Ni dhambi kupromote umasikini misikitini/makanisani

Ni dhambi kupromote umasikini misikitini/makanisani

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,462
Reaction score
23,247
Adam na Eva waliumbwa na kuwekwa kwenye mazingira ya utoshelevu. Kama haitoshi Mungu aliwawekea akiba kubwa ya Dhahabu (Dhahabu ya Havira) na vito ili viwasaidie watakapoongezeka.

Bustani ya Eden hapakuwa mahala pa kimasikini. Eden maana yake ni protected place of pleaseure (Sehemu ya Starehe/Furaha inayolindwa ).

Mafunzo MENGI ya Mungu KWA waisrael yaliweka wazi KUWA umasikini wa mali na kipato ni matokeo yasiyohepukika ya ukiukwaji wa kanuni tajirishi za Mungu. (Torati 8, 28).

UMasikini ni ubinafsi, Mtu yeyote anamcha Mungu lazima ajitahidi apate zaidi ya mahitahi yake ili awe msaada KWA wale ambayo wamechagua KUWA masikini KWA hiyari au KWA kujisababishia. Wale wahusika asioupinga bali wanautetea na kuukumbatia KWA kuutafutia vifungu.

Hivyo makanisa na misikiti yawqfundishe waumini KUWA na vipato zaidi ya mahitahi yao.

Tanzania ni masikini KWA sababu ya mafundisho potofu ya kidini yanatohamasisha na kutetea umasikini wa mali na kusisitiza utajiri wa kiroho.

Ni hayo tu.
 
Tanzania ni masikini KWA sababu ya mafundisho potofu ya kidini yanatohamasisha na kutetea umasikini wa mali na kusisitiza utajiri wa kiroho.💪🏿👌🏿
 
Hapa naungana nawe mtaalam, unaambiwa toa yote, mara utajiri wa dunia hauna thawabu
Yesu alimwambia Petro atalipwa hapahapa na vya mbinguni atakula. Vya mbinguni SIO mbadala wa ZAWADI zetu hapa duniani.
 
Back
Top Bottom