KWELI Ni hatari kiafya kulala muda mfupi baada ya kula

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Haya mambo yasikie tu, watoto wetu siku za shule huwa wanalazimishwa kulala tu punde wamalizapo kula. Hii ni hatari kwa mujibu wa tafiti za afya. Uelewa mdogo na kutojali kwa wazazi kunaweza kupelekea watoto wetu kupata madhara hapo mbeleni.

Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii si nzuri kiafya, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wansayansi wa chuo kikuu cha Loannina Medical watu wanaosubiri kulala kwa muda kidogo mara baada ya kula wana nafasi ndogo ya kupata ugonjwa wa mshtuko na hii ndio sababu inashauriwa kukaa masaa mawili mara baada ya kula ndipo kulala.

1709074481007.png
 
Tunachokijua
Kulala ni hali ya kupumzika ambayo mwili hupitia mara kwa mara kila siku, kwa kipindi fulani. Wakati wa kulala, mwili na akili hupumzika, na mchakato wa kurejea kwenye hali yake bora hufanyika.

Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa kulala ni muhimu sana kwa afya ya mwili na akili, na inasaidia katika kuboresha kumbukumbu, na ustawi wa mwili wa binadamu kwa ujumla. Wakati wa kulala, mwili unajirekebisha na kujenga upya tishu za mwili, wakati akili inapumzika na kusafisha taka za kemikali zilizojikusanya wakati wa mchana.

Kumekuwapo na tabia za baadhi ya watu katika jamii yetu kulala punde tu baada ya kumaliza kula. Kama anavyoeleza mleta mada hii, watu wengi hasa wazazi/ walezi wa watoto wadogo huwalaza watoto wao punde tu baada ya kuwalisha chakula.

Hata hivyo mleta mada hii amedokeza kuwa kuna tafiti ambazo zimefanya uchunguzi kuhusu athari za kulala muda mfupi baada ya kulala na kugundua kwamba kitendo cha kula punde tu baada ya kulala ni hatarishi kwa Afya.

Upi uhalisia kuhusu hoja hii?
Katika kupata uhalisia wa hoja hii JamiiCheck imepitia kurasa mbalimbali za Wataalamu wa Afya ili ufafanuzi wa kina. Aidha, vyanzo vyote vilivyopitiwa vinakubaliana kuwa ni hatari kiafya mtu kulala punde tu anapomaliza kula.

Mathalani ukurasa wa Afya unaoitwa VerywellHealth.com wameandika makala yenye kichwa chenye mtindo wa swali kikihoji Je, ni vibaya kulala punde tu baada ya kupata chakula?. Makala hiyo inajibu swali hilo kwa kufafanua athari anazozipata mtu anayelala muda mfupi baada ya kula. Sehemu ya makala hilo inaeleza:

Wakati unapoenda kulala, mwili wako unajikita katika kupumzika na kujiweka sawa na si kumeng'enya chakula. Kula kabla ya kulala au usiku kunaweza kuvuruga mchakato wa umeng'enyaji, kusababisha usumbufu, matatizo ya tumbo, na kuharibika kwa kimetaboliki. Kadri muda unavyosonga, hii inaweza kuchangia kuongezeka uzito na hali zingine za kiafya zinazohusiana.
Nao, Ukurasa wa Afya wa OnlymyHealth, unafafanua namna tabia ya kuzoea kulala muda mfupi baada ya kulala kunavyoweza kuchangia mwili kutengeneza uzito uliopitiliza. Zaidi ya hayo, andiko hili linaeleza kiwango cha chakula ambacho mtu anapaswa kula kiafya ambapo linashauri watu kuepuka kula vyakula vizito wakati wa usiku ili kuupa mwili nafasi nzuri ya kupumzika.

Wakielezea hoja hii OnlymyHealth wanafafanua:

Kula mlo mzito kabla ya kulala usiku si jambo la kupendekeza," anasema Dk. Raj, akiongeza kwamba kuna ushahidi wa kisayansi wa kutosha unaopendekeza kwamba kula mlo mkubwa kabla ya kwenda kulala kunaweza kusababisha madhara na hatari za kiafya kama vile kuongezeka kwa uzito, kusumbuka katika usingizi, kichefuchefu, na kiungulia.

Kwa upande wao, HealthFoundation wanaeleza kuwa kula chakula karibu sana na wakati wa kulala kunaathiri umeng'enyaji wa chakula pamoja na kuleta shida ya Kiungulia. Wanaeleza kuwa, kiungulia hutokea wakati asidi ya tumboni inaporudi kwenye mrija unaounganisha kinywa na tumbo.

Hivyo, kutokana ufafanuzi huo wa Wataalamu wa Afya JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa kulala muda mfupi baada ya kula ni hatari kwa afya ina ukweli. Hata hivyo, wataalamu wanapendekeza kuwa mtu anapaswa kulala angalau baada ya saa mbili baada ya kula chakula cha usiku ili kuepusha madhara haya yaliyobainishwa na kurasa za Wataalamu wa Afya hapo juu.
Ni kweli sio baada ya kula tu hata baada ya kunywa maji hautakiwi kulala muda huo huo unatakiwa ukae at least nusu saa,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom