chizcom
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 7,581
- 15,721
Jana Julai mosi, wananchi wa Burundi waliadhimisha miaka 60 tangu nchi yao ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Jumapili ya Julai mosi, 1962. Mwaka moja kabla ya siku ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa Umoja Mataifa na chama kilichoshinda katika uchaguzi huo UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore, aliyemuoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili.
Hata hivyo, Jumamosi ya Oktoba 13, 1962 Rwagasore aliyefikiriwa kuwa alikuwa anajenga uelewano wa kuishi pamoja kati ya Watutsi na Wahutu, aliuawa. Kifo chake kilikatisha ndoto ya shirikisho la Tanganyika na Burundi alilokuwa nalo Mwalimu Julius Nyerere.
Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9, 1961 na baadaye ikawa Jamhuri Desemba 1962. Baada ya Uhuru wa Tanganyika katika hotuba yake kwa mkutano wa mwaka wa chama cha Tanu mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alionyesha wazi kufadhaishwa kwake kulikotokana na mauaji ya Rwagasore.
Soma zaidi Gazeti la Mwananchi leo Jumamosi Julai 2,2022