Ni muda wa kanisa katoliki kuongozwa na waafrika wanaoongoza kwa waumini na imani kuliko wazungu wanaozidi kutoamini Mungu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Dini imebakizwa kwajili yetu waafrika yafaa viongozi wake wawe waafrika.

Huko kwa wazungu wengi wamezikimbia dini, kanisani kwenda huwa ni wazee, hata rais anaenda mara moja moja matukio maalum sio kama huku Afrika karibu kila mwezi lazima rais aende, vijana nao utawakuta na biblia mikononi siku ya jumapili, hali ni tofauti sana kwa wazungu ambao kwa vijana kanisani ni kwenye kuoana na kuzikana pekee

Wazungu kwa sasa hali ya maisha yao inaafikiana na maagizo ya Mungu na yeyote anaediriki kupinga mtindo wa maisha yao anaonekana muovu huko nchi zao, mfano mashoga na wasagaji na watu wanaobadili jinsia wanalindwa mnooo, yani ukidiriki kuwakashifu waweza onekana zaidi ya gaidi, mambo ya sex education yanaruhusiwa hata kwa watoto ikiwemo kuwafundisha kujiridhisha kwa mikono, watoto wana maamuzi ya kuamua kubadili jinsia na ole wako mzazi umpinge, mzazi huruhusiwi kumchapa mwanao hata kwa kanga.

Nachoona hii dini kwa wenzetu ishaingizwa zaidi na utamaduni wao, na ndio maana hata papa huwa anaogopa kuzungumzia mambo flani ama nae tayari yumo humo anatetea.

Ilianza kidogo kidogo papa anakaa meza moja na wanaume wanaoingiliana wanaotaka kuwa wakristo huku bila kuacha hio tabia ya kupekechana wanaume kwa wanaume, Panya ukimpa siagi atahitaji na maziwa !! leo hii ni ruksa kwa wanaume wanaoingiliana kingono kunatizwa na kuwa wazazi watakatifu, kifuatacho ni wao kudai haki za kupewa nafasi za uongozi waingize zaidi mambo yao kwa kizazi kibichi cha kuanzia 2010, mambo haya yote hatuwezi kumlaumu papa pekee bali ni mfumo wa maisha ya wazungu ambao wengi walishaachana na mambo ya dini ila dini imebaki kupush ajenda za utamaduni wao duniani, waathirika wakubwa wanakuwa waafrika ambao wapo mstari wa mbele kwenye kufuata misingi ya dini ya kikatoliki.

Ni wakati sasa wa dini hii iongozwe na sisi waafrika tunaoiwekea bidii zaidi
 
Kwanini tuongoze dini za kufikia kwani zetu zina shida gani? Zina mapungufu gani?
Bado naona dini zetu ni bora na imara zaidi mara 1000 kuliko hizo dini zingine
15d15ba1-2926-4e71-8e17-a2116f7d271b.jpg
 
2. Hao mashoga, wasagaji na wanaobadili jinsia kama wanamchukiza Mungu sana, mbona anaruhusu uwepo wao?
hata majambazi ruksa kwenda makanisani lakini wanaenda kwa nia ya kubadilika hawaingii na mapanga, Wazinzi ruksa kuingia kanisani lakini wanaenda kwa nia ya kubadilika wanayaacha mavumbi ya kongo, sasa shoga iweje aingie kavaa kishoga.
 
hujajibu swali, nimeuliza, kama Mungu anachukizwa na mashoga kwanini anaruhusu uwepo wao? uwezo wa kuwaondoa si anao?
Hawezi kuwaondoa, anawapa nafasi ya mwisho wajirekebishe,Makanisani ni sehemu ya watu wenye dhambi waende kukutana na wokovu, ukiwa msafi na ukijiona huna dhambi baki kwako.

Sijui kuhusu msikitini kama ni wasafi pekee ndio wanakwenda.

YESU alikuja kwaajili ya wenye dhambi, alimuita mwanamke kahaba na akasema ambaye hajazini awe wa kwanza kurusha jiwe{maustaadhi walitawanyika wote], aliishi na Fisadi wa TRAya kipindi hicho zakayo-mtoza ushuru.
 
Hawezi kuwaondoa, anawapa nafasi ya mwisho wajirekebishe,Makanisani ni sehemu ya watu wenye dhambi waende kukutana na wokovu, ukiwa msafi na ukijiona huna dhambi baki kwako.
Sijui kuhusu msikitini kama ni wasafi pekee ndio wanakwenda.
YESU alikuja kwaajili ya wenye dhambi.
Hatuelewani, turudi nyuma kidogo, nini kinasababisha ushoga?
 
Hatuelewani, turudi nyuma kidogo, nini kinasababisha ushoga?
Mambo ya Kibiolojia:Utafiti unapendekeza kwamba kunaweza kuwa na sababu za kibayolojia zinazoathiri mwelekeo wa ngono. Baadhi ya tafiti zimegundua athari za kijeni na homoni kwenye mwelekeo wa ngono, lakini hakuna "jini la mashoga" maalum ambalo limetambuliwa.

Athari za Homoni: Athari za homoni kabla ya kuzaa wakati wa ukuaji wa fetasi zimedhaniwa kuwa na jukumu katika mwelekeo wa ngono. Hata hivyo, taratibu sahihi hazieleweki kikamilifu.

Sababu za Kinasaba:Ingawa kuna uthibitisho kwamba chembe za urithi zinaweza kuchangia mwelekeo wa ngono, kuna uwezekano kwamba mchanganyiko wa mambo ya kijeni, homoni, na mazingira unahusika. Ni mwingiliano changamano badala ya kipengele kimoja cha kubainisha.

:Sababu za kijamii na mazingira pia zinaweza kuwa na jukumu. Watafiti wengine wanapendekeza kwamba uzoefu wa utotoni, mienendo ya familia, na mazingira ya kijamii yanaweza kuchangia ukuzaji wa mwelekeo wa ngono. Walakini, mambo haya hayazingatiwi kuwa ya kuamua.

Utambulisho Usiochaguliwa:Muhimu zaidi, maoni yaliyopo kati ya mashirika makubwa ya matibabu na afya ya akili ni kwamba mwelekeo wa ngono sio chaguo. Watu binafsi hawachagui kuwa mashoga, wasagaji, wapenzi wa jinsia mbili au wa jinsia tofauti. Ni kipengele cha msingi cha utambulisho wao.

Utofauti wa Uzoefu: Ni muhimu kutambua utofauti wa uzoefu ndani ya jumuiya ya LGBTQ+. Hakuna simulizi moja, na uzoefu wa mtu binafsi wa kuelewa mwelekeo wa kijinsia unaweza kutofautiana sana.

Kwa hapa Tanzania, tumejikita kwenye sababu za kijamii na mazingira, mfano mtoto anaanza kupigwa miti akiwa shule, au hawa bongo fleva anapigwa miti ili apate hela za kurekodi, na baadae anaendelea na mchezo mpaka anzoea na yeye anakuwa anapiga miti wenzake.
 
Back
Top Bottom