Njoo uifahamu Taxi Mtandao BOLT/UBER

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,668
12,240
Ndugu zangu mnaopambana na maisha Leo nawaletea fursa Kwa vijana wanawake na wanaume ambao mna Leseni ya udereva mnaweza kuendesha gari/pikipiki.

PIKIPIKI ni ajira acheni maneno ya Lema aliesema kuwa bodaboda sijui ni LAANA. Mimi niwaondoe hofu kuwa bodaboda ni ajira kana ajira nyinginezo.

Kwa ambao mnazo pikipiki zenu fungueni mitandao ya Tax mtandao ambayo ni Bolt/Uber japo Kwa sasa IPO mitandao mingi mingine kama FARASI ama Indrive, lakini Mimi nawashauri Kwa mnao Anza mtumie sana BOLT ndio yenye matokeo mazuri Kwa hapa dar es salaam.

Bolt inalipa asikwambie mtu japo safari zake zinaonekana ni za bei ya chini lakini amini usiamini bei hiyo hiyo ya chini Kuna mtu analaza Hadi elfu 50 Kwa siku siku.

Na ukikomaa bila kuchoka ukafanya kazi Kwa muda mrefu Zaidi ya masaa 12 Kwa siku utapata pesa na utayaona maisha mepesi.

Screenshot_20230417-172746.jpg


Mitandao ya Tax mtandao ya Bolt na Uber haitumiwi bure ni lazima uilipie ili uweze kuzidi kupata wateja. Bolt ukifikisha deni la shilingi elfu 15,000/= hutopata abiria Hadi ulipie.​

Screenshot_20230624-082952.jpg

Mimi sijaanza kuitumia muda mrefu lakini Kwa kiasi Fulani ninaishukuru sana hii mitandao... Haswa bolt manaa huo wa Uber kwakweli kwangu haifanyi vizuri kabisa, Ila bolt muda mwingine naweza kupata Hadi elfu 50 Kwa siku na hapo Huwa naifanya Kwa muda mchache sijawahi kufanya masaa Zaidi ya manne. Japo wenyewe ukifanya masaa 12 mfululizo wanakupa mapumziko ya lazima, japo Kuna ujanja wa kufanya ili ufanye kazi Hadi masaa 18 Zaidi Kwa siku.​

Screenshot_20230419-200253.jpg


nilishawahi kuomba ushauri humu ndani kuwa maisha kwangu yamekuwa magumu kazi hailipi ila namshukuru Mungu kwasasa kula na kulala uhakika kupitia Bolt na Uber...

Usisahau kuwa hii mitandao ili upate abiria ni lazima ulipie na Kwa bolt ukifikisha deni la shilingi elfu 15 hupati abiria...​

Screenshot_20230531-081334.jpg

Ila ili upate pesa ni lazima ujue ni sehemu gani zenye uhitaji wa abiria, Kwa jiji la dar es salaam kariakoo, posta, sinza, masaki, na mwenge Bolt inafanya vizuri sana.

Kwa mtandao wa bolt unatakiwa kuzitunza sana point zako za udereva maana hizo point ndio zitakazo kufanya upewe kipaumbele pindi mteja atakapo kuwa anahitaji usafiri...Kwa kawaida ukijiunga Kwa mara ya kwanza na bolt unapewa score 100.

Screenshot_20230624-093214.jpg


Lakini matumizi mabaya ya huo mtandao yanaweza yakasababisha ukapunguziwa points zako na hiyo inaweza ikakufanya ukafungiwa au ukawa hupewi kipaumbele Cha kupata abiria hivyo utajikuta unapata wateja wachache...

Screenshot_20230419-090058.jpg

Picha hapo juu inaonyesha dereva Ambae score zake Ilikuwa zinashuka kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo...
✓kukatisha safari kabla ya kufika...
✓kukataa baadhi ya request
✓chombo kuwa kibovu hivyo abilia aliweka feedback mbaya
N.k
Malipo yapo mazuri hapo chini nitawaonyesha jinsi dereva anavyo ingiza mapato yake Kwa wiki ama Kwa mwezi...
Screenshot_20230624-093941.jpg
hapo utaona kuwa maingizo yalikuwa ni 508500/= lakini baada ya bolt kuchukua chao dereva anabakiwa na 392911/= ikumbukwe kuwa huyu dereva anafanya hii kazi kama part-time job Kwa masaa yasio zidi manne TU Kwa siku. Kwa hiyo ndugu zangu mnao tafuta maisha msiogope kujiunga na Uber/bolt Kwa hapa mjini inalipa...ila unaweza ukafanya kama full-time
Job....ukapata malipo Zaidi ya hayo.
IMG_20230406_101539_180.jpg

