Katika pita pita yangu mahakamani, pamoja na sheria kurekebishwa bado nimegundua matumizi ya lugha ya Kingereza katika kutoa hukumu za wananchi yanaendelea kama kawaida huku lugha ya Kiswahili ikipuuzwa!!
wananchi wengi wanashangazwa sana na kinachoendelea bila kujua nini kinaendelea, maswali mengi wanajiuliza, je, dhamira iliyo kusudiwa na Bunge kwa kubadilisha sheria imepuuzwa!!
Je mahakama zetu haswa mahakama za wilaya, mikoa hadi mahakama kuu kwa nini hazitilii mkazo matumizi ya lugha ya kiswahili? Haki wanazo zitoa ni za watanzania au wazungu?
Je, ni kweli kuwa wizara ya katiba pamoja na mamlaka zingine zimeshindwa kutafasiri sheria mbalimbali kutoka kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili?
Uzito unatoka wapi?! uzito wa jambo hili uko wapi? wananchi wanahitaji ufafanuzi, sio kukaa kimya na kuwapuuza.
Waziri wa Katiba na Sheria halioni hili?
Tunaomba ufafanuzi maana wananchi tunao enda kutafuta haki zetu Mahakamani tumeachwa njia panda!!
mara sijui unatafasiriwa kizungu kwa kiswahili!! mara sijui andika kiswahili na kizungu!! yaani ni vurugu tupu na kero kwa wananchi.
kesi imeamuliwa mahakama ya mwanzo kwa lugha ya kiswahili, unaamua kukata rufaa mahakama za juu unakutana na kizungu kuhusu jambo lililo amuliwa kwa kiswahili!!!
huku ni kuwababaisha wananchi katika kutafuta haki.
Kama Lugha ya Kiswahili imeshindikana kutumika kwenye Mahakama zetu basi ni bora jambo hilo lifahamike tu kuliko kuwasumbua wananchi na kutafasiri sijui kutoka kizungu kwenda kiswahili!! huu ni usumbufu mkubwa na utumwa!!
Amueni moja, kama ni kizungu basi twendeni na kizungu kuanzia mwanzo hadi mwisho, kama ni kiswhili vivihivyo, lakini sio kuchanganya, mara kizungu na kichina!! mnatubabisha, sisi sote ni waswahili wa kitanzania mnasumbuka kwa nn?! mnataka kumridhisha muwekezaji au mfadhili?!! badala ya mwananchi!!!