SoC02 Ni mpango kazi wa miaka 100-50

Stories of Change - 2022 Competition

Lenin23

Senior Member
Feb 9, 2022
138
218
Ati tujifunze Kwa Kiswahili masomo ya sekondari, icho Kiswahili chenyewe mnakijua? au mnataka kuzalisha kizazi cha lomolomo? Je, kwani tumesahau visa na Mikasa ya vijana wadogo maarufu kama panya road? Kwa idadi wapo wangapi au tunahitaji wangapi zaidi Ili kujua kua swala la ajira ni changamoto?

Mnataka kuzalisha ongezeko la vijana walevi? au wavutaji wa unga kwa idadi ambayo haijawai tokea? Leo hi mnataka masomo ya Fizikia na Hisabati ati katika levo ya Sekondari mfundishe kwa Kiswahili halafu hizo Kazi wakafanyie wapi?

Nilisikitishwa na kushangazwa sana kuona hata wasomi wenye elimu ya juu wakisapoti masomo ya Sekondari yafundishwe Kwa Kiswahili bila mpango wowote au mkakati wowote ule ati kwa kisingizio kwamba ufaulu utaongezeka Kweli? Kwani lengo la elimu ni nini jamani, kwani tunataka kutokomeza ujinga na kuwapa Watu maarifa yatakayowaonyesha fursa zilizopo popote duniani au tunataka ufaulu uongezeke? Hakuna radhi yoyote tutakayotoa itakayokeleweka.

Ati kwasababu nchi zilizoendelea kiuchumi Kama Ujerumani, China , Uingereza na nyinginge nyingi wanatumia lugha zao basi kizazi cha wasomi wachache ambao ni wavivu Tanzania na wao wanataka Kiswahili ni huzuni sana kwakweli? Je, mmewahi kuuliza ni kwanini nchi nyingine hutumia lugha yao wenyewe au sie tunataka fuata mkondo ingelikuwa kina na urefu wa maji hatujui kwani siye dira yetu ni ipi , dira yetu na mpango kazi wetu wa miaka hamsini Au Mia ijayo ni upi , nawaachia WanaJF uwanja mnisaidie

Haya ni madhara yatakayotoea baada ya Kiswahili kupitishwa kama lugha ya kufundishia level za sekondari na wataoumia ni watoto wa masikini na wazazi wenye hali duni

Kutakuwa na wimbi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira, yaani mpaka sasa hali ni mbaya na Kila mwaka vijana wanamaliza vyuo na kuja mtaani yaani navowasilisha hii meseji tayari kuna wimbi la vijana wengine tayari wapo mtaani waliomaliza vyuo mwezi hu wa Julai

Serikali haina uwezo wa kuwaajili wote kimbilio ni mashirika yasiyo ya Kiserikali (yaani private sectors) na mengi ni ya wawekezaji toka nje ambao wengi lugha yao ni Kiingereza Naam , Je hamuoni tatizo hapo ? nawachia Wana Jf wanasaidie ,

Tukija katika soko la kidunia, lugha ya kingereza ndio lugha yenye soko nikiwa namaana ya kwamba wapo vijana wengi watanzania ambayo wanafanya Kazi nje ya chi na wengi waliweza fanikiwa kupata hizo nafasi kwasababu ya kigezo kimoja ( lugha ya kingereza) yaani masomo yao ya sekondari na shahada zao na stashada walizipata Kwa lugha ya kingereza Kwa maana nyinginge isingekua hivyo ingewabidi kufanya mitihani kama IELTS, GMAT nk ambazo Ada ni dola 250 Sawa na laki sita kasoro ya kitanzania je wazazi wetu waloshindwa kutulipia ada ya shilingi 10000 sekondari wangeweza? Nawachia Wana Jf wanisaidie pia usisahau kua hiyo mitihani sio rahisi mtu aliesoma kiswahili tu hawezi kuifaulu ,sababu waliosoma Kwa kingereza tu wanashindwa tuamke tuwe macho watanzania.

Tutazipa soko shule binafsi ( yaani private schools). Sio vibaya shule binafsi kuwa na soko ila nina maana kua Kama Kiswahili kitapitishwa kua lugha ya kujifunzia masomo yote watakao soma shule za serikali ni watoto wa wazazi wenye Khali duni , wazazi wengi watakimbilia kuwapeleka watoto wao shule binafsi ( yaani private schools) Kama nilivoainisha apo mwanzo ajira Kwa watakaokua wamesoma kiswahili tu zitakua ngumu zaidi Kwa mashirika ya watu binafsi ( private sectors) na ajira za selikali ni chache je tunataka kutengeneza kitu Gani nawachia wanazuoni mnisaidie kujibu!

Soko la wasomi kidunia litapungua yaani wale Watanzania wachache wanaopata bahati ya kwenda kusoma nje masomo Kama udaktari na mengine, kingereza ni nyenzo muhimu sana katika hiyo sekta , tukitaka Kiswahili kitumike Kama lugha ya kufundishia tutajiwekea ukizanzani katika kupata wasomi wanaotoka katika familia duni kupata bahati ya kwenda kupata ujuzi wa masomo kutoka Kwa wataalamu wa nje ambao wameendelea tayari , je ni lini Tanzania yetu itaweza kutengeneza ndege , kutengeneza meli, na miundo mbinu kibao ambayo bado tunategemea wasomi kutoka nje watutengenezee kwanini tusiweke mpango Kazi na sheria zitakazosomesha Watu katika sekta izo na badala yake tunang'ang'ania Kiswahili , je tukianza kukitumia kitatokea nn? lini tutatengeneza treni, meli na ndege zetu wenyewe nawachia Wana JF mnisaidie kujibu? Kwa kiswahili chetu bila mpango Kazi tutatoboa?

Kutakuwa na uhitaji mkubwa wa watafasiri wa lugha Yani wakarimani ? badala ya Serikali kuweka bajeti ya elimu Bure vyuoni italazimika kuweka mpango wa bajeti ya kuwaajili wakalimani Karibia Kila sekta ya serikali je hi ndo dira ya maendeleo yetu? hiki ndicho tunahitaji Kwa taifa letu?

Kuna msemo wa lugha ya kigeni unasema success is like leap of faith maana yake mafanikio ni kama jaribio la kiimani kuzifikia nyota nilazima unyoshe mkono wako kuzifikia mbingu, hakika ni swala zuri sana na la kujivunia lugha yetu lakini hatuwezi kufanya jambo Kwa kushitukiza, Jambo hili liundiwe dira ya miaka hamsini Au Mia Moja Ili kuweka misingi mikubwa ya uchumi wa viwanda ,elimu ya mitandao Kwa masoko ya kifedha yaani ( financial markets ,stocks and foreign exchange) Ili vijana waweze kujifunza na kujipatia kipato ,elimu ya viwanda Ili vijana waweze kuanzisha viwanda na kuajiliwa viwandani lakini Katika upande wa elimu ya kimitandao lugha inayotawala ni ya kingereza na wanaofanikiwa na kuwa mahili ni vijana wenye uelewa mzuri wa maswala ya lugha ya kingereza. Tumekuwa na wezi wengi sana wa mitandao ,na tukitumia lugha yetu tutaongeza jopo lingine tena Kwa kasi zaidi ya ilivyo Sasa, tukitaka wawekezaji waje wawekeze tena Kwa kutumia kiswahili chini ya sheria itakayowalazimisha wawekezaji kujua lu gha ya kiswahili ni lazima tuweke misingi mikubwa Katika sekta ya viwanda na uchumi

Itoshe kusema mawazo yangu sio sheria yanaweza kuvunjwa, kupingwa kuungwa mkono au kutupiliwa Mbali

Naomba usiache kunipigia kura kwa mawazo hayo machache Ili niweze kuibuka mshindi wa kitita
Mimi ni jitu lenye akili,

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom