Kilwa na Historia ya Kupigania Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
Naweka hapo chini makala za historia ya Kilwa nilizopata kuandika katika nyakati tofauti katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

ABDULKARIM HAJJ MUSSA, MWINYI MCHENI OMARI NA JULIUS NYERERE KATIKA KUIJENGA TANU KILWA

Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar akifahamiana vyema na Julius Nyerere.
Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar na Mwinyi Mcheni Omar ni kati ya watu waliomuunga mkono Nyerere na kasaidia sana katika kuiingiza TANU Kilwa Mtoni.

Abdulkarim akimpakiza Mwalimu kwenye pikipiki yake BSA 500 wakienda kote sehemu za Kilwa kuhamasisha watu kujiunga na TANU kudai uhuru wa Tanganyika.

Katika harakati hizi Nyerere alikuwa akifikia na kulala nyumbani kwa Mwinyi Mcheni Omari na mikutano yote ya ndani ya TANU ikifanyika katika nyumba hiyo.

Taifa lina deni kubwa sana kwa wazalendo hawa.

Hapo chini ni picha ya pikipiki aliyokuwa akipada Baba wa Taifa na nyumba ambayo alikuwa akifikia na kulala pamoja na kufanya mikutano ya ndani.

(Picha zote kwa hisani ya marehemu Abdulkarim Shah maarufu kwa jina la Bulji mjukuu wa Abdulkarim Hajj Mussa).

1707708079541.png

1707708124394.png

1707708186557.png

Siku moja Bulji kaniandikia na akanipigia simu baada ya kusoma historia niliyoandika jinsi TANU ilivyoingia Southern Province (Jimbo la Kusini) kupitia wazalendo ambao yeye wengine amewaona akiwa mtoto na akacheza na watoto wao.

Alishangaa vipi sijataja mchango wa Kilwa.

Abdulkarim akaniambia, ‘’Mwamu babu yangu Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar ambae mimi nimepewa jina lake akifahamiana vyema na Mwalimu Nyerere na ni mmoja kati ya watu waliomuunga mkono na kasaidia sana katika kuiingiza TANU Kilwa Mtoni na akimpakiza Mwalimu kwenye pikipiki yake BSA 500 wakienda kote sehemu za Kilwa kuhamasisha watu kujiunga na TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.’’

Haukupita muda mrefu Bujji akanirushia picha ya pikipiki ya babu yake aliyokuwa akimchukua Nyerere, kijiji hadi kijiji, katika miaka ile ya 1950 pamoja na picha ya nyumba ambayo Nyerere alikuwa akifikia na kulala.

Bulji akaniletea na picha ya nyumba ya Mwinyi Mcheni Omari ambae mikutano yote ya ndani ya TANU ikifanyika.

Nilimshauri Abdulkarim kuwa tupate wasaa tukae kitako tuiandike historia hii kwa utulivu na yeye awasilaine na Makumbusho ya Taifa ili ile pikipiki ya somo yake Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar ihifadhiwe kama kumbukumbu ya taifa.

Nilimweleza Bulji kuwa hivi tukifanya tutakuwa na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na pia tutakuwa na kumbukumbu ya babu yetu Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar na kila atakaeiangalia pikipiki ile na akasoma maelezo yake ataona juu au chini yake picha ya wazalendo hawa wawili zimewekwa ubavu kwa ubavu.

1707708370951.png

Kushoto ni Abdulkarim Hajji Shah (mjukuu wa Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar, Yussuf Manzi, Nusura Faraj, chini kushoto, Mshike JK na Shariff Pazi

MKESHA WA MAULID NA SAFARI YA JULIUS NYERERE KILWA 1955

John Iliffe amepata kusema kuwa historia ya TANU nyingi iko katika mikono ya watu.

Hakika maneno haya ni ya kweli wala hayana shaka.

Nimepokea nyaraka nyingi na picha kutoka kwa watu zinazohusu historia ya TANU na historia ya Mwalimu Nyerere kutoka kwa watu na sehemu ambazo sikutegemea kabisa.

