Ni kweli mwanafunzi akisoma Shule binafsi hatapewa mkopo akifika chuo?

Sahvi si naskia Kuna selform wanajazia online ajaze shule ya bweni inayoendana na ufaulu wake.
Tunahofia kutokana na matokeo yake kuna uwezekano mkubwa mtoto akapangiwa tena shule za day hapa hapa Dar. Mfano Jangwani, Kibasila, Benjamin Mkapa nakadhalika.

Sasa huyu binti kwa kweli amechoka sana kusoma day Dar. Purukushan za usafiri kutoka Tegeta au Bunju mpaka posta kwenda kurudi. Ukizingatia PCB mzee sio mchezo.

Na tukisema tusubiri apangiwe Day kisha tumfanyie uhamisho usumbufu wake sio mchezo kupata shule ya boarding.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Budget haitoshi ndio maana wanafanya hivyo ingekuwa inatosha hata bila kulipia chuo kikuu ingewezekana
Najiuliza sipati majibu, kama mkopo anapewa mwanafunzi ili pindi atakapomaliza chuo arejeshe huo mkopo, sasa kwanini kuwe na ubaguzi wa kutoa hiyo mikopo!? Mimi nazani mikopo wangepewa wote wenye vigezo vya kwenda chuo kikuu bila kubagua shule aidha ya serikali au binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Budget haitoshi ndio maana wanafanya hivyo ingekuwa inatosha hata bila kulipia chuo kikuu ingewezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini swala hili lisipewe kipaumbele ikaandaliwa Budget inayoweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote wanaohitaji mikopo!, na pia kukawekwa utaratibu mzuri wa kufuatilia urejeshaji wa mikopo hiyo pindi wanafunzi hawa watakapokuwa wamemaliza vyuo. Mimi nazani inawezekana, ni basi tu nchi yetu inapenda kuvipa kipaumbele vitu visivyo vya msingi na vile vya msingi wanavipuuza.
 
Back
Top Bottom