Ni bora CHADEMA ifutwe

Ni bora CHADEMA ifutwe

Kutokana na yaliotokea na ambayo yanaendelea kutokea nnaiomba serikali kwa kuangalia sheria zinavyoelekeza kuhusu uwepo wa vyama ambavyo vinawagawa watanzania, vinachochea uvunjifu wa amani, udini na ukabila kuwa ni vyama visivyohitajika tanzania

kwa hio nnaomba kama mwananchi mwenye mapenzi ya nchi yengu chama hiki kifutiwe usajili na viongozi wake wakumbane na mkono wa sheria

Ulikuwa wapi 'CCM' waliposababisha mauaji na wakimbizi Pemba? Au Vasco da Gama anadhani tumesahau?

Iweje kila CCM wanaposhindwa ndo yanatokea mauaji!
 
OOOOOOOOH GUYS,, :hungry: THIS MAN WHO POSTED THE TOPICS ANAFIKIRI WE LIKE SUCH CCM WE TIRED FOR EXPLOITATION WE NEED RIGHT TOWARDS OUR OWN LIFE....SASA YEYE HAS LIFE GIVEN BY CCM THATS WHY ANATAKA CDM IFUTWE MY FRIEND UR STILL ASLEEP WHILE US WE WAKED UP WE DONT WANT TO BE RULED OUT LIKE CUF. MTAISHIA KUSHIND KIUJANJA UJANJA KILA SIKU. WANASEMA MAENDELEA HAYAJI KWA BAHATI MBAYA LAZIMA WATU WAJITOE MUHANGA...NDIO CHADEMA YENYEWE... POLE SANA FOR FEW SUPPORT. TEHE TEHE TEHE.

Nimekipenda kiingereza chako mkuu, hata flow yako ya mawazo inaonyesha wewe ni kijana msomi!!!!!!!!! kweli CDM inasapotiwa na vijana wasomi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Umesahau wana watu zaidi ya mil 2.2(jumlisha uchakachuaji??)?? Hahaha unataka nchi ifumuke nini?? Maana sasa ndio tutajua kuhesabu wafuasi kwa kutumia kidole tuu.. Kila nyumba itaulizwa jumlisha kituo cha oysterbay(ambacho Slaa alipata kura 58 na JK 54)... Watu walijua pale ndo wasaliti kumbe weee nchi nzima hahawawataki CCM... Mkwere kapata pwani tuu na Unguja kwishnei.....

Ulitaka msimamo wa aina gani?? kama Ivory coast au?? Mi hata sikuelewi maana hujui tume ilifanya nini siku ile?? CHADEMA walipewa mill 66 kila mwezi kuanzia 2005/10 lakini wamepanda wafuasi kutoka 6% to 26%.. Hao CUF unaosema walikuwa wakipata mill 99 lakini uliza walitoka wapi kwenda wapi kama sio 11% to 8% ooh shame on Lipumba bora arudi Stanford atufundishe uchumi tuu siasa kipaji sio bahati!!!

Wao(CUF) walikubali mshindi huku wakidai tume sio huru...nafuu CHADEMA wanajua wanachokifanya .. wametoka bungeni na hisia za katiba mpya na tume huru zikaingia... Lakini CUF wamedandia mada kama wanaharakati uchwara waliojaa tanzania....
CUF ina wabunge 2 na wengine zanzibar... Lakini CHADEMA ina wabunge 23 huku kwetu Tanganyika.. Labda kakigute Zanzibar na CUF kifutwe huku Tanganyika..

Nawasilisha

The count is now minus two voters and the count is on. How many corpses will it take to make CDM a party with leaders who have sober mind? when Slaa comes to power the party flag will all be red!
 
katika watu waloishiwa hoja na hawajui ni nini wanaongea hapa tanzania wewe ni mmojawapo, utaropokaje bila kuweka vipengele vya sheria na kusimamia hoja yako ukawashawishi watu? nani siku hizi anasoma sentnsi kama hii ya kwako na kuifanyiakazi? wa wapi wewe upo dunia gani au upeo wako una kikomo cha kuanzisha mada nzito kama hizi/ nyamaza tu kama huna la kuongea bwana
 
hivi we mwiba nadhaniulikua unaandika hiyo comment akatibado una matongotongo kichwani hebu toa tongotongo kijana kumekucha tayari......................umegundua kua bila kujipendekeza CCM huwezi pata hela la wizi enh?
 