Nimepokea simu kutoka kwa rafiki yangu yuko Kilwa Pande ananiambia kakutana na kijana jina lake Hassan Mtarika amekaa anaangalia video yangu moja nazungumzia historia ya uhuru wa Tanganyika.

Huyu ndugu yangu akamfahamisha yule kijana kuwa anamfahamu huyo anaemtazama kwenye hiyo video.

Hivi ndivyo nilivyokutana na huyu kijana akanipa kipande cha historia ya nyumba ya Bi. Mgumba, nyumba ambayo Mwalimu Nyerere alilala mwaka wa 1955 wakati wa kueneza TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Yule kijana akanirushia picha ya nyumba hiyo na akanipa na simu za mtu ambae yeye alikuwa kijana mdogo kiasi cha miaka 10 wakati Nyerere alipokwenda Kilwa Pande.

Huyu bwana Sheikh Suleiman Mwandu nilimpata na tukafanya mazungimzo.
Nilistarehe na nafsi yangu.

‘’Mimi nilikuwa na umri kiasi cha miaka 10 wakati Nyerere alipokuja Pande wakati wa kupigania uhuru akapokelewa na Bwana Abdul Manafi, baba yake Bi. Mgumba.

Hawa vijana wa leo wanapoieleza ile nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere wanasema kalala nyumba ya Bi. Mgumba.

Huyu Bi. Mgumba wakati ule yeye alikuwa mtoto lakini hiki kizazi cha leo wamekuta nyumba ile anakaa Bi, Mgumba kwa kuwa baba yake Abdul Manafi alikuwa keshafariki na Bi. Mgumba ambae jina lake khasa ni Halima bint Abdi Manafi ndiye akiishi nyumba ile.

Aliyempokea Mwalimu Nyerere ni Bwana Abdul Manafi na yeye alikuwa mtu akijiweza akifanya biashara ya duka hapo nyumbani kwake.

Pamoja na yeye walikuwa Khamisi Mamboya, Bakari Suleiman Mtondoo na Suleiman Shaweji ambao baadae walikuja kuwa viongozi wa tawi la TANU hapa Kilwa Pande.

Hii nyumba ambayo unayopicha yake ndiyo khasa nyumba aliyofikia Mwalimu Nyerere lakini ile ilikuwa nyumba ya makuti hii nyumba hivi sasa imeezekwa bati.

Mwalimu Nyerere aliingia na mguu wa kulia Kilwa Pande akitokea Kilwa Masoko na alikuja na boti inayoitwa, ‘’Makunganya.’’

Mtandula ndipo kilipo kivuko kuja Pande.

Hapa ilibidi nimkatishe kauli mpashaji habari wangu Sheikh Suleiman Mwandu kutaka uhakika kama nimesikia vizuri kuwa Mwalimu Nyerere kenda Kilwa Pande na boti inaitwa Makunganya.

Hassan Omari Makunganya alipigana na Wajerumani na walipomkamata walimnyonga na mnara wa kumbukumbu yake na wazalendo wengine upo Kilwa.

Hapakuwa na tawi la TANU lakini Pande kulikuwa na wanachama wa TANU waliokuwa na kadi zikiuzwa senti hamsini lakini wakizificha kuogopa serikali.
Mwalimu Nyerere aliingia Pande kwa mguu wa kulia kwa kuwa siku ile usiku wake kulikuwa na mkesha wa Maulidi, kulikuwa na Ziara ya kila mwaka ya Tariqa Qadiriyya tarehe 14 kuamkia 15 Rajab.

Mji ulikuwa umefurika watu kutoka vijiji vya jirani kuitika mwito wa Khalifa wao Sheikh Athmani Ahmed aliyechukua uongozi wa kutoka kwa Sheikh Khamis Abdallah ambae alikuwa kafariki mwaka wa 1952.

