Curtis De Mi Amor
Senior Member
- Jan 9, 2022
- 134
- 498
Za asubuhi wapendwa, hope nyote mu wazima wa afya, na kwa wale wagonjwa Mwenyenzi Mungu awafanyie wepesi.
Hapa mtaani kuna mama amerehemika, huyo mama ameacha mume na watoto 3. Mali zote alizokuwa nazo huyo mama kawarithisha wanawe, yaani mume mtu kaambulia pangu pakavu.
Kumetokea mvutano wa nani ndio anapaswa kusimamia hiyo mirathi, huku baba mtu akisema ni juhudi zake mpaka hizo mali zimepatikana na watoto wakisema ni haki yao kutoka kwa mama yao.
NB: Huyo mzee alianza mechi 2-0 na akafanikiwa kuchomoa 1 tu. Hivyo mpaka umauti unamfika huyo mama mechi iliisha 2-1.
Sasa swali langu ni kwanini wanandoa kwa asilimia kubwa mmoja wapo anapokuwa amefariki basi mirathi hupewa watoto au mtoto na sio mwenza wake ambaye amebaki yaani walichuma wote?