Bila shaka umechanganyikiwa. Nyerere alitabiri kuwa CHADEMA ni chama mbadala
Baba wa Taifa alipofariki Chadema ilikuwa haipo ? Nyerere alimwita Seif Sharif Hamad Butiama wakafanya private masungumso ,hakuna kiongozi yeyote yule aliewahi kufanya masungumso ya siri na Mwalimu au yupo ? Sema basi kama ni Slaa ,Slaa amevamia mambo ya watu lakini nakuhakikishieni kabisa hawezi hawezi hawezi kufanya kazi ya siasa ,ataulisha watu kwa maelufu ,na nyie angalieni kauli zake hata macho yake yanaashiria ubabe.Na ndio huyo kishawasukuma watu bila ya mpango !
 
Fikiri kwanza itakusaidia kupunguza kuzomewa kila ukisimama na hihs ndo tatizo linalokusumbua, mimi sio mganga ni mwanasaikolojia.
 
Baada ya kupoteza dira na mkondo wa siasa za kidemokrasia, na dhamira halisi ya kuwepo upinzani, chadema kimepoteza uhalali wake wa kisiasa hivyo hakuna sababu kuwapo katika daftari la msajlli wa vyama vya siasa Tanzania, hivyo kifutwe!

Nasema hivyo kwa sababu chadema baada ya kukubali mtego wa CCM wa kupenyeza mamluki ndani ya chama chao wakiwamo magwiji wa usalama wa taifa wastaafu (Mabere N. Marando), pamoja na magwiji wa siasa za kipropaganda kutoka CCM (John M. Shibuda), hakina tena ile rangi yake ya siasa za upinzani.

Akina Marando wanafanya kazi yao ndani ya chadema, ya kushawishi vurugu makusudi ili kuharibu muelekeo wa chadema ulionza nao, naye ameshafanikiwa hilo, kama alivyofanya na kufanikiwa akiwa ndani ya NCCR-Mageuzi, yeye na Agustino Mrema.

Maoni yangu, chadema kifutiliwe mbali, tayari kimeshajionyesha au kimeshafanywa kijionyeshe kuwa hakitaki siasa za ushindani bali vurugu na kuleta machafuko nchini.

Mbali na kugeuzwa huko kwa hila za makusudi, chadema kimegeuka na siyo chama cha matumaini kwa wantanzania kama kinavyojidai, au kinavyodanganya wananchi, kwani ndani ya dhamira za baadhi ya viongozi wao ni kukifanya chama kuwa mtaji wa kukuza vitega uchumi vyao na kujipatia fedha tu.

Chama kinachojiita, au kinacholazimisha kuwa ni chama rasmi cha upinzani bungeni hali ya kuwa hakiwakilishi jiografia ya upinzani wa Tanzania, hakiwezi kuwa na uhalali wa kusimama na kujiita chama cha kitaifa, hivyo kifutwe!

Wakati bunge la Tanzania lina vyama vingi na wabunge wa vyama kutoka maeneo tofauti, chadema kama chama rasmi cha upinzani bungeni kinawakilisha majimbo kinayoyaongoza tu, katika serikali yao kivuli, wakati wananchi wa maeneo mengine ambao wamechaguwa upinzani pia hawana uwakilishi wowote ndani ya serikali kivuli ya chadema.

Kwa maana hiyo basi chadema wamepoteza uhalali wa kuwa chama cha kitaifa, hivyo Kifutwe!
 
Wishful thinking....keep on dreaming dude...may be...aaaaaaaaaaand may be ...!
 
Ninaheshimu sana mawazo yako ila naona kama yana sura ya kutaka kuchokonoa zaidi(provocative) kuliko mtazamo halisi.
 
Madikteta wote wana tabia ya kutotaka kupingwa; wao ni wa kupongezwa tu. Ukimpinga Dikteta kwa jambo lolote basi anafuta maisha yako. Amin, Bokassa, Ghadaffi,..........., ***CCM***
 
Kufuta chadema ni sawa na kusema tu edit katiba yetu turudie mfumo wa chama kimoja - wote wanaunufaika na ufisadi wa CCM na Serikali yake hawapendi upinzani kwani wanajua mabadiliko yoyote yanaweza kuwanyima ulaji.

Hoja za kuifauta CHADEMA mlizozitoa ni hafifu sana na CHADEMA inapanda juu kila kukicha na itawanyima usingizi na kadri mnavyozidi kuiandika kwenye vyombo vya habari na hapo zote hizi ni njia za kuipaisha juu.

Boss wenu anasema haongei na vyama vya msimu - sasa mbona kaongea kuhusu CHADEMA - Maji ku shingo...

FANYENI KAZI MLIZOZIOMBA...... KULALAMIKA NI DALILI NA UONGOZI DHAIFU.
 
Baada ya kupoteza dira na mkondo wa siasa za kidemokrasia, na dhamira halisi ya kuwepo upinzani, chadema kimepoteza uhalali wake wa kisiasa hivyo hakuna sababu kuwapo katika daftari la msajlli wa vyama vya siasa Tanzania, hivyo kifutwe!

Nasema hivyo kwa sababu chadema baada ya kukubali mtego wa CCM wa kupenyeza mamluki ndani ya chama chao wakiwamo magwiji wa usalama wa taifa wastaafu (Mabere N. Marando), pamoja na magwiji wa siasa za kipropaganda kutoka CCM (John M. Shibuda), hakina tena ile rangi yake ya siasa za upinzani.

Akina Marando wanafanya kazi yao ndani ya chadema, ya kushawishi vurugu makusudi ili kuharibu muelekeo wa chadema ulionza nao, naye ameshafanikiwa hilo, kama alivyofanya na kufanikiwa akiwa ndani ya NCCR-Mageuzi, yeye na Agustino Mrema.

Maoni yangu, chadema kifutiliwe mbali, tayari kimeshajionyesha au kimeshafanywa kijionyeshe kuwa hakitaki siasa za ushindani bali vurugu na kuleta machafuko nchini.

Mbali na kugeuzwa huko kwa hila za makusudi, chadema kimegeuka na siyo chama cha matumaini kwa wantanzania kama kinavyojidai, au kinavyodanganya wananchi, kwani ndani ya dhamira za baadhi ya viongozi wao ni kukifanya chama kuwa mtaji wa kukuza vitega uchumi vyao na kujipatia fedha tu.

Chama kinachojiita, au kinacholazimisha kuwa ni chama rasmi cha upinzani bungeni hali ya kuwa hakiwakilishi jiografia ya upinzani wa Tanzania, hakiwezi kuwa na uhalali wa kusimama na kujiita chama cha kitaifa, hivyo kifutwe!

Wakati bunge la Tanzania lina vyama vingi na wabunge wa vyama kutoka maeneo tofauti, chadema kama chama rasmi cha upinzani bungeni kinawakilisha majimbo kinayoyaongoza tu, katika serikali yao kivuli, wakati wananchi wa maeneo mengine ambao wamechaguwa upinzani pia hawana uwakilishi wowote ndani ya serikali kivuli ya chadema.

Kwa maana hiyo basi chadema wamepoteza uhalali wa kuwa chama cha kitaifa, hivyo Kifutwe!

Mimi ni mwanachama wa CCM toka mwaka 1987, ni kiongozi ndani ya CCM katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza hapa JF nimechukizwa na hii Post haiwatendei haki CHADEMA, so far sijaona kosa walilofanya mpaka wafungiwe na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi CCM tuwe wa kweli wananchi wamechoka na ubabaishaji wetu chini ya huyu kiongozi wetu wa kitaifa tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

Natofautiana sana nawewe kwa hii thread
 
Ikiwa Chadema imeshindwa na ustaarabu bora Msajili akifute Chama hiki,chama ambacho kinashindwa kujidhibiti na kuwezaa kufuata mkondo wa kisiasa,kwa nini hawaiangalii CUF wapi imetoka na wapi ipo ,hii leo !!

Mimi nawashauri Chadema wasitishe kuingia kwenye Bunge mara moja,nawahakikishia serikali itabadili muelekeo ,ni lazima itabadili muelekeo na vile vile lile lengo la kutomtambua Kikwete kama Raisi halali au alieshinda kihalali, hapo hapana ubishi ni lazima CCM na serikali yake ikae sawa na ni njia moja ya kidemokrasia kabisa.

Lakini kuwarubuni wananchi wakati mnaingia bungeni na kula na kusaza ,hili halikubaliki kabisa kisha kutaka kuwaburuza wananchi kwenda kuchezea maji ya washawasha ,nyie wabunge mnakuwa tandize na majokofu ya jumba la bunge,huo utakuwa utapeli kushinda wa mafisadi,amueni moja tuwafahamu.

waache tu kwani kazi za midomo ni kusema tu, Na kelele za mlango hazimzuilii mwenye nyumba kupata usingizi wake.

Ile kama wataleta za kuleta kutaka kuleta machafuko na kuvuruga amani nguvu zza dola zitaaangukia kwa kishindo chote mpaka wajute kuzaliwa. wanatakiwa wajue kuwa nchi inaendeshwa kwa utawala wa sheria na sio vurugu
 
Mimi ni mwanachama wa CCM toka mwaka 1987, ni kiongozi ndani ya CCM katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza hapa JF nimechukizwa na hii Post haiwatendei haki CHADEMA, so far sijaona kosa walilofanya mpaka wafungiwe na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi CCM tuwe wa kweli wananchi wamechoka na ubabaishaji wetu chini ya huyu kiongozi wetu wa kitaifa tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

Natofautiana sana nawewe kwa hii thread

Brilliant post, nimeipenda kwa transperency yako.
 
Back
Top Bottom