Usiku ule katika Maulid yale uwanjani kwa Sheikh Ahmed Athmani Waislam wakatangaziwa kuwa kesho Julius Nyerere anakuja Pande watu watoke kumpokea Mtandula na kutakuwa mkutano wa hadhara uwanjani kwa Abdul Manafi na Julius Nyerere atawahutubia wananchi wa Tanganyika.

Hivi ndivyo TANU ilivyobisha hodi Pande na wananchi sasa wakapata nguvu ya kuitangaza TANU.

Ikawa makarani wa kununua mbata na korosho katika kazi zao wakiwahimiza wale wanaokuja kuuza mazao yao kuwa watoe senti hamsini wakate kadi ya TANU.

Kama wanavyopenda kusema Waingereza, ‘’The Rest is history,’’ yaani yaliyobakia ni historia.

Hakika historia ya uhuru wa Tanganyika iko katika vichwa vya watu kama alivyosema John Iliffe.

Picha: Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu Manafi aliyofika Baba wa Taifa Kilwa Pande mwaka wa 1955, wa katikati ni Hassan Omari Makunganya alipokamatwa na Wajerumani.

Kaka mkubwa Mohamed, Niko dar miaka ya sabini mwishoni kutokea hapa Itumbili butosa(Buchosa). nikaona barabara inaitwa makunganya kumbe ni kumbukumbu ya shujaa kutoka kilwa!Asante Kwa kunielimisha mkubwa wangu
 
Ukiangalia kwa makini uhuru wa nchi ulianza kama harakati za kidini kutokana na nia ovu ya Berlin conference ya kuufuta uislam pwani ya Africa.
 
Historia inajifungua yenyewe,
Ni kama magofu ya kale yanavyotoa siri ya historia iliopotea.
Asante Mzee Mohammmed Said kwa juhudi zako.
Hawa tulio wajua leo ni baadhi ya walijitolea kwa hali na mali kwa ajili ya uhuru tunao ufurahia leo.
 
Ingekua sababu ni dini wa singe mkubali Nyerere na wengine.
Usiwe na ubongo butu
Sikia nikueleze mapambano dhidi ya uhuru yalikuwa na mlengo wa kidini tambua hadi wanafariki hao wakina mzee mnonji,nabidu hawakuwahi kumtambua mwarabu kama ni mmojawapo wa wakoloni..hata ukiangalia dhamira ya sheikh Suleiman Takadir ilikuwa ni islamic state na isingekuwa akili nyingi ya nyerere naye angekuwa kama Alli Bongo...muislamu wa kiafrika asieenda shule tena mwenye uarabu mpya ndani yake yeye kwake mwarabu hakuwa na kosa lolote lile hapa Tanganyika
 
Ingekua sababu ni dini wa singe mkubali Nyerere na wengine.
Usiwe na ubongo butu
Unaposema wasingemkubali Nyerere na wengine unamaanisha wengine gani wakati kila siku Mohamed anakuambia hauwezi kuzitenganisha harakati za uhuru na uislamu?
 
Naweka hapo chini makala za historia ya Kilwa nilizopata kuandika katika nyakati tofauti katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

ABDULKARIM HAJJ MUSSA, MWINYI MCHENI OMARI NA JULIUS NYERERE KATIKA KUIJENGA TANU KILWA

Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar akifahamiana vyema na Julius Nyerere.
Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar na Mwinyi Mcheni Omar ni kati ya watu waliomuunga mkono Nyerere na kasaidia sana katika kuiingiza TANU Kilwa Mtoni.

Abdulkarim akimpakiza Mwalimu kwenye pikipiki yake BSA 500 wakienda kote sehemu za Kilwa kuhamasisha watu kujiunga na TANU kudai uhuru wa Tanganyika.

Katika harakati hizi Nyerere alikuwa akifikia na kulala nyumbani kwa Mwinyi Mcheni Omari na mikutano yote ya ndani ya TANU ikifanyika katika nyumba hiyo.

Taifa lina deni kubwa sana kwa wazalendo hawa.

