Utajiri wa pesa za ndagu

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
16,409
2,000
Mwaka huu mwanzoni nilikuwa mkoani Arusha kwa jamaa yangu mmoja tuliyetoka nae Kijiji kimoja huko mkoani kwa baba wa taifa.

Siku moja katika matembezi mjini na huyu jamaa yangu, Ghafla nikasikia naitwa jina langu kwa kilugha changu na mchoma mahindi aliyekuwa pembeni yetu "Requal, Omwanono Ge zisiku ndola ukulili igo" nikashangaa kidogo maana alikuwa mmama wa makamo na sikuweza kumkumbuka kabisa. Ikabidi nimjibu "Mazomu", baadae akahamia kwa jamaa akawa anamuuliza umempata wapi huyu kiumbe maana sijamuona zaidi ya miaka 10, katika maongezi ndio nikaja kugundua ni Sarah, sio jina sahihi (Jirani yangu kabisa kule kijijini) ni kweli hatujaonana miaka 10 na zaidi.

Ule urembo wake umeisha kabisa na sasa anaonekana kama bibi yangu japo amenizidi miaka 4 tu ya kuzaliwa.Kiukweli alikuwa amechoka sana na alionekana mtu aliyekata tamaa na maisha kabisa na hapa ndipo nilipoona Kuna haja ya kuweka hapa huu mkasa ili wengine wajifunze.

STORY YA FAMILIA YA AKINA SARAH.

Sarah ametoka familia ya watoto watano pale kijijini kwetu, wa kike wawili na wakiume watatu, mkubwa tumpe jina Joseph, anaefuata wa kiume "nyanza", na wa mwisho wa kiume aitwe "Gedo". Hiki kisa kinamhusu zaidi Sarah, Gedo, mama yao pamoja na mume aliyekuja kumuoa Sarah. Kabla hatujafika huko tutamzungumzia kidogo Joseph ili kupunguza maswali huko mbeleni.

Baba yao Sarah alikuwa na wake wawili na mama yao Sarah hakuwa kipaumbele Cha baba yao, mke mdogo ndiye aliyependwa zaidi na familia ya mke mkubwa ni kama ilitelekezwa vile.

Baba yao Sarah alikuwa na ndugu mmoja tu wa tumbo moja wa kiume na wa kike mmoja pia walipenda sana. Hawa wazee ilikuwa ni mfano kijijini pale kwa jinsi walivyokuwa wanapendana. Huyu wa kiume ambaye ni baba yake mkubwa Sarah alikuwa na wake wawili na mke mkubwa alikuwa anasadikika ni mchawi mkubwa sana pale kijijini; anasadikika kufuga misukule Kule kijijini watu wanamuogopa mno tukikutana nae porini mwenyewe huwa tunajificha ili apite, huwa havai viatu akitembea na haachi unyao anapokanyaga. Naye atahusika kidogo kwenye huu mkasa.

MKASA WA JOSEPH.

Joseph ni mtu mzima kidogo amezaliwa miaka ya 70's, huyu jamaa ana asili ya roho nzuri sana, mcheshi na mkarimu mno alikuwa family friend wa ukoo wetu, alioa mwanamke mrembo sana kutoka Kijiji cha jirani yule mke hata ukikutana nae leo ni vigumu kujua Kama ile ni product ya kijijini.

Nikiwa bado niko elimu ya msingi kipindi hicho, Joseph akapotea pale kijijini kwa vile alikuwa family friend ilikuwa rahisi kujua mahali alikoenda, tukaambiwa ameenda mgodini Arusha Merelani kutafuta maisha kwenye machimbo ya Tanzanite, mkewe alibaki na baada ya mda mkewe alimfuata na huko ndio yakawa makazi yao.

Maisha ya familia hii yalikuwa ya kawaida sana, mama yao alikuwa anaishi nyumba ya suit yaani imejengwa kwa mabati chakavu kuanzia chini mpaka juu..na wao walikuwa na nyumba za nyasi pembeni na zaidi walikuwa wanategemea kilimo Cha jembe la mkono ili kuendesha maisha.

