Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Mr mutuu

JF-Expert Member
Jan 27, 2023
2,027
10,031
Hizi shule(mzumbe,pugu,kisimiri,ilboru,kibaha and the likes) japokua siku izi nyingi zimepoteza sifa zake aisee kama una moyo mwepesi usiende huko unaweza kupata depression au pressure ukashindwa kusoma

Miaka Hio mwisho wa miaka ya 2000 niliripoti Moja ya shule tajwa hapo combination ya pcm... Kipindi hicho special school wamejaa watoto wa dar kutoka (kibaha, Azania, pugu) aisee Hawa madogo wana sifa kishenzi.... Mtu anakuja kuripoti form 5 ameshamaliza topic zote za form 5 anakaribia kumaliza za form 6

Sasa si matozi tulivyomaliza form 4 vitabu tukatupa Kule mpaka siku ya kuripoti hujawahi kupiga pindi lolote... Unakutana na vitoto vimesoma sijui mchikichini huko aisee wamefuta topic zote, aisee nilipata presha sana mpaka kuzoea ile Hali.... Nakuta madogo wanapiga integration kama hawana akili, ukikaa bwenini wanaulizana kwa nguvu reaction za organic. Chemistry huko....

Dah yaani mwezi wa kwanza form 5 watu wanasolve necta review nikasema hapa nimeyatimba... Aisee ile presha ya ku catch up nilipata shida Sana sio Siri... Ukiwa na roho nyepesi unaweza kukata tamaa Moja kwa Moja

Kuna dogo tumeingia form 5 alikua anaitwa T.O (Tanzania one) alitukimbiza wote form 4 aisee huyu Jamaa mpaka Leo hua namuogopa. Hua namwambia hata hii kazi ya u engineer unayofanya unastahili kua somewhere else una potential kubwa sana, picha linaanza tumeingia form 5 hapo.... Sasa form 6 walikua wanafanya fitness tests (hii anatokea mwanafunzi mmoja au wawili wanatunga mtihani alafu wengine wanafanya japo sio lazima)

Ujinga wa hii mitihani wanafunzi wanajua kukomoana yaani maswali yote unakuta ya kibabe... Kuzungusha 0 huku ni kawaida tu ndo maana wengi walikua hawataki huu ujinga, dogo bana tunafika form 5 kaskia form 6 wanafanya fitness test ya physics dogo akazamia akapiga Pepa... Matokeo yanatoka form 6 karibu wote wamefeli dogo kawakimbiza.... Wote wanaulizana hili jina nani mbona hatumjui... Kuja kuulizia wakaja kugundua ni dogo wa form 5 aisee jamaa walimind kinoma akapigwa marufuku kabisa kusogeza pua kwenye fitness tests za form 6

Huyu dogo tulipofika form 6 sidhani kama aliwahi kukaa akasoma, jamaa alikua anakaa zake class watu wamepanga foleni na maswali Yao yaliowashinda dogo anapiga yote tu hajali kama ni ya physics, chemistry, pure au bam ye anasolve tu. Alikuja kua Tanzania one tena form 6 jamaa walimtangaza hesabu paper 1 na 2 zote alipiga 100%.

Huku kama una roho ndogo sio pa kwenda mi nusura panishinde nilitaka nirudishe mpira kwa kipa(kuhamia private)
 
Tatzo la walimu wa specials schools hawafundishi, wanapiga lecture TU,

Na wako bize na miradi yao mbalimbali mitaani, hawana njaa njaa sana ndo maana uchagua wanafunzi cream.

Kama ulizoea spoon-feeding lazma uteseke
Wanafunzi pia hawapendi kufundishwa wanaona kama wanapotezewa muda tu... Tulikua na mwalimu wa chemistry jamaa alikua anafundisha shule mbili za private huku kaajiriwa serikali

Jamaa ukiacha practical sidhani kama aliwahi hata kutufundisha, alikua mtu wa vyombo alikua anakuja class tunapiga nae story tu za mademu😃😃
 
Umenikumbusha kijana mmoja anaitwa Rajabu ndegeulaya.

Tuna report advance Azania yeye alipitisha tangazo la kuwa anafundisha tuition Kwa WANACHUKUA PHYSICS, CHEMISTRY NA PURE MATHEMATICS.

WATU walizani ni form six kumbe ni form five alishamaliza topic zote mpaka za six basi ikabidi tuendelee kupiga mapindi kwa Ndegeulaya.
 
Umenikumbusha kijana mmoja anaitwa Rajabu ndegeulaya.

Tuna report advance Azania yeye alipitisha tangazo la kuwa anafundisha tuition Kwa WANACHUKUA PHYSICS, CHEMISTRY NA PURE MATHEMATICS.

WATU walizani ni form six kumbe ni form five alishamaliza topic zote mpaka za six basi ikabidi tuendelee kupiga mapindi kwa Ndegeulaya.
Rajabu juma ndegeulaya ,o'level alipiga na additional mathematics aisee alisoma azania na akarudi hapo hapo
 
Back
Top Bottom