Ni kweli kuna utajiri wa nguvu za giza?

Jack Wabukoba

Member
Dec 11, 2014
11
9
Hi ndugu,

Naambiwa sana na kusoma simulizi kuwa mganga wa kienyeji anaweza kumuwezesha mtu kupata utajiri. Utajiri tena wa pesa taslimu (CASH) noti tupu. Kwamba unaenda kwa mganga na ukitoka tayari unazo, unatoka na maburungutu ya kutosha kwenye mfuko (begi).

NAOMBA anayejua anijuze kwamba JE, HII HABARI NI YA KWELI? Na huyo mganga huipata wapi hiyo cash anayokupa mfano 250M?
 
Anaipata benk
 
Pesa hizo za mabulungutu utazipata kwa waganga kwa sababu wanatumia nguvu za Giza. Lakini ujue kuwa pesa hizo huzipati kirahisi hivo. Lazima utalipa kwa gharama kubwa Sana.

Kama unataka pesa hizo, jiandae kwa matokeo haya .
1.kupata kidonda kisichopona (donda ndugu).
2. Kufa ghafla kwa Mzazi wako , Baba au Mama.
3. Kufa ghafla kwa mmoja wapo wa watoto wako unayempenda sana.
3. Jiandae kwenda motoni baada ya kifo chako kwa sababu Mungu muumba hapendi watu wategemee watu bali wamtegemee yeye Mungu , maana yake ni machukizo mbele za Mungu.

" Kalaga bahho ".
 
Kuna story huku ya Lwanda Magere itafute.

Hii hapa

Kuna M/MUNGU then kuna SHETANI kwa hivyo ni free tu ukitaka mafanikio/utajiri kwa njia ya M/MUNGU utapata na pia ukitaka kutoka kwa SHETANI utapata pia ..hakuna haja ya kwenda kwa mganga hapo hapo ulipo mkane M/MUNGU kwa kusema tu umtambui na zungumza maneno kwa kumtaja/kumuomba SHETANI chochote unachotaka na utapata kwa mda maalumu utakaomwambia akupe sema ni vina madhara sana vitu vya SHETANI .. na ukisha mkana M/MUNGU hakuna njia sahihi ya kumrudia.. Asante MKUU
 
Naona mpaka hapa ni kua jibu lake upo huo utajiri

Hayo mengine sijui kufiwa kwenda motoni sijui na nini haijalishi

Kinachoitajikana ni kua pesa hapa duniani bila pesa ni kunyanyapaliwa tu

Wekeni connection za hao watu wa ndagu kama wapo kweli msilete story
 
Pesa hizo za mabulungutu utazipata kwa waganga kwa sababu wanatumia nguvu za Giza. Lakini ujue kuwa pesa hizo huzipati kirahisi hivo. Lazima utalipa kwa gharama kubwa Sana.
Kama unataka pesa hizo, jiandae kwa matokeo haya . 1.kupata kidonda kisichopona (donda ndugu). 2. Kufa ghafla kwa Mzazi wako , Baba au Mama. 3. Kufa ghafla kwa mmoja wapo wa watoto wako unayempenda sana. 3. Jiandae kwenda motoni baada ya kifo chako kwa sababu Mungu muumba hapendi watu wategemee watu bali wamtegemee yeye Mungu , maana yake ni machukizo mbele za Mungu.
" Kalaga bahho ".
Umeishi duniani miaka 45 lakini maisha yako ni kuungaunga mpaka leo....nyumba za ibada huendi.hutoi sadaka na wala hujishughulishi kufanya jambo lolote la kumpendeza mungu...ukifa unahisi utakwenda wapi peponi au motoni?😁😁
 
Kuna story huku ya Lwanda Magere itafute.

Hii hapa

Hii kitu haifiki mwisho japo hatar asee, imeishia katikati. Hauna link nyingine inayoweza kunipa story hyo A-Z?
 
Jamani hivi kweli kuna waganga wa kienyeji wanaoweza kumpa mtu utajiri? Maana marangazo Kila Kona lakini ukifwatilia ni utapelitu wote hao wanataka pesa,nisaidieni tafadhali
 
pesa inamazingira yake hakuna uchawi ni utapeli wakisaikolojia tu!
 
Back
Top Bottom