Ni kweli mwanafunzi akisoma Shule binafsi hatapewa mkopo akifika chuo?

Mlolongo

JF-Expert Member
Jul 4, 2019
3,269
5,883
Wakuu wangu wazuri nawabusu.

Kuna mdogo wangu amemaliza Form Four Kisutu girls pale posta (Shule ya serikali) ana division two.

Sasa kuna Uncle alimuahidi kuwa akipata ufaulu mzuri atamsomesha Advanced shule moja private ipo Tanga.

Dogo anatarajia kusoma PCB (tuseme combination za science)

Sasa jana kuna jamaa alikuja home akatutisha akasema huo mpango wa kumpeleka private tuachane nao mara moja. Badala yake tusubiri selection za form five.

Amedai kuwa Sera za hivi sasa za HESLB kama umesoma private (either O level ama Advanced au level zote mbili) basi mkopo hupati bila kujali ume apply course gani chuo.

Sasa nauliza wenye watoto au wadogo zenu na wadau mlioko sekta ya elimu, hii Sera ni kweli iko hivi?

Kumbuka hiyo private anatarajia kusomeshwa kwa msaada wa mtu, baada ya hapo msaada unakoma. Tunatarajia asome combination mfano PCB.
 
Mkopo atapata endapo atapata kozi zenye priority.

Lkn kusoma private iwe primary,ordinary au advanced level kunapunguza % kadhaa kwenye vigezo vya kupata mkopo.

BTW kwa nn aende private? Shule za advance za government zinafanya vzr sana. Pia advance huwa ni wewe mwenyewe plus tuition kwa sana.

Mshauri huyo mjomba wako hizo pesa za kumsomesha private azielekeze kwenye kumsomesha tuition kwa sana.

Unforgetable
 
Hicho kitu kina Ukweli Fulani wanachukua aliyesoma shule za serikaki Mzazi wake maskini kitu ambacho si kweli Kuna wazazi Wana pesa na mavyeo serikalini na bungeni ila bahili. Wanasomesha watoto shule za serikali

Sasa hivi baada ya bodi kuonyesha wazi kuwa inapendelea waliosoma shule za serikali wazazi Wenye uwezo Wengine wameamua watoto wao wasome za serikali

Ila nitoe angalizo msingi wa mtoto kielimu unatakiwa kuwa imara hasa kuanzia shule za msingi na sekondari.Mzazi usiogope kumpeleka mtoto private kisa tu unaogopa mbele bodi ya mikopo itamnyima!!! Wewe andaa tu mwanao awe vizuri kwa level zote hasa za msingi na sekondari mengine mwachie Mungu atamsaidia mwanao mbele ya Safari
 
Mshauri huyo mjomba wako hizo pesa za kumsomesha private azielekeze kwenye kumsomesha tuition kwa sana.

Unforgetable
Private shule nzuri huwa hawataki kabisa mwanafunzi asome tuition inamchanganya mtoto .shule anafundishea hivi tuition vile.

Ila hili la bodi kupendelea wanaosoma shule za Serikali Lina madhara makubwa Sana nitatoa mfano .Shule za msingi za private ndizo hufaulisha Sana watoto kuliko za Serikali.Hivyo wengi huchaguliwa kwenda shule za sekondari za Serikali Lakini huwa hawaendi wanaamua kwenda sekondari za private.Wakienda huwapa nafasi wale ambao wasingeenda sekondari kuchukua nafasi zao.sasa Kama bodi inapendelea wa sekondari za Serikali Hawa wanasoma shule za msingi priivate wakiamua kuwa tunaenda soma za Serikali ili tupate mikopo mbeleni kundi kubwa la watoto maskini litakosa elimu ya sekondari.
 
BTW kwa nn aende private? Shule za advance za government zinafanya vzr sana. Pia advance huwa ni wewe mwenyewe plus tuition kwa sana.

Mshauri huyo mjomba wako hizo pesa za kumsomesha private azielekeze kwenye kumsomesha tuition kwa sana.

Unforgetable

Tunahofia kutokana na matokeo yake kuna uwezekano mkubwa mtoto akapangiwa tena shule za day hapa hapa Dar. Mfano Jangwani, Kibasila, Benjamin Mkapa nakadhalika.

Sasa huyu binti kwa kweli amechoka sana kusoma day Dar. Purukushan za usafiri kutoka Tegeta au Bunju mpaka posta kwenda kurudi. Ukizingatia PCB mzee sio mchezo.

Na tukisema tusubiri apangiwe Day kisha tumfanyie uhamisho usumbufu wake sio mchezo kupata shule ya boarding.
 
mimi O Level nilisoma private na A Level serikari ila sijapata mkopo na pia marafiki zangu wengi niliosoma O Level nao hawajapata labda uwe yatima au mlemavu unaweza ukapata

Chuo unasoma major ya kitu gani. Yaani unachukua degree program gani. Engineering ama Finance, ama Afya
 
Kma mnajua hamuwez kumudu gharama za chuo mpelekeni gov

Maan priority inaanza kwa wale waliopiga gov kwa sabab tunaamin wanahitaj back up

Kweny suala la koz ni hvyo hvyo hata kma umesoma priority kozi za serikal kama umesoma private school tutakupunguzia mkopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya priority course sijui kama inafanya kazi. Mimi mdogo wangu
alisoma engineering na hakupata mkopo.
O' level alisoma private alisomeshwa na shirika na advance alisoma private na alisomeshwa na mtu baada ya kuona ana uwezo darasani Ila hana mtu wa kumsomesha advanced level.
 
