Part II: Bado safari yangu ya kusaka utajiri wa nguvu za giza inaendelea

Status
Not open for further replies.

Aigle

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
711
6,186
Kama ambavyo awali nilikwisha jitokeza kuomba 'Connection' ya mtaalam au wataalam wa ndagu za utajiri au utajiri wa nguvu za giza.

Nasikitika kusema kuwa bado sijapata haswa sehemu ambayo mhusika anaweza kunishika mkono kunipeleka au kuwa kama 'Godfather' kuniinguza katika ufalme huo wa giza haswa kupata utajiri.

Mwanzoni uzi wangu nilishuhudia walioniunga mkono, nilipata madalali wengi, matapeli pia walikuepo, wachache walionielekeza sehemu asilimia kubwa nilikuta mtaalam amehama / kufariki kwahio kuniwia vigumu.

Najua pia ilivyo ngumu mtu kuamini haswa kwa dhati kwamba huyu mtu kweli anataka kuchukua njia hio na kupelekea hata aliyekua na connection au alie upande huo kuwa na ugumu sana kukupa connection. Wengine tu hawataki, hakuna sababu maalum lakini hawataki tu na huwezi kumlazimisha.

Mimi bado naendelea na safari yangu ya kuutafuta utajiri wa nguvu za giza au ufalme wa giza, hakuna ubaya katika hilo, ni imani kama imani nyingine, umasikini ni laana, umaskini hauzoeleki, siutaki umaskini, nimeulaani umaskini, na mpendwa wangu Lucifer alisema wazi kuwa ukinisujudia nitakupa mali zote za dunia hii, nami nataka ku claim hiyo power.

Hivyo naendelea kujitokeza kwa wale ambao wataweza kunisaidia kunipa.connection ya UHAKIKA ama kunipeleka basi waweze kunisaidia katika hilo.

Hail Lucifer!

ANGALIZO: Wale walokole na wafia dini nawaomba mtulie, siwahitaji kwenye uzi wangu.
 
Aliekuambia wanataka kutoka nani? Ulishafatwa na mmoja wao..? Nitajiskia fleshi sana.
Yupo na ni brother wangu na alishakimbilia Kanisani kuungama na alihadithia Vyote baada kutoka huko Mali zote zimepukutika lakini Hali aliyokua nayo Saa hz anafurahi kuliko alivyokua na hela halafu pesa za kishirikina Ukianza mashart madogo hila mafanikio yanavyozidi na wao wanataka zaidi
 
Lucifer anatafuta watu wa aina flani, wenye akili flani, wenye ushawishi kwenye jamii, sio kila mtu, hao wengine anawafanya vibweng'o tu na misukule inayoishi.

Hata andiko ulilolinukuu, shetani alimwambia Yesu amsujudie ili ampe Mali kwani yeye Lucifer humpa AMTAKAYE, sio amtafutae!!! Sasa we endelea kujipendekeza kwake uone atakavyoiteketeza familia yako!!
 
Kama ambavyo awali nilikwisha jitokeza kuomba 'Connection' ya mtaalam au wataalam wa ndagu za utajiri au utajiri wa nguvu za giza.

Nasikitika kusema kuwa bado sijapata haswa sehemu ambayo mhusika anaweza kunishika mkono kunipeleka au kuwa kama 'Godfather' kuniinguza katika ufalme huo wa giza haswa kupata utajiri.

Mwanzoni uzi wangu nilishuhudia walioniunga mkono, nilipata madalali wengi, matapeli pia walikuepo, wachache walionielekeza sehemu asilimia kubwa nilikuta mtaalam amehama / kufariki kwahio kuniwia vigumu.

Najua pia ilivyo ngumu mtu kuamini haswa kwa dhati kwamba huyu mtu kweli anataka kuchukua njia hio na kupelekea hata aliyekua na connection au alie upande huo kuwa na ugumu sana kukupa connection. Wengine tu hawataki, hakuna sababu maalum lakini hawataki tu na huwezi kumlazimisha.

Mimi bado naendelea na safari yangu ya kuutafuta utajiri wa nguvu za giza au ufalme wa giza, hakuna ubaya katika hilo, ni imani kama imani nyingine, umasikini ni laana, umaskini hauzoeleki, siutaki umaskini, nimeulaani umaskini, na mpendwa wangu Lucifer alisema wazi kuwa ukinisujudia nitakupa mali zote za dunia hii, nami nataka ku claim hiyo power.

Hivyo naendelea kujitokeza kwa wale ambao wataweza kunisaidia kunipa.connection ya UHAKIKA ama kunipeleka basi waweze kunisaidia katika hilo.

Hail Lucifer!

ANGALIZO: Wale walokole na wafia dini nawaomba mtulie, siwahitaji kwenye uzi wangu.
Huu muda wote unaohangaika kwa nguvu namna hii kumtafuta shetani, hii nguvu unayoitumia kumtafuta shetani ungeiweka Kwenye kutafuta Ufalme wa Mungu, nakuambia ungekuwa mbali sana.

Unamuhitaji Yesu,yeye ni jibu la mambo yote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom