Ni nini kipaumbele cha serikali chini ya Rais Samia na CCM kwenye Sekta ya Elimu?

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
810
1,652
▶️Ni kweli kabisa kuwa, katika Sekta ya Elimu serikali imeelekeza nguvu kubwa sana kwenye ujenzi wa madarasa katika Elimu msingi na Sekondari na vyuo vya kati na kuyaacha au kusahau maeneo mengine muhimu ktk Sekta hii ambayo kiuhalisia ndiyo yanayobadilisha mindset ya mwanafunzi ktk tendo la kujifunzia.

▶️Kusema hivi Sina maana ya kwamba majengo yaitwayo shule si muhimu. Ni ya muhimu Kwa nje lakini Kwa jamii yenye rasrimali fedha chache inapaswa kuwa makini ktk kupanga vipaumbele vyake vya kisekta..

▶️Na ndipo tunapoweza kujiuliza swali hili, kwamba, ni kipi kinapaswa kuanza kwanza kushughulikiwa Kwa ufanisi na ukamilifu wake katika sekta ya elimu kati ya haya katika mchakato mzima wa kujifunza na ufundishaji?

✓ Uwepo wa walimu wa kutosha na wenye ujuzi wa kutosha kufundisha..?

AU

✓ Uwepo wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia mfano vitabu nk nk?

▶️Kuna shule kadhaa ktk baadhi ya majimbo ya uchaguzi ktk mikoa yote Tanzania ambazo serikali imeanza kuzijenga mwaka jana 2022 kwa ufadhili wa 100% fedha za serikali.

▶️Hizi shule zimepewa wanafunzi wa kidato Cha kwanza mwaka huu 2023 japo ujenzi wake haujakamilika Kwa sababu inasemekana fedha zake zilishapigwa na wajanja.

▶️Utafiti wetu unaonesha kuwa, licha ya ujenzi wake kutokamilika, vilevile hazina vifaa vya kufundishia na kujifunzia Kwa maana ya vitabu nk nk

▶️Aidha hata shule nyingi za zamani msingi, sekondari na vyuo kwa sasa zina upungufu mkubwa wa walimu na serikali haijali kufanya lolote huku walimu maelfu wenye taaluma wakiwa mitaani tu wakifanya shughuli zingine na wengine wakiwa hawana kazi yoyote ya kufanya.

⌨️Ndiyo nauliza, ni vipi vipaumbele vya serikali ya Samia na CCM kwenye Sekta hii muhimu Kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi?
 
Back
Top Bottom