Ni kweli Burundi ilitaka kuunganika na Tanganyika ilivyopata Uhuru na ingekuwa sehemu ya Tanganyika?

Yote Mungu ndio mpangaji...
Yaan Mungu anapanga mauwaji? Jamn mtamsingizia Mungu mpka lini?

Hiyo migogoro ilkuwa njama za wahuni wachache kwa faida zao na ndio hawa hawa wahuni wanaofaidika na migogoro ya kongo, Mungu hawezi husika ktk mateso ya watu jmn labda kama mnamuongelea huyo mungu wenu ambaye yuko limited mnaemuomba anashindwa kujibu, mungu ambaye anawaza nadharia za kipuuzi
 
Jana Julai mosi, wananchi wa Burundi waliadhimisha miaka 60 tangu nchi yao ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Jumapili ya Julai mosi, 1962. Mwaka moja kabla ya siku ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa Umoja Mataifa na chama kilichoshinda katika uchaguzi huo UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore, aliyemuoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili.

Hata hivyo, Jumamosi ya Oktoba 13, 1962 Rwagasore aliyefikiriwa kuwa alikuwa anajenga uelewano wa kuishi pamoja kati ya Watutsi na Wahutu, aliuawa. Kifo chake kilikatisha ndoto ya shirikisho la Tanganyika na Burundi alilokuwa nalo Mwalimu Julius Nyerere.

Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9, 1961 na baadaye ikawa Jamhuri Desemba 1962. Baada ya Uhuru wa Tanganyika katika hotuba yake kwa mkutano wa mwaka wa chama cha Tanu mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alionyesha wazi kufadhaishwa kwake kulikotokana na mauaji ya Rwagasore.
Soma zaidi Gazeti la Mwananchi leo Jumamosi Julai 2,2022View attachment 2280084
Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanganyika kabla eneo hilo kupewa umiliki kwa Ubelgiji baada ya ushirikia wao katika vita vya kwanza ya dunia.
Pia inasemekana Kenya ilikuwa landlocked hivyo sehemu ya Mombasa ili ipate bandari na Kenya ikatoa eneo lenye mlima Kilimanjaro, sehemu ya Arusha pamoja na ziwa Natron kwa Tanganyika kipindi hicho.
 
Kama zenji eti nayo ni nchi na inajitutumua..

Zenji ilipaswa iwe mkoa ama wilaya kama ilivyo mafia.

#MaendeleoHayanaChama
Kuna nchi, dar es salaam kama mji ni mkubwa kuliko zenyewe na ni nchi tajiri, mfano ndio washataja watu huko juu, singapore, vatican, luxermborg etc
 
Ikiwezekana tutengeneze muungano wa namna fulani kama ule wa Zanzibar tu, halafu tulichakachue Jeshi lao liwe moja and then Tujuze majeshi Burundi na silaha za kisasa.
 
Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanganyika kabla eneo hilo kupewa umiliki kwa Ubelgiji baada ya ushirikia wao katika vita vya kwanza ya dunia.
Pia inasemekana Kenya ilikuwa landlocked hivyo sehemu ya Mombasa ili ipate bandari na Kenya ikatoa eneo lenye mlima Kilimanjaro, sehemu ya Arusha pamoja na ziwa Natron kwa Tanganyika kipindi hicho.
Ruanda-Urundi (ndivyo ilivyokuwa ikiitwa) mpaka eneo la Congo zilikuwa sehemu ya utawala wa Tippu Tip wakati wa biashara ya meno ya tembo na kutafuta watumwa. Alikuja kuporwa na Ubelgiji.

10 mile coast (ukanda wa maili 10) kutoka Msumbiji mpaka Kismayuu Somalia zilikuwa chini ya utawala wa Zanzibar na ilikuja kuachiwa kwa Kenya baada ya makubaliano baina ya Mjerumani na Muingereza ya kubadilishana maeneo (soma Heligoland treaty). Wakati huo tayari Zanzibar na Tanganyika vilishawekwa kwenye himaya ya Muingereza baada ya mgawanyo wa afrika huko Berlin 1884.
 
Unajua ukubwa wa nchi Singapore ni kmsq 728.6 tu (yaani Mia saba ishirini na usheee hapo, hawana hata kilomita za mraba buku? Na population Yao Ni watu mil 5.6 huku GDP Yao Ni $340bil.

Ni shiiiiiiiiiiiiida.
Hamna nchi hapo, wilaya tu
 
Unajua ukubwa wa nchi Singapore ni kmsq 728.6 tu (yaani Mia saba ishirini na usheee hapo, hawana hata kilomita za mraba buku? Na population Yao Ni watu mil 5.6 huku GDP Yao Ni $340bil.

Ni shiiiiiiiiiiiiida.
Na mbaya zaidi kila kitu hadi maji anaimport kutoka nchi zingine
 
Na mbaya zaidi kila kitu hadi maji anaimport kutoka nchi zingine
Uzuri pesa anayo,yaani Singapore na yeye Kuna Muda akiangalia kwny ramani anakua anasema hivi inawezekanaje kunakua na nchi kubwa hivi huko dunianizenye kila kitu na bado tumemezizidi kiuchumi kwa mbali hivi.That's life.
 
Warundi ni ndugu zetu wa damu kabisa kuliko Wanyarwanda. I love these people. Hongereni sana Warundi kwa kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wenu.

Mwenyezi Mungu aendelee hivyo hivyo kuwajalia moyo wa kuwaona Watanganyika kama ndugu zenu wa damu. Hakika nyinyi ni watu msio na makuu, majivuno na kujimwambafai kama Wanyarwanda.
Kuna katibu mkuu wa Zamani wa CNDD-FDD ni mpwa wa Mustafa Nyang'anyi wa Rufiji.
 
Back
Top Bottom