Kwa ambao hamna piki piki na mnatamani sana kuanza hii kazi Kwa sasa Kuna kampuni nyingi hapa dar es salaam zinazokopesha pikipiki na hazina masharti magumu...Kuna kampuni inaitwa WATU IPO pale MWENGE mpakani, wao wanatoa PIKIPIKI mpya kabisa Kwa kianzio Cha shilingi laki nne TU Kwa boxer.. au laki tatu TU Kwa Tvs au Hero... Baada ya hapo utakuwa unawalipa kulingana na mtakavyo kubaliana...NAMBA ZAO NI 0745599611 au unaweza ukapiga namba yao ya bure kabisa 0800750228
Screenshot_20230624-095032.jpg
nakaribisha maswali juu ya hii mitandao ya UBER na Bolt
Screenshot_20230704-060922.jpg

Angalizo ni marufuku kumpa mtu mwingine atumie account Yako ya mitandao hii ya Taxi Mtandao kama Bolt na Uber...wakikubaini akaunti Yako inafungwa hapo hapo
Screenshot_20230710-183210.jpg

Kama umeamua kuwa Uber ukianza kuchagua request nakwambia utapata tabu sana. Ukianza kutopata request mnaanza makasiriko kumbe tatizo ni wewe.

Uber wanavyokupa request afu unazikataa unazidi kujiweka kwenye nafasi mbaya, kama unakataa request bhasi uwe na sababu maalumu mfano labda usiku umepata request mteja anakwenda Mbagala Rangi 3 ndani ndani huko sasa hutaki kwenda huko.

Unaweza kucancel ile request afu ukaandika “Nimewasiliana na mteja, nikamwambia nitamuacha Rangi 3 stand sababu ya usalama wangu, lakini amegoma”. Hapo hata Uber watakuelewa sio una cancel afu unanyamaza tu itawacost sana.

Wengi mnataka request za kwenda Posta, Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach, Kariakoo, Mliman city, Sinza nknk.

Jitahidi sana uwe na rating za juu pamoja na recommendation nzuri kutoka kwa wateja kitakufanya upate request nyingi.

Screenshot_20230717-061214.jpg

Ubao wa Uber huo...japo sikuwa seriously sana ndani ya siku 4 nikawa nime make 91,100/= kama inavyoonekana.

Bolt inapesa ila bila kuwapiga hautoboi hata kidogo na chombo kinachoka kwa haraka maana engine inapiga kazi bila kupumzika.

Kwa kawaida mafuta na commission huwa zinalamba 50% ya mapato. Mfano ukifanya kazi ubao ukasoma 100k, ujue hapo bolt wanalamba 24k, mafuta yanalamba 26k unabaki na 50k. Hapo inabidi itoe pesa ya kula, umlipe boss kama chombo ni cha hesabu na usave pesa ya service bila kuwasahau matrafic. Unaweza kujikuta home unafika na 20k tu.

Ili uione pesa lazima ujitahidi kutengeneza wateja nje ya mtandao. Hawa wateja wa nje ya mtandao wanafaida 2. Kwanza hukatwi commission pili nauli zao huwa ziko juu tofauti na mtandao hivyo unasave wese . So kwa pikipiki ukiweza kutengeneza 20-30k nje ya mtandao basi unauhakika wa kurudi home na 50k. Ila ukirudi na 50k huo uchovu wake usipime na unakuwa umeupuyanga mji vibaya mno.​
 
Gharama ya kujiunga bolt ni koasi gani?
Kujiunga ni bure bure kabisa unatakiwa uwe na
✓LESENI ya udereva yenye Madaraja ya pikipiki kama unataka kuendesha piki piki au c1 kama unataka kuendesha tax
✓chombo chako kiwe na Leseni ya usafirishaji abiria inayotolewa na Latra
✓uwe na bima yoyote hata Third party
✓chombo chako kiwe na usajiri wa biashara
 
Kujiunga ni bure bure kabisa unatakiwa uwe na
✓LESENI ya udereva yenye Madaraja ya pikipiki kama unataka kuendesha piki piki au c1 kama unataka kuendesha tax
✓chombo chako kiwe na Leseni ya usafirishaji abiria inayotolewa na Latra
✓uwe na bima yoyote hata Third party
✓chombo chako kiwe na usajiri wa biashara
Aisee kumbe simple tuu. Wacha nitumie hii boda yangu kuoata japo kitu
 
Back
Top Bottom