Hapo chini ni picha ya pikipiki aliyokuwa akipada Baba wa Taifa na nyumba ambayo alikuwa akifikia na kulala pamoja na kufanya mikutano ya ndani.

(Picha zote kwa hisani ya marehemu Abdulkarim Shah maarufu kwa jina la Bulji mjukuu wa Abdulkarim Hajj Mussa).

Siku moja Bulji kaniandikia na akanipigia simu baada ya kusoma historia niliyoandika jinsi TANU ilivyoingia Southern Province (Jimbo la Kusini) kupitia wazalendo ambao yeye wengine amewaona akiwa mtoto na akacheza na watoto wao.

Alishangaa vipi sijataja mchango wa Kilwa.

Abdulkarim akaniambia, ‘’Mwamu babu yangu Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar ambae mimi nimepewa jina lake akifahamiana vyema na Mwalimu Nyerere na ni mmoja kati ya watu waliomuunga mkono na kasaidia sana katika kuiingiza TANU Kilwa Mtoni na akimpakiza Mwalimu kwenye pikipiki yake BSA 500 wakienda kote sehemu za Kilwa kuhamasisha watu kujiunga na TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.’’

Haukupita muda mrefu Bujji akanirushia picha ya pikipiki ya babu yake aliyokuwa akimchukua Nyerere, kijiji hadi kijiji, katika miaka ile ya 1950 pamoja na picha ya nyumba ambayo Nyerere alikuwa akifikia na kulala.

Bulji akaniletea na picha ya nyumba ya Mwinyi Mcheni Omari ambae mikutano yote ya ndani ya TANU ikifanyika.

Nilimshauri Abdulkarim kuwa tupate wasaa tukae kitako tuiandike historia hii kwa utulivu na yeye awasilaine na Makumbusho ya Taifa ili ile pikipiki ya somo yake Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar ihifadhiwe kama kumbukumbu ya taifa.

Nilimweleza Bulji kuwa hivi tukifanya tutakuwa na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na pia tutakuwa na kumbukumbu ya babu yetu Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar na kila atakaeiangalia pikipiki ile na akasoma maelezo yake ataona juu au chini yake picha ya wazalendo hawa wawili zimewekwa ubavu kwa ubavu.

View attachment 2901360
Kushoto ni Abdulkarim Hajji Shah (mjukuu wa Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar, Yussuf Manzi, Nusura Faraj, chini kushoto, Mshike JK na Shariff Pazi

MKESHA WA MAULID NA SAFARI YA JULIUS NYERERE KILWA 1955

John Iliffe amepata kusema kuwa historia ya TANU nyingi iko katika mikono ya watu.

Hakika maneno haya ni ya kweli wala hayana shaka.

Nimepokea nyaraka nyingi na picha kutoka kwa watu zinazohusu historia ya TANU na historia ya Mwalimu Nyerere kutoka kwa watu na sehemu ambazo sikutegemea kabisa.

Nimepokea simu kutoka kwa rafiki yangu yuko Kilwa Pande ananiambia kakutana na kijana jina lake Hassan Mtarika amekaa anaangalia video yangu moja nazungumzia historia ya uhuru wa Tanganyika.

Huyu ndugu yangu akamfahamisha yule kijana kuwa anamfahamu huyo anaemtazama kwenye hiyo video.

Hivi ndivyo nilivyokutana na huyu kijana akanipa kipande cha historia ya nyumba ya Bi. Mgumba, nyumba ambayo Mwalimu Nyerere alilala mwaka wa 1955 wakati wa kueneza TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Yule kijana akanirushia picha ya nyumba hiyo na akanipa na simu za mtu ambae yeye alikuwa kijana mdogo kiasi cha miaka 10 wakati Nyerere alipokwenda Kilwa Pande.

Huyu bwana Sheikh Suleiman Mwandu nilimpata na tukafanya mazungimzo.
Nilistarehe na nafsi yangu.