Baada ya Kama miaka miwili Joseph akarudi pale kijijini na kabla yeye kurudi kusalimia taarifa zilikuwa zimeshazagaa kwamba Joseph Sasa amewin maisha, watu pale tukawa na hamu ya kumuona kama mnavojua maisha ya kijijini.

Jamaa alikuja kwa gari lake akiwa anaendesha mwenyewe alikuwa ni gumzo pale kijijini na isitoshe alikuwa anagawa pesa kwa kila mtu anaekutana nae ambaye wanajuana, hili halikuwapa watu maswali kwa sababu ya roho yake nzuri toka mwanzo, aliwawezesha sana ndugu na akaanza ujenzi rasmi wa nyumba mpya na ya kisasa kabisa ya mama yake kuishi.

Baada ya kuanza ujenzi baba yao akahamishia kambi kwa mke mkubwa na akapewa kazi ya kusimamia ule ujenzi wa ile nyumba na Joseph akarudi Arusha kuendelea na kazi zake.

Joseph Ghafla akawa na maisha mazuri mno, na mke wake ule urembo ukang'ara zaidi, alikuwa ni zaidi ya mrembo yule mwanamke, walifungua miradi mingi na kujenga nyumba nyingi huko Arusha na wakawa wanakuja kijijini kusalimia mara kwa mara, miaka ikaenda huku utajiri wao unazidi kukua.

Sasa kuna mwaka kukawa na harusi ya ndugu yao inafanyika pale kijijini, bado niko shule ya Msingi mpaka kipindi hicho, maandalizi yakaandaliwa na Joseph alitegemewa kama mgeni mahsusi na marafiki zake atakaokuja nao. Basi bhana, siku ya mkesha ilipofika kwa yale madisko ya kijijini kwa mnaoyafahamu tulicheza balaaa kunakucha unajikuta una vumbi kuanzia kwenye ukucha mpaka kwenye kope za uso.

Joseph na rafiki zake waliingia usiku huo wa mkesha; tulikula nyama za kutosha ile harusi, kesho yake ikawa ni siku ya kuzawadia, Joseph huohuo usiku akaanza kugawa pesa kama kawaida yake.

Baada ya Joseph kuzawadia akaaga kuondoka pamoja na marafiki zake na walifanya kufuru ya kutisha kwenye kutoa zawadi kabla hajaondoka akaenda kumuaga mke wa baba yake mkubwa yule mchawi na akampa 50k.

Bwana eeeh Kumbe yule mama alikuwa anaona nongwa huyu Joseph kufanikiwa, alichokifanya akachukua zile 50k akazilowanisha then akazisaga zikawa ungaunga kabla ya kuzichanganya na madawa anayojua yeye ili kuuyeyusha utajiri wa Joseph..huku mbele utafahamu ni namna gani hii siri ya huyu mchawi ilivuja.

Safari ya huyu Joseph na rafiki zake kurudi Arusha ikawa ya misukosuko sana walipotea sana huko njiani iliwachukua siku saba kufika Merelani na alipofika mambo yake yakaanza kuwa mabaya mno.

Baada ya ugumu wa miezi kadhaa akaanza kuuza kitu kimoja baada ya kingine, nyumba zote zikauzwa, gari na miradi yote ikafirisika akawa anaomba hata 500 na wanawake aliowajengea wakawa hawataki tena hata kumuona, mke wake pia akamkimbia..Joseph akarudi kwenye umaskini wa kutupwa.

Kwa mujibu wa wazee pale kijijini, Wanasema huyu Joseph Utajiri wake ulikuwa wa masharti nafuu kulingana na nyota yake na masharti yake ilikuwa ni kugawa pesa na mengine madogomadogo na Kama Ingekuwa sio huyu mama yake mkubwa kumuonea wivu na kumroga basi jamaa angekuwa mbali.

HukuJuu tumemzungumzia Joseph kidogo ili kupunguza maswali huko mbeleni lakini mlengwa wa huu mkasa hasa ni Sarah, Gado, mama yake Sarah na mume atakayekuja kumuoa Sarah.

