Ni kwanini kipindi cha Mfungo wa Ramadhani bei ya vyakula hupanda?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,563
Nilitegemea kipindi cha mfungo wa Ramadhani kwasababu watu hufunga kula, basi bei za vyakula zingeshuka sana na hata wafanyabiashara kukosa biashara kabisa, lakini ndio kwanza vyakula havishikiki na bei zipo juu hata zaidi ya wakati wa kawaida.

Ndio kumaanisha wakati wa mfungo watu hula zaidi ya wakati usio wa mfungo? Basi kama kuna mtu ana maelezo mazuri ya kitaalam ya jambo hili tungefurahi akatuelimisha hapa.
 
Gharama za maisha zimepanda na mfumuko wa bei uko juu wala hakuna uhusiano na mfungo, tatizo lenu mnadhani nyinyi ni watu maalum.

Wakristo wapo kwenye kwaresma Yao kimyakimya na Imani Yao Bila makelele, tatizo lipo Kwa Muslims Yani inahitajika attention ili kila mtu ajuwe kuna kufunga.

Kiti Moto haijapandishwa bei, bia hazijapanda bei wacha tuenjoy, usicomplicate.
 
Ramadhani mara nyingi hata watu wanaoishi mbali na familia zao hupenda kujumuika na familia zao hivyo kuna ulazima mkubwa wa chakula kuliwa yani futari , mfano mimi nipo nje ya nchi kwa sasa muda wa kufuturu ukinikuta popote napiga juice na mkatw na kuendelea na shughuli zangu ila nikiwa nyumbani na familia yangu siwezi kuleta usela huo.
Pili ramadhani watu wanatoa sana sadaka na kila muislamu ana hakikisha muislamu mwenzake anapata futari ukienda misikiti mingi utakuta kuna futari inaletwa watu wote wanakula , miezi ambayo siyo ramadhani kuna wanaoshinda njaa ila ni siri yao na familia zao.
Hayo ni machache ila ukichunguza utakuta kuna mengi ambayo yanaongeza demand ya chakula, jana mfano ikulu kuna wakristo na waislamu ila wamefuturu pamoja ile yote inaongeza demand ya chakula, acha maofisini ambapo kuna mazoea ya maofisi ya serikali na private kufuturisha kipindi hichi
 
1)Waislam hupungua uzito Ramadan?

2)jumla ya uzito wa chakula anachokula muislam kwenye ramadan ukilinganisha na miezi mingine. Upi uzito mkubwa?

Hayo maswali mawili yakijibiwa yanawezatoa mwanga katika swali lako
 
Wakristo 90% hawafungi kubali ukatae huo ndio ukweli angalia hata wakristo wanaokuzunguko tu eneo lako la kazi au unapoishi utapata jibu
 
Ramadhani mara nyingi hata watu wanaoishi mbali na familia zao hupenda kujumuika na familia zao hivyo kuna ulazima mkubwa wa chakula kuliwa yani futari , mfano mimi nipo nje ya nchi kwa sasa muda wa kufuturu ukinikuta popote napiga juice na mkatw na kuendelea na shughuli zangu ila nikiwa nyumbani na familia yangu siwezi kuleta usela huo.
Pili ramadhani watu wanatoa sana sadaka na kila muislamu ana hakikisha muislamu mwenzake anapata futari ukienda misikiti mingi utakuta kuna futari inaletwa watu wote wanakula , miezi ambayo siyo ramadhani kuna wanaoshinda njaa ila ni siri yao na familia zao.
Hayo ni machache ila ukichunguza utakuta kuna mengi ambayo yanaongeza demand ya chakula, jana mfano ikulu kuna wakristo na waislamu ila wamefuturu pamoja ile yote inaongeza demand ya chakula, acha maofisini ambapo kuna mazoea ya maofisi ya serikali na private kufuturisha kipindi hichi
Ahhaa haaa haaaa, manake wakati wa Ramadhani ndio watu hula zaidi kuliko wakati wa kawaida?!
 
Nilitegemea kipindi cha mfungo wa Ramadhani kwasababu watu hufunga kula, basi bei za vyakula zingeshuka sana na hata wafanyabiashara kukosa biashara kabisa, lakini ndio kwanza vyakula havishikiki na bei zipo juu hata zaidi ya wakati wa kawaida.

Ndio kumaanisha wakati wa mfungo watu hula zaidi ya wakati usio wa mfungo? Basi kama kuna mtu ana maelezo mazuri ya kitaalam ya jambo hili tungefurahi akatuelimisha hapa.
Pambano jingine hili linaanza muda si mrefu, ngoja nivute siti nifutalie taratibu
 
Ahhaa haaa haaaa, manake wakati wa Ramadhani ndio watu hula zaidi kuliko wakati wa kawaida?!
Nadhani hata wewe mkristo hapo ofisini kwenu mnafuturisha au umelikwa kufuturu sehemu , na 70% ya taasisi private na public zinafuturisha mwezi huu wa ramadhani so always the demand is going to be higher thats simple logic, wakati supply ya chakula duniani kote ikizidi kupungua kutokana na tabia nchi, vita na kadhalika
 
Lakini kuna mamilioni ya waislama wanaofunga hivyo tusingetemea kuona ndio kwanza mahitaji ya chakula yanaongezeka, kwani hao wanaofuturishwa ni wengi kuliko waislamu? Na kwamba kwani wanaofuturishwa huwa kawaida hawali? Je mabadiliko ya hali ya hewa hutokea Ramadhani tu?
 
UKweli kwamba watanzania wengi kula yao ya kuunga unga ila mwezi wa ramadhani wengi wana uhakika wa kupata futari kupitia sadaka ambayo ni wajibu kwenye mwezi huu kutoa , kama ilivyo eid ambayo watu wana uhakika wa kula kupitia zakatul fitr ambayo ni lazima kwa kila muislamu kutoa
 
Sio kwa ubaya Ila jamani ndugu zangu, sijawahi kuona mkurya muislamu nadhani hata huko Tarime hakuna miskiti.
Sijawahi kusikia Mohammed Chacha Mwita, Hasan Magesa au Jabir Wangwe.
 
UKweli kwamba watanzania wengi kula yao ya kuunga unga ila mwezi wa ramadhani wengi wana uhakika wa kupata futari kupitia sadaka ambayo ni wajibu kwenye mwezi huu kutoa , kama ilivyo eid ambayo watu wana uhakika wa kula kupitia zakatul fitr ambayo ni lazima kwa kila muislamu kutoa
Kama kuna mamilioni ya wanaofunga, tusingepaswa kuona ndio kwanza vyakula vinapanda bei.
 
mamilioni ya waislamu wanafunga na mamilioni wanafuturu waislamu na wasio waislamu huo ndio utamaduni wa mwezi wa ramadhani jana ikulu pale si uliona mchanganyiko wa kila dini wakifuturu ? Wale wengi wao siku za kawaida wengine wangekula soda na keki siku ikaenda
 
1)Waislam hupungua uzito Ramadan?

2)jumla ya uzito wa chakula anachokula muislam kwenye ramadan ukilinganisha na miezi mingine. Upi uzito mkubwa?

Hayo maswali mawili yakijibiwa yanawezatoa mwanga katika swali lako
Watapunguwa Vipi uzito wakati wengi wakati wa Ramadhan ndio wanakula zaidi?

Bila kuattack Imani ya mtu kuna ambao NI kama wanakuwa wamebadili ratiba ya Kula tu.

Sasa unaamka Saa 10 usiku near to alfajiri Kwa ajili ya daku Kwa kalenda zote za Gregorian na kalenda ya kiislamu siku inakuwa imeshabadirika hapa unakula msosi wa kushiba, sasa siku hiyo unakuwa umefungwa nini?
 
Watapunguwa Vipi uzito wakati wengi wakati wa Ramadhan ndio wanakula zaidi?

Bila kuattack Imani ya mtu kuna ambao NI kama wanakula wamebadili ratiba ya Kula Tu.

Sasa unaamka Saa 10 usiku near to alfajiri Kwa ajili ya daku Kwa kalenda zote za Gregorian na kalenda ya kiislamu siku inakuwa imeshabadirika hapa unakula msosi wa kushiba, sasa siku hiyo unakuwa umefungwa nini?
Mkuu binaadamu huwa active na kufanya shughuli zake mchana na sio usiku, na kufunga kunaendana na ibada nyingi za lazima kwa muislamu kama kusoma quran, kutoa sadaka na kuswali sala tano , hayo ya kubadilisha muda wa kuka unayaona wewe kwa upeo wako mdogo
 
Wakristo wapo kwenye kwaresma Yao kimyakimya na Imani Yao Bila makelele, tatizo lipo Kwa Muslims Yani inahitajika attention ili kila mtu ajuwe kuna kufunga.
 
Wakristo wapo kwenye kwaresma Yao kimyakimya na Imani Yao Bila makelele, tatizo lipo Kwa Muslims Yani inahitajika attention ili kila mtu ajuwe kuna kufunga.
JUst look around your christian friends uone kama wanafunga? Huwezi kuheshimiwa kama mwenyewe hujiheshimu, kwaresma haiheshimiwi kwa sababu wakristo wenyewe hawaiheshimu na kuidharau huo ndio ukweli mchungu, ndio masna hata makampuni ya wasio wislamu yanaipa kipaumbele ramadhani na kuiheshimu duniani , hata wakristo wengi wanaiheshimu ramadhani , usibishe humu just look around halafu tafakari
 
Back
Top Bottom