‘’Mimi nilikuwa na umri kiasi cha miaka 10 wakati Nyerere alipokuja Pande wakati wa kupigania uhuru akapokelewa na Bwana Abdul Manafi, baba yake Bi. Mgumba.

Hawa vijana wa leo wanapoieleza ile nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere wanasema kalala nyumba ya Bi. Mgumba.

Huyu Bi. Mgumba wakati ule yeye alikuwa mtoto lakini hiki kizazi cha leo wamekuta nyumba ile anakaa Bi, Mgumba kwa kuwa baba yake Abdul Manafi alikuwa keshafariki na Bi. Mgumba ambae jina lake khasa ni Halima bint Abdi Manafi ndiye akiishi nyumba ile.

Aliyempokea Mwalimu Nyerere ni Bwana Abdul Manafi na yeye alikuwa mtu akijiweza akifanya biashara ya duka hapo nyumbani kwake.

Pamoja na yeye walikuwa Khamisi Mamboya, Bakari Suleiman Mtondoo na Suleiman Shaweji ambao baadae walikuja kuwa viongozi wa tawi la TANU hapa Kilwa Pande.

Hii nyumba ambayo unayopicha yake ndiyo khasa nyumba aliyofikia Mwalimu Nyerere lakini ile ilikuwa nyumba ya makuti hii nyumba hivi sasa imeezekwa bati.

Mwalimu Nyerere aliingia na mguu wa kulia Kilwa Pande akitokea Kilwa Masoko na alikuja na boti inayoitwa, ‘’Makunganya.’’

Mtandula ndipo kilipo kivuko kuja Pande.

Hapa ilibidi nimkatishe kauli mpashaji habari wangu Sheikh Suleiman Mwandu kutaka uhakika kama nimesikia vizuri kuwa Mwalimu Nyerere kenda Kilwa Pande na boti inaitwa Makunganya.

Hassan Omari Makunganya alipigana na Wajerumani na walipomkamata walimnyonga na mnara wa kumbukumbu yake na wazalendo wengine upo Kilwa.

Hapakuwa na tawi la TANU lakini Pande kulikuwa na wanachama wa TANU waliokuwa na kadi zikiuzwa senti hamsini lakini wakizificha kuogopa serikali.
Mwalimu Nyerere aliingia Pande kwa mguu wa kulia kwa kuwa siku ile usiku wake kulikuwa na mkesha wa Maulidi, kulikuwa na Ziara ya kila mwaka ya Tariqa Qadiriyya tarehe 14 kuamkia 15 Rajab.

Mji ulikuwa umefurika watu kutoka vijiji vya jirani kuitika mwito wa Khalifa wao Sheikh Athmani Ahmed aliyechukua uongozi wa kutoka kwa Sheikh Khamis Abdallah ambae alikuwa kafariki mwaka wa 1952.

Usiku ule katika Maulid yale uwanjani kwa Sheikh Ahmed Athmani Waislam wakatangaziwa kuwa kesho Julius Nyerere anakuja Pande watu watoke kumpokea Mtandula na kutakuwa mkutano wa hadhara uwanjani kwa Abdul Manafi na Julius Nyerere atawahutubia wananchi wa Tanganyika.

Hivi ndivyo TANU ilivyobisha hodi Pande na wananchi sasa wakapata nguvu ya kuitangaza TANU.

Ikawa makarani wa kununua mbata na korosho katika kazi zao wakiwahimiza wale wanaokuja kuuza mazao yao kuwa watoe senti hamsini wakate kadi ya TANU.

Kama wanavyopenda kusema Waingereza, ‘’The Rest is history,’’ yaani yaliyobakia ni historia.

Hakika historia ya uhuru wa Tanganyika iko katika vichwa vya watu kama alivyosema John Iliffe.

Picha: Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu Manafi aliyofika Baba wa Taifa Kilwa Pande mwaka wa 1955, wa katikati ni Hassan Omari Makunganya alipokamatwa na Wajerumani.

Dah!...,huyu Hassan Makunganya kumbe hakuwa mwarabu ?
 
Back
Top Bottom