Tuendelee sasa.

Gado naye hakukaa mda pale kijijini kwa mda mrefu akaenda Merelani kutafuta maisha pia

Sasa pale kijijini kwetu Kuna mmama mmoja maarufu anaitwa Wasosi ni jina lake halisi, huyu mama ni mcheshi sana kiasi kwamba vijana wengi waliotaka kuoa hasahasa waliokuwa nje ya pale kiutafutaji walimuomba awatafutie mke mwenye tabia nzuri ili waoe..yaani ilikuwa yeye anatafuta Mali inapelekwa halafu mwanamke anaenda kwa mume wake huko mikoani ili kupunguza gharama na wengi wao wanakuwa hata hawajuani.

Sasa huyu Wasosi alikuwa na kaka zake mkubwa nimemsahau jina lakini mwingine namjua kwa jina moja Kiringo ambaye ni mkuu wa Auxiliary police hapo UDSM. Huyu ni mtu wa dini, mcha Mungu hasaaa na mpenda haki na kwa mara ya kwanza nimeonana nae mwaka huu msibani hapa Dar.

Kaka yake mkubwa huyu Wasosi akatangaza nia ya kuoa, Dada mtu huyu Wasosi akamuambia kaka huku kijijini Kuna msichana mrembo sana na mpole mno anakufaa kuoa, kaka mtu akataka atumiwe picha ili ajiridhishe akatumiwa, kweli Sarah alikuwa mzuri kaka mtu akajikuta amempenda akaruhusu wasosi apeleke ujumbe kwao Sarah na alipopeleka akakubaliwa taratibu za kaka kuja pale kijijini kuonana za sarah na familia yake zikafanyika na hatimae harusi ikafika wakaoana wakawa mke na mume.

Wakahamia Dar kimakazi, baada ya mda Gedo akarudi pale kijijini kusalimia vile na Mimi ndio nikawa namalizia Elimu yangu ya msingi. Kumbe jamaa alikuwa ameanza harakati za kuutafuta Utajiri wa giza.
Gado alimfata mzee mmoja pale kijijini na akamuelezea dhamira yake ya kutaka utajiri huu wa NDAGU na akamueleza anataka iwe Siri, yule mzee alikuwa ni mtu anaefahamu sana waganga na alikuwa anajua dawa nyingi za kutibu kienyeji, wakapotea na Gado kwenye vijiji vya mbali huko usukumani na baada ya wiki kadhaa wakarejea pale kijijini kwetu na Gado akarudi Arusha

Sasa kuna mwaka kukawa na harusi ya ndugu yao inafanyika pale kijijini, bado niko shule ya Msingi mpaka kipindi hicho, maandalizi yakaandaliwa na Joseph alitegemewa kama mgeni mahsusi na marafiki zake atakaokuja nao. Basi bhana, siku ya mkesha ilipofika kwa yale madisko ya kijijini kwa mnaoyafahamu tulicheza balaaa kunakucha unajikuta una vumbi kuanzia kwenye ukucha mpaka kwenye kope za uso.

Joseph na rafiki zake waliingia usiku huo wa mkesha; tulikula nyama za kutosha ile harusi, kesho yake ikawa ni siku ya kuzawadia, Joseph huohuo usiku akaanza kugawa pesa kama kawaida yake.

Baada ya Joseph kuzawadia akaaga kuondoka pamoja na marafiki zake na walifanya kufuru ya kutisha kwenye kutoa zawadi kabla hajaondoka akaenda kumuaga mke wa baba yake mkubwa yule mchawi na akampa 50k.

Bwana eeeh Kumbe yule mama alikuwa anaona nongwa huyu Joseph kufanikiwa, alichokifanya akachukua zile 50k akazilowanisha then akazisaga zikawa ungaunga kabla ya kuzichanganya na madawa anayojua yeye ili kuuyeyusha utajiri wa Joseph..huku mbele utafahamu ni namna gani hii siri ya huyu mchawi ilivuja.

