Mchakato wa kubadilisha combination na shule kwa waliomaliza kidato cha Nne mwaka huu umeanza tayari

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
10,949
23,088
Habari za mchana Wana Jf.

Kuna mdogo wangu amefaulu kidato cha Nne nataka nimbadilishie shule na combination alizochagua awali huko Shuleni baada ya yeye kuja na mapendekezo mapya

Muda sasa tokea mwaka 2018 umekuja utaratibu mpya wa online unao muwezesha mwanafunzi kubadilisha shule , combination au kuchagua chuo ama advance baada ya matokeo ili kuendana na uhalisia na matakwa husika . Mpaka sasa naona kimya nimekuja humu kuuliza ili kupata muongozo kama tayari, nado au hakuna kabisa mwaka huu.

#UziTayari
 
Tayari,sasa rasmi mtu anaweza kubalisha combinations kupitia mfumo ramsi.
 
NB:Kuchaguliwa Kwa Tahasusi husika hutegemea mambo mengi sio kwamba umeingia hapo umebadili ukajua umemaliza.1.Idadi ya Shule Kwa Tahasusi husika.2.Kiwango Cha ufaulu Kwa Mwaka husika n.k.Sasa Kuna mwingine ana CCC ya Chem,Phys na Bios anaweka PCB chagua la kwanza wakati Mwaka husika watu wamepiga A na B za kutosha.Ndio wanajikuta wanapelekwa HKL huko wanapagawa na kutupa kazi ya cancelling.Ni utaratibu unaoleta sintofahamu Maana wanaofanikiwa Kwa Tahasusi aliyochagua na Shule aliyochagua ni wachache Sana.
 
Shukran ni kitu kipya kwangu na kimekuja wakati tunawaza tunafanyeje kwa huyu mtoto wa wifi yangu
 
NB:Kuchaguliwa Kwa Tahasusi husika hutegemea mambo mengi sio kwamba umeingia hapo umebadili ukajua umemaliza.1.Idadi ya Shule Kwa Tahasusi husika.2.Kiwango Cha ufaulu Kwa Mwaka husika n.k.Sasa Kuna mwingine ana CCC ya Chem,Phys na Bios anaweka PCB chagua la kwanza wakati Mwaka husika watu wamepiga A na B za kutosha.Ndio wanajikuta wanapelekwa HKL huko wanapagawa na kutupa kazi ya cancelling.Ni utaratibu unaoleta sintofahamu Maana wanaofanikiwa Kwa Tahasusi aliyochagua na Shule aliyochagua ni wachache Sana.
Kweli kabisa ,tokea mfumo huu unanze mwaka 2018 mwaka jana malalamiko yalikuwa mengi watu kupangiwa vitu tofauti kabisa na walivyovichagua natumaini mwaka huu umakini utaongezeka kama miaka ya nyuma yake .

Kingine ni katika kuchagua shule unakuta mwanafunzi anachagua shule zenye ushindani wakati matokeo yake sio ya juu ,hii inapeleke mara nyingi kutupwa shule za mbali sana.
 
Back
Top Bottom