Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Ni jambo lilizoeleka kwa mkaguzi mkuu na mdhibiti wa pesa za Serikali (CAG) kuibuka na ripoti kila mwaka, inayoonyesha namna mabilioni ya pesa ya walipa zinavyotafunwa na "wajanja" wachache walioko Serikalini, pasipo kuchukuliwa hatua zozote.
Lakini tunashuhudia magereza yetu, yakiwa yamefurika wafungwa, wakiwa wamehukumiwa kwa vijikesi, vidogo vidogo, kama vile wizi wa kuku!
Ndiyo hapo ninapouliza, hivi kuna sababu gani ya kutusomea hadharani ripoti hizo za CAG, kama Serikali yetu, haina dhamira ya dhati kuwachukulia hatua za kisheria?
Tumeshuhudia, makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdrahman Kinana, eti akisema, atamshairi Rais Samia, aweze kuwachukulia hatua za kisheria, wale wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo ya CAG!
Hivi umewahi kuona wapi watu waliotenda makosa makubwa kama hayo ya kutafuna mabilioni ya pesa ya walipa kodi wa nchi hii, eti mpaka Rais ashauriwe Ili achukue hatua za kisheria?
Mbona hawa wanaotuhumia kwa vijikesi vidogo vidogo, kama vile wezi wa vibasikeli, wakiwa wamejazana magerezani, wakiwa wameshahukumiwa tayari, kutumikia vifungo vyao, je na hao Rais ameshauriwa kabla ya kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa' vifungo vyao??
Huu mtindo unaotumika na Serikali hii ya CCM, ni wa hatari Sana, unaofanya upendeleo wa wazi kabisa na "kubariki" kwa kuwaona wale wezi wa mabilioni ya Serikali, kama mashujaa na kuachiwa watembee kifua mbele, wakati wezi wa vitu vidogo vidogo, kama wale wanaowakwapua vipochi kwa abiria kwenye daladala, ndiyo wahukumiwe vifungo mahakamani na watuhumiwa wengine hata wakipoteza Maisha yao kwa "kuhukumiwa' vipigo na wananchi wenye hasira kali!
Ndiyo maana nchi hii kodi zinakuwa nyingi mno, kama vile tozo mbalimbali, kwenye miamala ya simu, ambazo zinawakamua watanzania wanyonge, kumbe pesa hizo, zinaliwa na watanzania wachache, tuliowaamini na kuwakabidhi madaraka ya juu, Katika nchi hii!
Tunaomba viongozi wetu wa Serikali hii ya CCM, wawe "serious" na wachukue hatua mara moja na tuone watuhumiwa wote waliotajwa na CAG kukwapua mabilioni ya pesa ya walipa kodi wa nchi hii wanafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.