Safari ya huyu Joseph na rafiki zake kurudi Arusha ikawa ya misukosuko sana walipotea sana huko njiani iliwachukua siku saba kufika Merelani na alipofika mambo yake yakaanza kuwa mabaya mno.

Baada ya ugumu wa miezi kadhaa akaanza kuuza kitu kimoja baada ya kingine, nyumba zote zikauzwa, gari na miradi yote ikafirisika akawa anaomba hata 500 na wanawake aliowajengea wakawa hawataki tena hata kumuona, mke wake pia akamkimbia..Joseph akarudi kwenye umaskini wa kutupwa.

Kwa mujibu wa wazee pale kijijini, Wanasema huyu Joseph Utajiri wake ulikuwa wa masharti nafuu kulingana na nyota yake na masharti yake ilikuwa ni kugawa pesa na mengine madogomadogo na Kama Ingekuwa sio huyu mama yake mkubwa kumuonea wivu na kumroga basi jamaa angekuwa mbali.

HukuJuu tumemzungumzia Joseph kidogo ili kupunguza maswali huko mbeleni lakini mlengwa wa huu mkasa hasa ni Sarah, Gado, mama yake Sarah na mume atakayekuja kumuoa Sarah.

Tuendelee sasa.

Gado naye hakukaa mda pale kijijini kwa mda mrefu akaenda Merelani kutafuta maisha pia

Sasa pale kijijini kwetu Kuna mmama mmoja maarufu anaitwa Wasosi ni jina lake halisi, huyu mama ni mcheshi sana kiasi kwamba vijana wengi waliotaka kuoa hasahasa waliokuwa nje ya pale kiutafutaji walimuomba awatafutie mke mwenye tabia nzuri ili waoe..yaani ilikuwa yeye anatafuta Mali inapelekwa halafu mwanamke anaenda kwa mume wake huko mikoani ili kupunguza gharama na wengi wao wanakuwa hata hawajuani.

Sasa huyu Wasosi alikuwa na kaka zake mkubwa nimemsahau jina lakini mwingine namjua kwa jina moja Kiringo ambaye ni mkuu wa Auxiliary police hapo UDSM. Huyu ni mtu wa dini, mcha Mungu hasaaa na mpenda haki na kwa mara ya kwanza nimeonana nae mwaka huu msibani hapa Dar.

Kaka yake mkubwa huyu Wasosi akatangaza nia ya kuoa, Dada mtu huyu Wasosi akamuambia kaka huku kijijini Kuna msichana mrembo sana na mpole mno anakufaa kuoa, kaka mtu akataka atumiwe picha ili ajiridhishe akatumiwa, kweli Sarah alikuwa mzuri kaka mtu akajikuta amempenda akaruhusu wasosi apeleke ujumbe kwao Sarah na alipopeleka akakubaliwa taratibu za kaka kuja pale kijijini kuonana za sarah na familia yake zikafanyika na hatimae harusi ikafika wakaoana wakawa mke na mume.

Wakahamia Dar kimakazi, baada ya mda Gedo akarudi pale kijijini kusalimia vile na Mimi ndio nikawa namalizia Elimu yangu ya msingi. Kumbe jamaa alikuwa ameanza harakati za kuutafuta Utajiri wa giza.

Gado alimfata mzee mmoja pale kijijini na akamuelezea dhamira yake ya kutaka utajiri huu wa NDAGU na akamueleza anataka iwe Siri, yule mzee alikuwa ni mtu anaefahamu sana waganga na alikuwa anajua dawa nyingi za kutibu kienyeji, wakapotea na Gado kwenye vijiji vya mbali huko usukumani na baada ya wiki kadhaa wakarejea pale kijijini kwetu na Gado akarudi Arusha.

