Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,504
- 86,054
Tumetoka Dar Shekilango saa 11 alfajiri na Bus la Kampuni ya New Force No. T 236 EBK kuelekea Mbeya. Tumefika Msolwa tumesimamishwa na askari kuwa Kuna msafara wa makamu wa raisi. Tumesimama hadi saa mbili na dakika kadhaa.
Tumeondoka muda magari yakawa mengi, malori, mabasi na magari binafsi. Kuna kipande kuna lory lilikua bovu hivyo mabasi na magari mengine yakatanua, baada ya muda gari zote zikawa haziendi kwa sababu ya mizani pale.
Akaja RTO akamfuata dereva WA bus husika na kumuamuru ahame Site Yake akakae opposite Site ili wayanasue pale, dereva alitii lakini alivyoweka bus upande ule, akaamuriwa Tena aliingize kwenye uchochoro ambao ulikua umejaa tope na kwa ukubwa wa Bus kuliingiza pale lingezama na tusingeweza kutoka Tena.
Dereva akamweleza na kumuelewesha ila yule Askari wa hovyo akamkazia jamaa, jamaa akagoma! Akamwambie TUTAONA.
Tukaruhusiwa kuondoka, tumefika Msamvu saa nne dakika 38 jamaa amekamatwa amewekwa lock-up.
Tunaendelea na safari na Dereva mmoja, sasa hapa ndio najiuliza kama kweli askari wetu wanatumia busara au lah.
Yaani unamuweka Driver lockup then uruhusu basi liendelee na safari na driver mmoja, huyu akichoka au akipata dharura, risk inakua kubwa kwa roho za watu.
Waliosema mabasi yawe na madereva wawili walikua na akili.