo mwisho. Halafu na lafudhi inakuwa ya kikenya ghafla.
Sasa sijui anataka ku appear kama msomi mbele zao au vipi.
Halafu hizo strory zake za facebook ndio atazigeuza mada kuwapasha mashemeji zake (ndugu zangu).
Sasa mimi sipendi mpenzi wangu kuonekana kichekesho mbele za watu , maana sio siri wananicheka na kumcheka yeye.
Natamani ningepata nafasi ya kukaa naye chini nimfundishe ili sasa akiongea mbele ya ndugu zangu wasiwe wanamcheka au kunicheka mimi.
Nimfundishe pia kuwa taarifa za facebook aachane nazo nyingi huwa sio za kweli, ili akiwa anawapasha habari ziwe za uhakika.
Mwanaume nini???? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mmeshakuwa malaika sasa (mayesu wapya)Mwanaume hakosei sasa huyo mwanamke akosoe nini ?