Kwenda kwa waganga kwa maisha ya kijijini ni jambo la kawaida lakini hakuna mtu aliyefikiria Gado ameenda kutafuta Utajiri huu wa kishetani. Mimi nikiwa nimemaliza mitihani yangu ya S/M najiandaa kwenda kidato cha kwanza shule niliyopangiwa huko mikoa ya mbali. Kabla ya X-Mass ilikuwa December Gado akaja tena kijijini kusalimia na wakapotea tena na yule mzee kwa wiki kadhaaa kabla ya kurudi na kuondoka tena.

Mimi nikaondoka Pale kijijini nikaenda masomoni sikuwa na simu wala mawasiliano na watu au ndugu wa pale kijijini kwetu zaidi ya wazazi wangu nikawa narudi likizo tu baada ya miezi 6.

Likizo ya 2006 narudi pale kijijini nasikia stori za Gado ni tofauti kabisa Jamaa alikuwa tajiri wa kutisha pale kijijini, alijenga nyumba nzuri kabisa na ya kisasa pale nyumbani kwa mama yake ukiachana na ile aliyojenga kaka yake. Kijijini kwetu kulikuwa hamna umeme.

Umeme ulikuwa mbali zaidi ya 5 km huyu mwamba akawafuata tanesco akawaambia wampigie mahesabu ya nguzo na gharama ya Transformer ili kuutoa umeme umbali huo mpaka nyumbani kwao TANESCO chapchap wakafanya hii kazi umeme ukaingia Hadi kwao na akanunua transformer kwa pesa zake ambapo mpaka leo ndiyo inayotumika pale kijijini, na kwa mara ya kwanza kijijini kwetu kukawa na umeme na nyumba ya kisasa kabisa Kama zilizoko mjini.

Huyu mwamba alikuwa na pesa sana, pale kijijini Kuna jamaa alikuwa ndio anaonekana tajiri alikuwa na ng'ombe zaidi ya 600, siku moja wakatofautiana kimaongezi na huyu jamaa akaenda mnadani alinunua zaidi ya ng'ombe 400 katika minada tofauti tofauti akaziweka pale kwao akaona haitoshi akaenda kununua zingine minada mingine akawa anaweka kwa rafiki zake.

Baba yake tayari alikuwa ameshahamishia makazi kwenye nyumba kubwa ambapo ni kwao kwa mama yake. Story ikawa ni GADO pale kijijini. Alipokuwa anakuja pale kijijini wazee walikuwa wanampisha kiti akae wao wanasimama au wanachuchumaa hata pale jamaa alipokuwa anakataa Hawa wazee wakawa hawataki. Cha kushangaza huyu jamaa sio mkubwa kiumri amezaliwa 1980's. Pesa si mchezo aisee.

Gado akananunua VX na V8, marafiki zake wakawa ni watu wazito Ma-RPC, wakubwa wengi wakati jamaa hata elimu hana na hata pale alipokuwa anakuja kijijini baadhi alikuwa anakuja nao.

Alijenga ghotofa 3 za maana Arusha na nyumba nyingi sana.

----------------------------------------

Mwaka 2007 kama sikosei mme wa Sarah akawa anapigiwa simu sana na Gado ahamie Arusha na yeye atamtafutia kazi alimshawishi sana na kupitia mke wake pia akawa anamsihi waende kwa kaka yao awatafutafutie kazi maana tayari kaka yao ameshakuwa na pesa kidogo.

Sasa huyu mume wa Sarah ikabidi amshirikishe mdogo wake ambaye ndio huyo Kiringo anaefanya kazi hapo udsm,Kiringo akamkatalia akamsihi kaka yake abaki na yeye atamtafutia hiyo kazi, Lakini ushawishi wa mwanamke ukawa juu zaidi hali iliyopelekea kumjibu vibaya mdogo wake na kweli wakaondoka kwenda Arusha na mkewe.

Kumbe kuna mipango ya Siri ilikuwa imesukwa kati ya Gado, mdogo wake Sarah na mama yao mzazi. Mpaka kipindi hiki wanatoka wanaenda Arusha Sarah alikuwa na mumewe walikuwa na mtoto mmoja wa kike.

Walipofika kule haikukaa mda mume wa Sarah aliumwa usiku ghafla na akafa.

