Kwanini wanaotoa ushuhuda makanisani huwa hawachukuliwi hatua za kisheria?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,373
Moja kwa moja....

Nilimsikia mama mmoja anasema katika ulimwengu wa roho amechinja wachawi karibu mia, alipewa upanga na malaika. Sasa watu mia kuchinjwa rohoni ni upotevu mkubwa wa nguvu kazi.

Mwingine unamsikia anasema walikuwa wachawi, wanasababisha ajali, wanakinga damu. Wanajinadi kuwa wameua watu wengi. Hii ni kama Genocide ukijumlisha mauaji hayo ya ajali zetu kwa mwaka.

Mwingine alienda mbali eti hadi Hayati Mkapa alipopata ajali akiwa kwake Ikulu yeye na team ya wachawi walikuwa wanapambana naye. Hii sio ajabu maana Ikulu hadi Brazili na Malawi tulishasikia hayo ya watu kupigwa kishirikina hadi kukimbia Ikulu.

Hapo achilia mbali majambazi, wauwaji na watenda maovu ya kutisha wanapotoa shuhuda zao live tena kwa kushangiliwa na hatuoni wanapelekwa Jela kutumikia kifu go cha uharifu huo wakati hawajamjua Bwana Yesu.

Najiuliza kama mtumishi

Huwa tunapangwa tu na Serikali huwa inajua na kuamua kupotezea?

Hakuna ushahidi wa kisheria kuwachukulia hatua kwenye mambo ya kiimani?

Au Serikali inatambua makanisa ni chombo saidizi cha kubadili mienendo ya jamii hivyo wanasaidiwa kazi na wachungaji

Wakuu kitaalam hii imekaaje. Au wewe ulishawahi kusikia shuhuda gani za kutisha hadi ukageuka kuona kama kuna Polisi anasikia?
 
MWENYEZIMUNGU ni mwongi wa kusamehe unapotubia bila kurudia
Hata Mahakamani unapotubia na kukili KOSA utahukumiwa kwa mujibu wa SHERIA
ndo unasikiaga kosa hili kifungo chake ni kati ya miaka 5 mpaka 10
Utaenda JELA lakini kam utaonesha TABIA njema
TEAM ya PAROLE itakuwa pamoja na wewe
Yote haya ni kutokana na NGUVU ya kutubia
 
🙏🙏
 
Kwenye sheria ya ushahidi kuna kitu kinaitwa Confession,mtu akifanya confession kanisani au kwa kiongozi yoyote wa kiimani huo ushahidi hauwezi kutumika dhidi yake.Yani hata ashike maiki kanisani atubu kwamba alikuwa jambazi akaua watu sheria haiwezi kumfanya chochote.
 
Nilimsikia mama mmoja anasema katika ulimwengu wa roho amechinja wachawi karibu mia, alipewa upanga na malaika. Sasa watu mia kuchinjwa rohoni ni upotevu mkubwa wa nguvu kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu zile shuhuda nyingine huwa zinatisha hadi unahofu, kwa kichapo hicho cha kiroho Mshana wa JF atakuwa hajachinjwa kweli hahahhah
 
Moja kwa moja....

Nilimsikia mama mmoja anasema katika ulimwengu wa roho amechinja wachawi karibu mia, alipewa upanga na malaika. Sasa watu mia kuchinjwa rohoni ni upotevu mkubwa wa nguvu kazi.

Mwingine unamsikia anasema walikuwa wachawi, wanasababisha ajali, wanakinga damu. Wanajinadi kuwa wameua watu wengi. Hii ni kama Genocide ukijumlisha mauaji hayo ya ajali zetu kwa mwaka.

Mwingine alienda mbali eti hadi Hayati Mkapa alipopata ajali akiwa kwake Ikulu yeye na team ya wachawi walikuwa wanapambana naye. Hii sio ajabu maana Ikulu hadi Brazili na Malawi tulishasikia hayo ya watu kupigwa kishirikina hadi kukimbia Ikulu.

Hapo achilia mbali majambazi, wauwaji na watenda maovu ya kutisha wanapotoa shuhuda zao live tena kwa kushangiliwa na hatuoni wanapelekwa Jela kutumikia kifu go cha uharifu huo wakati hawajamjua Bwana Yesu.

Najiuliza kama mtumishi

Huwa tunapangwa tu na Serikali huwa inajua na kuamua kupotezea?

Hakuna ushahidi wa kisheria kuwachukulia hatua kwenye mambo ya kiimani?

Au Serikali inatambua makanisa ni chombo zaidizi cha kubadili mienendo ya jamii hivyo wanasaidiwa kazi na wachungaji

Wakuu kitaalam hii imekaaje. Au wewe ulishawahi kusikia shuhuda gani za kutisha hadi ukageuka kuona kama kuna Polisi anasikia?
"WAIGIZAJI NA WASANII" WACHUKULIWE HATUA??...HAIWEZEKANI..
 
Kwenye sheria ya ushahidi kuna kitu kinaitwa Confession,mtu akifanya confession kanisani au kwa kiongozi yoyote wa kiimani huo ushahidi hauwezi kutumika dhidi yake.Yani hata ashike maiki kanisani atubu kwamba alikuwa jambazi akaua watu sheria haiwezi kumfanya chochote.
Asante sana. Ukiweka kifungu itanoga zaidi. Kuna jambazi lilipita Church usiku kuelekea kwenye timing zake, mlinzi Prayer worrier akalidhibiti kiroho usiku huohuo likapiga magoti na kukili maasi yake.

Ule ushuhuda Prayer Worrier alitulia nao hadi leo maana aliogopa wenda miongoni mwa waumini ni Mashushushu wakamtaka awaonyeshe alipo, wakati walimalizana usiku huohuo na jamaa likatokomea kusikojulikana.
 
Soma kifungu cha 27 na 28 imetaja watu wenye mamlaka ya kupokea confession ya mtuhumiwa.
IMG_1525.png
 
Soma kifungu cha 27 na 28 imetaja watu wenye mamlaka ya kupokea confession ya mtuhumiwa.View attachment 2897907
Asante sana mkuu. Elimu haina mwisho.

Vipi kama ataconfess mbele ya dunia nzima. Namaanisha Kanisani na tunamrusha Online social media zote zinafuatilia. Huoni kama anaweza kuleta taharuki ikiwa alichokisema kitaenda viral na kinagusa hisia za watu na watu wao mtuhumiwa aliyewadhuru wakati akiwa bado hajamjua Bwana Yesu vizuri.
 
Mkuu kwa mujibu wa hiyo sheria ungamo lolote nje ya hao watu waliopewa mamlaka ya ku record confession haliwezi kutolewa kama sehemu ya ushahidi,video hiyo itakayo enda viral haiwezi kutumika kama ushahidi kumbuka kazungumza hayo akiwa kanisani.

Labda akisha fanya confession kama hiyo,mamlaka husika za upelelezi zikusanye ushahidi mwingine nje ya confession yake ambao utamuunganisha kwenye hayo makosa aliyofanya alafu wataweza kumfikisha mahakamani,kumbuka jinai haiozi,kwa mantiki hiyo mahakamani watatumia ushahidi mwingine na sio confession yake ya kanisani.
 
Asante sana. Umejibu kisomi sana.
 
Back
Top Bottom