Hii stage nimewahi ipitia mara mbili
First time(in my late teens)
Aisee huyu mdada alikuwa family friend, tumekua wote, tumesoma wote. Tulianza ku date kipindi fulani, Aisee huyu mbwa aliniendesha. Nilimpenda kupitiliza, akaamua kuninyoosha. Nimewahi kumlilia usiku kucha, nampigia simu huku nalia😂😂. Aliniambia nisubiri mpaka ndoa na nilikubali kwa roho nyeupe(nikikumbuka huwa najicheka aisee😂😂)
Second time( mid twenties)
Hapa nilipigwa pesa za kutosha, kuna mwanangu alikuwa ananishauri sana kuhusu hiyo manzi lkn ilikuwa kazi bure.
Kuna kipindi nilisafiri zaidi ya km 1000 kwenda kumuona. Nilivofika nikachukua chumba cha 80k, aisee tulilala usiku mzima na sikupewa chochote( ata kiss nilinyimwa😂😂). Niliendelea kumpenda pamoja na kunifanyia vile na pesa akiomba anapata.
Siku hz nipo emotionless. Naamini love is a choice not feelings and emotions