----------------------------------------

Kwa mujibu wa watu hapa kijijini hakuna mtu yeyote aliyehusisha ule msiba na dhana potofu ilionekana Kama vifo vingine vya kawaida.

Mambo yakaendelea kuwa mazuri zaidi kwa Gado, nakumbuka mwaka mmoja alikuja pale kijijini na Mimi nilikuwepo likizo nilishuhudia anafanya operation ya kuondoa vitanda vyote vya ngozi ama vile vya spring vilivyokuwa vinatumika sana kule kijijini kwenye nyumba za ndugu, jamaa na marafiki zake walikuwa ni wengi akawawekea vitanda vipya vya mbao na magodoro.

Huyu mwamba nadhani alijifunza kutokana na makosa ya Kaka yake, alikuwa hatoi pesa taslimu yeye alikuwa anawanunulia ndugu vitu au anampa pesa mtu mwingine akupe.Huyu Gado akaendelea kuwa tajiri sana mwenye ukwasi wa kufa mtu, nakumbuka mwaka 2015 alimuita ndugu yangu mmoja hotelini pale Musoma mjini baada ya kuja kusalimia kijijini Hawa walikuwa hawajaonana siku nyingi katika maongezi yao aligusia kwamba kwa mda ule alikuwa na akiba bank kama 1.9 bilioni hivi.

Jamaa akawa anaogolea kwenye ukwasi na pale kijijini akawa anaheshimika sana na akawa tayari amepata watoto wawili na yule mkewe traffic. Kitu nilichogundua ukiwa na pesa hata watu wakijua ni za madhara bado watakuheshimu na kukunyekea tu yaani huyu jamaa alikuwa ananyenyekewa pale kijijini utafikiri mfalme.

Kuna mwaka, mama mkwe wa Wasosi ambaye Sasa ni shemeji yake na huyu Gado maana Kaka yake ni yule aliyetolewa kafara akafariki pale kijijini na Mimi Kama kijana nikaenda kushiriki ule msiba, Cha kushangaza Gado sijui alipata wapi Ujasiri akafunga safari kuja msibani.

Pale Msibani alikuwepo mama yake Wasosi pia, wakawa wamepata taarifa za ujio wake huyu mwamba msibani jamaa alipofika na mkewe lile gari tu kuingia yule mama yake Wasosi alipiga ukunga ambao sijawahi uona Aisee huku akilalamika kwa uchungu na kutukana..nanukuu baadhi ya maneno ninayayakumbuka..." Uwiiiiiiiiiii mbwa wewe, Shetani mkubwa umemuua mwanangu Sasa wewe unafurahia na maisha, umeuua mwananangu, kweli umeuua mwananangu au hiyo gari ndio mwanangu" huyu mama alikiwa akiongea haya huku akionekana kuishiwa nguvu.

Wabibi wenzake wakawa wanamtuliza na baadhi ya wazeee lakini hali ya pale Msibani ikawa sio nzuri japo jamaa hakuonekana kujali kabisa..na baada ya kuzika yeye akaondoka.

Mimi nilikuja kuondoka pale kijijini nikaendelea na harakati za kutafuta maisha mikoani, mwaka juzi nikapata habari za huyu mwamba kwamba ameanza kufirisika ..kweli mpaka nakuja Arusha huyu Gado amebaki na Ghorofa moja tu zingine zote ameshauza na hata gari Hana..mke alishamkimbia nadhani hata hii ghorofa itauzwa mda si mrefu sijui alikosea wapi kwenye masharti yake huyu mwamba.

Mishe zimemgomea kabisa, Hana pesa tena.

Kibaya zaidi familia imeshaparanganika baba yao alishafariki.., watoto wote na mama hawaaminiani tena na hata upendo kati yao haupo kabisa yaani wanapitana Kama unavyompita mtu njiani..wanaishi kwa kuviziana sana.

Huyu mkubwa Joseph kwa Sasa ni Dereva Merelani hapo na afadhari amerudi kupatapata vipesa yuko njema kiasi chake kwa Sasa.

