Aliyevamia Kiwanja cha mwingine kwa miaka 20 Mbezi Africana avunjiwa ghorofa

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
1709316688178.png
ALIYEVAMIA KIWANJA CHA MTU AVUNJIWA GHOROFA

Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Slaa leo amesimamia zoezi la Uvunjwaji wa Nyumba ya Johnson Mahululu ambaye anatuhumiwa kujenga nyumba katika eneo ambalo halimiliki kihalali .

Waziri wa Ardhi amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa eneo hilo ni mali halali ya Bi Naomi ambaye alikuwa akihangaika kulipata eneo lake kwa zaidi ya miaka 20.

Aidha amewaonya watu wenye tabia ya kuvamia maeneo ambayo si yao, na kusema kuwa Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha inatatua kero zote za ardhi na kuwashughulikia wanaosababisha migogoro hiyo.
 
Ndio mpaka Waziri akasimamie? Au Naomi ni mchepuko wa mheshimiwa?

Waziri ameenda sababu huyo mvamizi ana kesi nyingi sana za viwanja ofisini kwake.

Maeneo ya Mbezi beach, Tegeta na bahari beach Kuna watu ni maarufu kwa kuvamia viwanja vya watu. Mfano huyo mzee mahururu na mzee Mushi.

Waziri ameona hilo jina akajua huyu mtu ni tapeli wa viwanja maarufu nisipoenda anaweza wadanganya wavunjaji
 
Waziri ameenda sababu huyo mvamizi ana kesi nyingi sana za viwanja ofisini kwake.

Maeneo ya mbezi beach Kuna watu ni maarufu kwa kuvamia viwanja vya watu. Mfano mzee mahururu na mzee mushi.

Waziri ameona hilo jina akajua huyu mtu ni tapeli maarufu nisipoenda anaweza wadanganya wavunjanji
In another words sababu anatajwa kuhusika kesi nyingi hii wamemfanya wa mfano?
 
Waziri ameenda sababu huyo mvamizi ana kesi nyingi sana za viwanja ofisini kwake.

Maeneo ya mbezi beach, tegeta na bahari beach Kuna watu ni maarufu kwa kuvamia viwanja vya watu. Mfano huyo mzee mahururu na mzee mushi.

Waziri ameona hilo jina akajua huyu mtu ni tapeli maarufu nisipoenda anaweza wadanganya wavunjanji
Huyo Mushi nimemsikia sana.
 
Back
Top Bottom