Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.

Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?

Kwanza inabidi utoe hiyo definition yako ya mjini ni wapi ambako utapata kiwanja kwa milioni tano na saizi yake ni nini? Halafu ndio urudi hapa.
 
Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.

Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?

Mi mwenyewe nataka ghorofa na lazima nijenge ni kupenda tuuuu
 
Mkuu hapana. Na material zingine tunachukua viwandani kabisa. Sishangai wewe kushangaa ama kukataa hizi gharama.

Nakumbuka enzi hizo kulikua na ugomvi wa majirani wawili. Mmoja na ghorofa mwingine hana. Na yule baba mwenye ghorofa ni engeneer. Yule wa chini ni ndugu yetu na ni wachokozi na wakorofi kwelikweli waakawa wanamtukana yile baba na kusema vibaha ghorofa lake. Nyumba ya wale ndugu zangu ni ya chini lakini kali mno. Nikisema kali ninkali. Sasa yule baba kwa hasira mwenye ghorofa akawaambia " sasa mnaongea nini wakati gharama ya nyumba yenu yote ndo msingi wa ghorofa yangu?" Nilishangaa sana watu wakanielekeza bado sikuelewa. Nilaja kufatilia kbs kwa wahusika wa kada hiyo. Na nikaona wanaojenga. Aisee... inafika. Nimeshuhudia kbs. Basi hapa namm najiliwaza nitajenga langu siku tuu

Niliambiwa watu huona gharama ni ndogo sometimes kwasababu wanajenga kwa kujibana sana na kuacha vitu vingine. Kama ulivyoona wataalam wakiainisha huko juu. Kuna mwingine anataka ujenz ule wa kufata protocols na uimara. Mwingine atapambana kwa mkono unapifikia mkuu. Ndo maana hata nyunba za chini tuu pia gharama hutofautiana.
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
 
hivi kulala juu ghorofa ya nne! ni zindiko tosha hata ndege za kichawi hazifiki hukoo, wazungu walilenga hapo!wakipanda sana ni usawa wa ghorofa ya tatu! lkn pia kuna mawimbi mengi yanawarudishaga chini! angalia hii video kwa mfano
 
mkuu
Hawawezi kuamini binafsi nilikuwa naandaa estimate ya mteja wangu, Msingi upo kwenye 42m, hata tukianza project tukajibana vipi hatuwezi kutumia chini ya 35m
uko sahihi. kuna jamaa yangu alijenga..msingi uligonga mpaka 100M. Unajua wengi wetu mawazo yetu yanaendana na vipato vyetu. kwa mwenye nazo..hiyo ni hela ya kawaida..asiye nazo..ndo hivo atakuja hapa atakwambia hiyo ni hela nyingi haiwezekani. Kikubwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake….

Kama una uwezo...ishi na kufurahia matunda ya jasho lako.
 
Dada cha kushangaza hapa Arusha hakuna kiwanja cha milion 5,labda huko ndani kijijini kabisa.
Kuna jirani yangu hapa anauza miguu kumi kwa kumi na tatu kwa milion kumi na nne. Yan ni balaa
Alipomaanisha mjini alimaanisha sehem zenye huduma muhimu sio lazima pawe mjini au manispaa.
 
mkuu

uko sahihi. kuna jamaa yangu alijenga..msingi uligonga mpaka 100M. Unajua wengi wetu mawazo yetu yanaendana na vipato vyetu. kwa mwenye nazo..hiyo ni hela ya kawaida..asiye nazo..ndo hivo atakuja hapa atakwambia hiyo ni hela nyingi haiwezekani. Kikubwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake….

Kama una uwezo...ishi na kufurahia matunda ya jasho lako.
Sahihi kabisa
 
Kijijini kwetu kuna hizo huduma zote za muhimu
Ni kijiji kwenu kwenye mabenki angalau matatu mannee au ikishindikana basi mawili..sio wakala wa benki.
Ni kijijini kwenu ambapo kuna maafisa mipango miji nk.
Kwa hilo hongera..ila sehemu kubwa ya nchi haina huduma zote muhimu.
 
mkuu

uko sahihi. kuna jamaa yangu alijenga..msingi uligonga mpaka 100M. Unajua wengi wetu mawazo yetu yanaendana na vipato vyetu. kwa mwenye nazo..hiyo ni hela ya kawaida..asiye nazo..ndo hivo atakuja hapa atakwambia hiyo ni hela nyingi haiwezekani. Kikubwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake….

Kama una uwezo...ishi na kufurahia matunda ya jasho lako.
Atleast wako ambao wana exposure zaidi. Maana kuna wengine wanaclaim ni show off. Binafsi maybe ningeambiwa bila kuona isingekua rahisi kuamini. Kila siku mpya tunajifunza jambo jipya
 
Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.

Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?

Fashion tu, kama una hela fetua usingizi wa kutosha
 
Badala ya kujenga nyumba kubwa kutapakaa eneo kubwa , ukijenga ghorofa inasaidia nafasi kubaki kwa matumizi mengine,

Pia eneo likibaki nafasi kubwa inapendeza zaidi kwa muonekano hata wakati wa kufanya shughuli za kifamilia unaweza kufanyia nyumbani kwako badala ya kwenda kukodi ukumbi kwa gharama kubwa.
 
Back
Top Bottom