Ni kwanini kipindi cha Mfungo wa Ramadhani bei ya vyakula hupanda?

Nilitegemea kipindi cha mfungo wa Ramadhani kwasababu watu hufunga kula, basi bei za vyakula zingeshuka sana na hata wafanyabiashara kukosa biashara kabisa, lakini ndio kwanza vyakula havishikiki na bei zipo juu hata zaidi ya wakati wa kawaida.

Ndio kumaanisha wakati wa mfungo watu hula zaidi ya wakati usio wa mfungo? Basi kama kuna mtu ana maelezo mazuri ya kitaalam ya jambo hili tungefurahi akatuelimisha hapa.
Ni ishara kuwa kuna familia zinataabika wakati usio wa mfungo hivyo huwa zinaahirisha kutumia baadhi ya bidhaa
 
Kwa hiyo wakati wa mfungo ndo watu hujirusha zaidi?
 
Nilitegemea kipindi cha mfungo wa Ramadhani kwasababu watu hufunga kula, basi bei za vyakula zingeshuka sana na hata wafanyabiashara kukosa biashara kabisa, lakini ndio kwanza vyakula havishikiki na bei zipo juu hata zaidi ya wakati wa kawaida.

Ndio kumaanisha wakati wa mfungo watu hula zaidi ya wakati usio wa mfungo? Basi kama kuna mtu ana maelezo mazuri ya kitaalam ya jambo hili tungefurahi akatuelimisha hapa.
Ni kweli mwezi wa Ramadhani watu hufunga kwa kutokula na kunywa kuanzia inapoingia alfajiri mpaka jua linapozama(magharibi). Badda ya hapo waliyofunga wanaruhusiwa kula na kunywa wakati wote huo wa usiku ambapo milo yao hugawanyika katika sehemu kuu mbili, ya kwanza ni futari na ya pili ni daku. Kwenye futari mara nyingi hupikwa vyakula vya aina mbalimbali kulinganisha na daku ambayo watu wengi hupendelea wali na mchuzi. Kwa kweli kwa mazingira yetu, vyakula vinaliwa sana kwenye mfungo wa Ramadhani kuliko nyakati zingine, kuna baadhi ya watu ambao wamekunjuliwa riziki zao huwa wana tabia ya kufuturisha watu katika mwezi huu wa Ramadhani na wengine huwa wanapika chakula kingi na kugawa kwa majirani au kubadilishana vyakula, ambapo miezi mingine utaratibu huu unakuwa haupo. Na kwa kuwa uhitaji wa vyakula unakuwa mkubwa na bei inapanda ikiwa usambazaji hauongezeki.
 
demand ikiongezeka halafu supply ikawa ni ile ile au ikashuka kidogo basi inasababisha scarcity au uhaba wa huduma au bidhaa husika,na kwa vyovyote vile Lazima gharama au bei ya bizaa hiyo itapanda tyuuuu 🐒
 
Ufungaji mwingi sio Kufunga kupunguza Idadi ya Chakula unachokula bali ni kubadilisha Ratiba ya Kula..., Badala ya kula Mchana unakula usiku....

Kwahio kwa matumizi bado ngoma draw tena watu katika ile futari wanakula hata zaidi ya walivyokuwa wanakula wakati wanabangaiza (Kupiga Pasi Ndefu)
 
JUst look around your christian friends uone kama wanafunga? Huwezi kuheshimiwa kama mwenyewe hujiheshimu, kwaresma haiheshimiwi kwa sababu wakristo wenyewe hawaiheshimu na kuidharau huo ndio ukweli mchungu, ndio masna hata makampuni ya wasio wislamu yanaipa kipaumbele ramadhani na kuiheshimu duniani , hata wakristo wengi wanaiheshimu ramadhani , usibishe humu just look around halafu tafakari
🚮🚮🚮
Huna hoja,subiri saa 12 ifike ukale msikitin🤣🤣
 
MAkafir mna shida sana yani mnaona wivu hadi wenzenu wakifunga aise
 
Ni kweli mwezi wa Ramadhani watu hufunga kwa kutokula na kunywa kuanzia inapoingia alfajiri mpaka jua linapozama(magharibi). Badda ya hapo waliyofunga wanaruhusiwa kula na kunywa wakati wote huo wa usiku ambapo milo yao hugawanyika katika sehemu kuu mbili, ya kwanza ni futari na ya pili ni daku. Kwenye futari mara nyingi hupikwa vyakula vya aina mbalimbali kulinganisha na daku ambayo watu wengi hupendelea wali na mchuzi. Kwa kweli kwa mazingira yetu, vyakula vinaliwa sana kwenye mfungo wa Ramadhani kuliko nyakati zingine, kuna baadhi ya watu ambao wamekunjuliwa riziki zao huwa wana tabia ya kufuturisha watu katika mwezi huu wa Ramadhani na wengine huwa wanapika chakula kingi na kugawa kwa majirani au kubadilishana vyakula, ambapo miezi mingine utaratibu huu unakuwa haupo. Na kwa kuwa uhitaji wa vyakula unakuwa mkubwa na bei inapanda ikiwa usambazaji hauongezeki.
Inaonekana waziwazi wakati wa Ramadhani ndo vyakula vinaliwa zaidi ya wakati mwingine. Sasa mfungu una maana gani hapa?
 
