Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
WANASEMA KWA KEJELI ATI NAJITIA KUJUA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
Vitabu hivi vingekeuwa vimeandikwa miaka mingi sana na waandishi na kuwa sehemu ya historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kwa nini haikuwa hivyo ni historia inayoanza mwaka wa 1962 mara tu baada ya kupatikana uhuru pale TANU ilipoamua kuandika historia yake.
Mradi huu haukukamilika.
Mwaka wa 1981 CCM ikaunda jopo la waandishi kuandika historia ya TANU.
Jopo hili lilikuwa chini ya Dr. Mayanja Kiwanuka.
Hiki hapo chini ndicho kilichotokea:
''Hassan Upeka, mmoja katika wasaidizi wa utafiti ule alipeleka katika jopo lile la utafiti na uandishi wa historia ya TANU, mahojiano aliyofanya na Abdulwahid Sykes miaka mingi iliyopita kuhusu historia ya TANU.
Hassan Upeka alifahamishwa kuwa historia inayoandikwa haimuhusu Abdulwahid Sykes.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Historia ya TANU ikaandikwa bila ya kutajwa Abdul Sykes na wazalendo wengi walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hii ilikuwa khiyana ya hali ya juu kabisa.
Matokeo yake ndiyo haya uwanja ukawa wazi na mtupu kwa kuandikwa historia hii wakati wake utakapofika.
Kama nisingenyanyua kalamu kuiandika hakika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika isingekuwapo.