Sifa kuu za Mwanamke High Class ni hizi!

Sifa kuu za Mwanamke High Class ni hizi!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
38,431
Reaction score
89,063
SIFA KUU ZA MWANAMKE HIGH CLASS NI HIZI!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Ni kawaida kwa vijana wasiokuwa na elimu ya sosholojia na saikolojia kubabaishwa na mikogo, mbwembwe za kila mwanamke wanayemuona mitaani huko.

Pia ni kawaida pia wanawake nao wenyewe kwa wenyewe kutingishana na kurushana roho kwa vitu visivyo na kichwa wala miguu.

Leo Mtibeli ataenda kutoa somo la sifa za mwanamke High Class. Utajuaje kwamba aliyesimama mbele yako au anayepita ni mwanamke wa daraja la juu.

Kupitia andiko hili, vijana wakiume watajifunza kuwatambua High Class woman. Ambapo watafaidika. Pili hawatasumbuliwa na wanawake uchwara wanaojichetua, wenye mikogo mshenzi isiyo na kichwa wala miguu.

Pia, wanawake nao watajifunza namna ya kuwa Wanawake High Class ambapo sio tuu itawasaidia wao kuheshimika bali pia kuwa na tija kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Zifuatazo ni Sifa kuu za Mwanamke High Class;

a) Anaakili na Kujitambua.
Kila mtu unayemuona Ana Akili. Kwa sababu Akili ni tools iliyowekwa kwa kila kiumbe kama ulinzi na nyenzo ya kukifanya kiumbe kiishi.
Ila kwa binadamu Akili ni zaidi ya nyenzo ya kuishi. Kwani Akili ni nyenzo pia ya kulinda utu wa binadamu tofauti na wanyama wengine.
Sasa utajuaje huyo mwanamke anaakili na anajitambua? Kwa uchache;
1. Anajua thamani yake, mfano: hakubali kudharauliwa ili apate kitu fulani au asimpoteze mtu fulani.

2. Anaweka mipaka yake, mfano: anaweza kusema “hapana” bila kujisikia ana hatia. Kitu kama hutaki sema hutaki. Sio unafanya mambo kinafiki.

3. Hajilinganishi na wengine, mfano: hafanyi maamuzi kwa sababu tu marafiki zake wanafanya hivyo. Kisa mwenzako kaolewa nawe unadandia mambo. Kisa mwenzako kanunua Kijora nawe umo. Mwanamke High Class hafuati mikumbo, hajilinganishi. Anaishi maisha yake.

4. Anajua anachotaka maishani, mfano: ana malengo yake ya kazi, biashara, elimu au maisha binafsi. Mwanamke High Class anandoto zake, hategemei mwanaume ila kwake mwanaume ambaye ni mumewe humchukulia kama mwenza wa kutimiza kwa pamoja malengo yao ambayo ni malengo ya familia yao. Hii ni kumaanisha Mwanamke High Class kabla hajaolewa huchagua mwanaume ambaye tupo ndani ya malengo yake. Wanaofanana ndoto. Wenye mitazamo na imani zinazofanana au kuelekeana.


5. Anakubali makosa yake na kujirekebisha, mfano: akigundua amekosea, anaomba msamaha bila kulaumu wengine. Mwanamke yeyote asiyependa kuambiwa ukweli huyo ni lower class. Umepewa mimba kabla ya ndoa ukatelekezwa hukubali ukweli kwamba umekosea. Unajiona ulikuwa sahihi. Unalaumu wanaume utadhani walikubaka.
Mwanamke High Class hukubali makosa yake na hutafuta njia ya kuyarekebisha bila kurudia.

6. Hachagui mahusiano kwa desperation, mfano: yuko tayari kuwa single kuliko kubaki kwenye uhusiano unaomnyang’anya amani na heshima. Sisi Watibeli Amani na Heshima ni mambo muhimu sana kwetu.
Mwanamke High Class haingii kwenye mahusiano kwa shinikizo. Sijui umri unaenda. Acha uende.
Anajua nini anataka, mwanaume yupi anamtaka.

2. MSAFI NA KUJITUNZA;
Anatunza mwili, mavazi, nywele, harufu na mwonekano wake kwa heshima. Si lazima awe na vitu vya gharama cha muhimu ni kuwa msafi, nadhifu na mwenye presentation nzuri.
Usafi wa Mwili unahusu pia hageuzi mwili wake kama dampo la wanaume kumwaga takataka zao. Yeye sio dampo. Mwanamke High Class anakinyaa. Hawezi kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja. Hawezi ku-share vitu vyake vya faragha kama sex, mswaki, kijiko, chupi, n.k. kwa sababu ni msafi.

Mwanamke High Class huwezi mkuta anachambana, anamaneno machafu ya hovyohovyo. Anajua yeye anathamani kubwa.

3. Tabia njema na Adabu.
Ana adabu, utu na uwezo mzuri wa kuwasiliana
Anajua kuzungumza kwa heshima bila kuwa mnyonge. Anaweza kutofautiana na mtu bila matusi, drama au kumdhalilisha mwingine. Tabia yake huonekana hata pale ambapo hakuna anayemwangalia.

Mwanamke High Class utamgundua anapoingiliana na wale aliowazidi, waliochini yake. Vile anavyowachukulia, anavyoongea nao. Hatumii uzuri, elimu, cheo chake kuwadharau waliochini yake.

4. Anajua Umuhimu wa Familia.
Mwanamke High Class anajua umuhimu wa kuanzisha famili yake. Kuwa Mke na kuwa Mama.
Kama mwanamke anajua thamani ya kuwa mke na mama bora katika familia yake.

5. Lazima ajitegemee.
Mwanamke High Class lazima aweze kumudu mahitaji yake ya msingi kama chakula, mvazi, malazi, mawasiliano na mahusiano(sex yenye maadili)

Kujitegemea ni kuwa na kitu chako mwenyewe. Uwezo wa kujimudu. Kujitegemea kimwili, kiakili, kihisia na kiroho.
Lakini kujitegemea huko hakumfanyi adharau wasioweza kujitegemea.

6. NI KIONGOZI KATIKA JINSIA YA KIKE.
Mwanamke High Class anajijua yeye ni mwanamke. Na lazima ajionyeshe na kuishi kama mwanamke. Kwa heshima na thamani.
Awe na uwezo wa kuiongoza familia yake kama Mke na kama Mama.
Ajue yeye ni mke ambaye ni upande wa pili wa sarafu kwa mwanaume.

Amshauri mumewe kwa uadilifu, kwa heshima, na upendo.
Asitumie uanamke wake kama udhaifu. Bali nyenzo ya kufanikisha malengo ya familia, jamii na taifa lake.

7. Ni Role model wa wasichana wadogo.
Mwanamke High Class anajua kwamba yeye ni kama kioo cha jamii kwa mabinti waliochini yake.
Lazima awe mfano wa matendo mema. Kiasi kwamba watoto wakimuona wanasema huyu ndiye mwanamke ninayetamani angekuwa mama yangu.
Huyu ndiye mwanamke ambaye nikiwa mkubwa natamani kumuoa.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hapana!
Sio pesa kwa maana ya utajjiri.
Mwanamke yeyote mwanataaluma anauwezo wa kuwa high class woman
Hata mimi sijazungumzia utajiri wa kwenda kula bata dubai kila mwezi. Naongelea hizi pesa za mboga, ukipata tatizo linalohitaji milioni ya haraka huhangaiki kumpigia sijui kaka, mjomba
 
Back
Top Bottom