Hapo ina maana nzuri kwamba kipindi cha ramadhani waislamu wanatoa sana sadaka kulisha wenye uhitaji waislamu na wasio kuwa waislamu , nadhani hata weww mleta mada una machimbo yako ya kupata futari pamoja kwamba hufungi
 
Ufungaji mwingi sio Kufunga kupunguza Idadi ya Chakula unachokula bali ni kubadilisha Ratiba ya Kula..., Badala ya kula Mchana unakula usiku....

Kwahio kwa matumizi bado ngoma draw tena watu katika ile futari wanakula hata zaidi ya walivyokuwa wanakula wakati wanabangaiza (Kupiga Pasi Ndefu)
INaonyesha kabisa huna hata elimu basic ya science, binaadamu hawezi kula zaidi ya uwezo wake wa kula hata awe na njaa vipi , punguzeni basi ujinga
 
Inaonekana waziwazi wakati wa Ramadhani ndo vyakula vinaliwa zaidi ya wakati mwingine. Sasa mfungu una maana gani hapa?
Kufunga ni mchana tu, jua likizama kula na kunywa ni ruhusa.
 
INaonyesha kabisa huna hata elimu basic ya science, binaadamu hawezi kula zaidi ya uwezo wake wa kula hata awe na njaa vipi , punguzeni basi ujinga
Unajua hata Kusoma ? Rudia nilochosema na wewe ulichojibu nadhani utajishangaa mwenyewe.... (mimi nimese haya)

Ufungaji mwingi sio Kufunga kupunguza Idadi ya Chakula unachokula bali ni kubadilisha Ratiba ya Kula..., Badala ya kula Mchana unakula usiku....

Kwahio kwa matumizi bado ngoma draw tena watu katika ile futari wanakula hata zaidi ya walivyokuwa wanakula wakati wanabangaiza (Kupiga Pasi Ndefu)

By the way uwezo wa kula wa Binadamu ni kiasi gani, according to your basic science ?
 
Nilitegemea kipindi cha mfungo wa Ramadhani kwasababu watu hufunga kula, basi bei za vyakula zingeshuka sana na hata wafanyabiashara kukosa biashara kabisa, lakini ndio kwanza vyakula havishikiki na bei zipo juu hata zaidi ya wakati wa kawaida.

Ndio kumaanisha wakati wa mfungo watu hula zaidi ya wakati usio wa mfungo? Basi kama kuna mtu ana maelezo mazuri ya kitaalam ya jambo hili tungefurahi akatuelimisha hapa.
Ujafanya uchunguzi kwanza chakula gani kilicho panda bei?viazi vitamu kwa sasa Tanzania nzima vinatoka runzewe na bukori nenda mabibo temeke Buguruni ukajionee fungu mzigo sh buku mzigo wa viazi tofaoti na miezi

Haya nenda mahaka ya ndizi ukashudie magali kutoka Tukuyu kagera Kisaki moro za sh 5000 watu 10 wanakula

Magingibi kidogo yamekufa na maji mwaka huu lakini miaka mingine mwezi wa mfungo uozea sokoni Mabibo kwa kukosa wanunuzi

Haya mihogo kutoka mkulanga kama yote na kutoka mkata fungu la 2000 watu 5 wanakula

Nyamba bei bado ni hile hile sh 8000 kwa kilo kuku bei hile hile njegele bei hile hile maharagwe njugu karanga kunde mahindi ndio ya mepolomoka mpaka sh 400 kwa kilo

Nyaya ziko juu tangu mwaka jana mwezi 9 vituguu maji navyo viko juu sababu ya mvua vimezidiwa na maji sio funga

Mchele bei bado nizile zile 2500 3000 mpaka 2200 pia mchele mpya umeanza baadhi ya maeneo

Sukari kabla ya ramadhani iko juu unapo sema viakula viko juu ulitakiwa kufafanua miezi ilio pita na sasa hili tulinganishe

Ingawa wakulima upandisha bei ya baadhi ya mazao matokeo yake wafanya biasha ununua na kukutana sokoni na kuzika mitaji yao sababu kila mtu udhani atapiga bao chungu mosi na chungu pili ifahamike biashara ambayo uleta usumbufu ni mali mbichi
 
Gharama za maisha zimepanda na mfumuko wa bei uko juu wala hakuna uhusiano na mfungo, tatizo lenu mnadhani nyinyi ni watu maalum.

Wakristo wapo kwenye kwaresma Yao kimyakimya na Imani Yao Bila makelele, tatizo lipo Kwa Muslims Yani inahitajika attention ili kila mtu ajuwe kuna kufunga.

Kiti Moto haijapandishwa bei, bia hazijapanda bei wacha tuenjoy, usicomplicate.
Wakati muingine unajizuia kusema sababu unaonekana kuchukia sana waisilamu,muulizaji kauliza kupanda kwa viakula wewe unakuja na makadiliko yako juu ya waisilamu utafanyaje sasa na waisilamu wapo na watazidi kuwepo hii nchi ni yao mwisho utaugua ugonjwa wa kiharusi bule
 
Back
Top Bottom