Priority haipo Siku hizi
 
Kma mnajua hamuwez kumudu gharama za chuo mpelekeni gov
Labda niseme maskini huwa hakopesheki husaidiwa bure.Kama seriksli inataka kusaidia watoto maskini isasomeshe bure kuwakopesha Ni kuwaonea mokopo wapewe watoto wa Wenye uwezo ili pesa zirudi wakimaliza.Chukulia mtoto wa mwenye uwezo.mfano kadomeshwa na Mzazi wake anamaliza chuo anaajiriwa yeye Hana Deni hata moja hivyo.mshahara mnono wote wake ,maskini aliyekopeshwa Alianza kazi anaanza na madeni makubwa ya mkopo.wa elimi ya juu anaanza maisha ya mateso kuanzia Mwezi anaoajiriwa.Mwenzie anatembea kitua mbele hadaiwi hata Mia.Serikali isomeshe bure tu hai watoto wa maskini siprndi binafsi kitendo Cha kuwakopesha
 
Na hawa wanaojiita viongozi wa wanyonge wote walisomeshwa chuoni buuuuure hawadaiwi hata 100 lkn leo wao ni wa kwanza kukomalia wenzao walipe.
Labda niseme maskini huwa hakopesheki husaidiwa bure.Kama seriksli inataka kusaidia watoto maskini isasomeshe bure kuwakopesha Ni kuwaonea mokopo wapewe watoto wa Wenye uwezo ili pesa zirudi wakimaliza.Chukulia mtoto wa mwenye uwezo.mfano kadomeshwa na Mzazi wake anamaliza chuo anaajiriwa yeye Hana Deni hata moja hivyo.mshahara mnono wote wake ,maskini aliyekopeshwa Alianza kazi anaanza na madeni makubwa ya mkopo.wa elimi ya juu anaanza maisha ya mateso kuanzia Mwezi anaoajiriwa.Mwenzie anatembea kitua mbele hadaiwi hata Mia.Serikali isomeshe bure tu hai watoto wa maskini siprndi binafsi kitendo Cha kuwakopesha

dodge
 
Kma mnajua hamuwez kumudu gharama za chuo mpelekeni gov

Maan priority inaanza kwa wale waliopiga gov kwa sabab tunaamin wanahitaj back up

Kweny suala la koz ni hvyo hvyo hata kma umesoma priority kozi za serikal kama umesoma private school tutakupunguzia mkopo

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi nilisoma chuo kikuu cha serikali zamani kidogo. Naomba kufahamu gharama za sasa za vyuo vikuu vya serikali kwa wanaosoma masomo ya sayansi zikoje? MUHAS, UDSM etc
 
Private shule nzuri huwa hawataki kabisa mwanafunzi asome tuition inamchanganya mtoto .shule anafundishea hivi tuition vile.

Ila hili la bodi kupendelea wanaosoma shule za Serikali Lina madhara makubwa Sana nitatoa mfano .Shule za msingi za private ndizo hufaulisha Sana watoto kuliko za Serikali.Hivyo wengi huchaguliwa kwenda shule za sekondari za Serikali Lakini huwa hawaendi wanaamua kwenda sekondari za private.Wakienda huwapa nafasi wale ambao wasingeenda sekondari kuchukua nafasi zao.sasa Kama bodi inapendelea wa sekondari za Serikali Hawa wanasoma shule za msing priivate wakiamua kuwa tunaenda soma za Serikali ili tupate mikopo mbeleni kundi kubwa la watoto maskini litakosa elimu ya sekondari.
Sio kweli kwamba hawaendi serikali eti kwakuwa.huwapa wengine nafasi ukweli ni kwamba

Waliosoma private wazazi wanao uwezo

So acha waliosoma kajambanani wapewe kipaumbele

Nina kijana kamaliza private English medium kafauli one of 3 best gov girls schools nimempeleka huko baada ya kuridhishwa na matokeo ya hio shule kwa miaka 5 kurudi nyuma

So option zote zingatia future ya mwanao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri nao kupa kwa div 2 hatusui pcb hio NI three ya advance

Abadili kombi haraka Sana ndio aende gov au aende na hio two yake best private schools
Tunahofia kutokana na matokeo yake kuna uwezekano mkubwa mtoto akapangiwa tena shule za day hapa hapa Dar. Mfano Jangwani, Kibasila, Benjamin Mkapa nakadhalika.

Sasa huyu binti kwa kweli amechoka sana kusoma day Dar. Purukushan za usafiri kutoka Tegeta au Bunju mpaka posta kwenda kurudi. Ukizingatia PCB mzee sio mchezo.

Na tukisema tusubiri apangiwe Day kisha tumfanyie uhamisho usumbufu wake sio mchezo kupata shule ya boarding.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom