Elimu Yetu na Lugha

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,578
7,281
Mengi yamesemwa kuhusu nini kinarudisha elimu yetu nyuma. Ukweli ni kuwa lugha inamchango mkubwa kwani ndio msingi wa mawasiliano. Kwa hapa kwetu kuna lugha tatu za msingi: kingereza, kiswahili na hesabu/hisabati. Sisi wengi wetu ni wabovu katika hayo pamoja na kiswahili.
Kingereza ni lugha ya kufundishia kwa mfumo wetu, pia ni lugha ya mawasiliano ya kimataifa na ndio maana wenzetu wengi huhakikisha vijana wao wanajifunza hii lugha. Ukitaka kujiendeleza kimasomo baada f4 utapata shida kama kingereza hakipandi.
Kiswahili kwa ujumla hakina msamiati wa kutosha kwenye masomo ya juu hata kama kuna wanaotaka kutuaminisha kuwa tunaweza kukitumia kufundishia hadi chuo kikuu. Ni ndoto nzuri lakini itahitaji uwekezaji mkubwa wa kujenga misamiati kwa kila somo , kupata walimu wabobezi wa hayo masomo kwa kiswahili na kutengeneza miundombinu kama vitabu, vijarida etc. Katika mijadala mingi hili la uwekezaji huwa silisikii.
Hisabati ni lugha muhimu ya biashara, uchumi na sayansi na jinsi unavyo kwenda juu ki elimu unagundua umuhimu wake.
Kwa masomo yote hayo tutahitaji walimu mahiri na hii itadai uwekezaji bila hilo tutaendelea kudanganyana. Kama tumeweza sgr, bwawa la umeme na kufufua atcl naamini tuna weza kuwekeza kwenye hizi lugha.
 
Back
Top Bottom