Ni mbinu gani zinatumika kutega abiria wa taxi mtandaoni (Bolt, Uber, Faras)?

African Geek

JF-Expert Member
Jul 29, 2022
778
1,353
Wakuu, habari za muda huu. Ningeomba kujuzwa na wataalamu wa hizi kazi za taxi mtandaoni, namna gani ya kupata abiria wengi. Mimi ni mgeni kwenye hizi kazi na ningependa kupata walau abiria 10 kwa siku.

Je, nifanye kazi muda gani, siku gani na maeneo gani ili niweze kunasa abiria kwa urahisi. Mimi ni mkazi wa Dar es salaam. Kwa sasa natumia Faras Captain, ila nimelenga kujiunga Bolt na Uber baada ya wiki chache.

Natanguliza shukrani.
 
1. Muda mzuri ni rush hours especially jioni kuanzia saa 10 hadi 2 usiku.
2. Weekend ndio nzuri zaidi kuanzia saa 8 mchana watu wanatoka out as family. Pia kuanzia saa 1 usiku either watu wanarudi mfano kutoka sehemu za mapumziko kwenda home. Na pia watu wanaenda out mfano bar clubs etc.
3. Maeneo ya ushuani mfano Mikocheni, Upanga, Masaki, Mbezi ushuani etc ndio watu wanatoka na maeneo yenye business centres kubwa mfano Mlimani City, Shoppers Plaza, Kariakoo etc.
4. Maeneo yenye huduma za kijamii kama stendi ya mabasi, hospital, beach, uwanja wa Taifa, etc haukosi.

Kwa ufupi hii kazi haina perfect spot. Ndio maana wengi wanaifanya kama part time job. Unaweza pata mteja ukamtoa Magufuli Bus Stand ukampeleka Chanika, ukapata Elfu 30. Hafu ukarudi Chanika hadi kijiweni kwako Ubungo mfano bure. Imagine.
 
Asante sana mkuu. Haya ni madini niliyokua nayatafuta
 
Back
Top Bottom