Yule mtoto wa Sarah, kwa Sasa ni binti mkubwa yuko vidato kadhaa na anajua kila kitu kuhusu stori ya kifo Cha baba yake, binti ana kisasi sana na Hawa ndugu ndugu zake.

kupitia kwa watu na hata Joseph mwenyewe anasema binti amesema hawatambui akiwemo mama yake mzazi Sarah na hajawahi hata kwenda kuwasalimia hata kwenye simu.

Maisha yao yamegeuzwa kuwa Arusha japo kwa Sasa yamekuwa magumu sana wanaona soni kurudi pale kijijini tena na pale Kijijini Kuna miamba mipya iliyofuata nyayo za Gado imeibuka ndio inatawala sasa.

Sarah kachoka sana hadi anatia huruma.

.................................................

Hiki kisa ni cha kweli na hakijatokea miaka mingi. Ukiwa unatoka mwanza au Bunda na unaenda Musoma mjini au Tarime shuka hapo sabasaba mbele ya kiabakari na Mazami. Hapohapo barabara kuu ya Musoma ulizia kwa mzee Nyanda au uliza mtu yeyote hii stori ukifika sabasaba.

Kwa mlioko mjini unaweza kumuona huyo Kiringo hapo udsm na atakupa huu mkasa uliochukua maisha ya kaka yake.

Credits: 40 BYB

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
9,310
2,000
Hiyo simulizi ilishaletwa huku!
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
4,836
2,000
Muraa wewe mzanaki hovyo kabisa!!! yaani niache ndagu yenye pesa eti naogopa kufirisika yaani utakuwa mjinga wa mwisho ni kawaida maskini hafilisikagi? nakuuliza? weee!!! amejenga mijumba, mighorofa mwee! unataka nini sasa hapo.

tena nimetembelea mji-VX, nimepanda ndege kwenda Ulaya nimenunua Helkopta weee! siyo padogo hapo ati! lakini si ameonja maisha mazuri? wacha nifilisike tu halooo! maisha nimeyakulamo!

Angalia familia ya nyerere, ilivo leo! watu walikuwa wana heshimika ile mbaya lkn leo Madaraka anakula vihepe km mtu wa kawaida tu! angalia familia ya Gadaffi piga picha walivokuwa na leo walivo!!! hiyo ni kawaida yetu matajiri! sisi!! hatuogopi!

Mifano ni mingi km watoto wa mwinyi wameajiliwa km watu wa kawaida kabisa!! lkn hawakufanya ndagu!! hata hiyo ndagu haimukubali kila mtu yeyote !!! Hurry leo yuko Canada anaishi maisha ya kawaida kabisaaaa!

Mama yake Hurry aliacha uroda Bukhingham palace akaenda kuliwa na mlevi!! tena siyo kuolewa kupiga ufuska km CD mutu wa kawaida kabisaaaa!! akafa, sasa hao ni watu maarufu nakusimulia!! sembuse hao wala ugali ya ulezi!! acha ushamba weye Mzanaki!

Unatupa habari za tu-Ghorofa twa mawazo hapa? ka ji vx kamtumba hako umeona ndo maisha shika adabu yako!! angenunua visiwa je? angemiliki Tetanic kumi ungesemaje? Mi- tanker, Viwanda vya siraha huo ndo utajiri, kukopesha nchi kama kumi hivi Africa hapo sawa!

Kufadhili mikutano ya SADDAC, EAC, AU, huo ndo utajiri! siyo unatwambia habari ya kucheza Disco la vumbi huko Bisarye! huyo ni tajiri wa maskini usirudie kutusimulia habari za wana vijiji!! Sie humu tunawaza habari za visima vya mafuta wewe unasema VX old model mweee!! umelewa au.....

wanavijiji bana shida sana.....
 
Bwana Mrefu

JF-Expert Member
Jul 17, 2018
295
1,000
Hiyo simulizi ilishaletwa huku!
Ni kweli na ndo maana mwishoni hapo akaandika credit : 40 BYB
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom