Kujirudi kwa CHADEMA kwashangaza! Wengi wahoji huenda ni mbinu za Mbowe kuzima makombora ya Sumaye?

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
KUAPISHWA KWA RAIS MLISUSA, RAIS ALIPOZINDUA BUNGE MKASUSA, SHEREHE ZA KITAIFA MNASUSA, MAENDELEO YA NCHI MNAPINGA, KULIKONI MSHIRIKI SHEREHE ZA UHURU?

Nimepokea kwa mshangao mkubwa kuhusu tamko la Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa viongozi wake wa kitaifa wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe, watahudhuria sherehe za kitaifa za Uhuru wa Tanganyika 09th Dec,2019 zinazotarajiwa kufanyika kikanda kwa mara ya kwanza Mkoani Mwanza.

Nasema, nimepokea tamko hilo kwa mshangao kwa sababu, kwanza sikuamini iwapo ni kweli limetolewa na Kamati kuu ya Chadema, lakini pia sikuamini kwamba kuna wakati shetani anaweza kujigeuza kuwa malaika. Hii ni kwa sababu shetani kamwe hajawahi kuzaliwa upya bali shetani ni yule yule, na kinachobadilika kwake huwa ni mbinu za uadui anazozitumia pindi anapotaka kumwangamiza mwanadamu. Kuna wakati anaweza kujigeuza kuwa katika umbo la nyoka, simba, chui na wakati mwingine hata kudiriki kuonyesha kwamba anayo tabia ya matendo mema sawa na malaika wakati si kweli.

Ni jambo la kushangaza kwamba, Chadema waliosusia sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli tarehe 05th Nov,2015 pale Uwanja wa Uhuru na kueleza kwamba, hawamtambuwi kama Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kwa kushinda kupitia uchaguzi, leo ndiyo wanasema wako tayari kuhudhuria sherehe za Uhuru, kwa maana wawe karibu au waketi jukwaa moja na Rais wasiyemtambua? Hili halikubaliki.

Ji jambo la kushangaza kwamba, Chadema waliosusia hotuba ya Rais wakati akizindua Bunge tarehe 20th Nov,2015 Jijini Dodoma, ambapo kupitia hotuba ile ndipo watanzania tumeweza kuona mwelekeo wa taifa tulilonalo kwa sasa na siku za usoni, eti leo ndiyo wanadai wako tayari kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Tanganyika (Tanzania)? Hii haikubaliki.

Ni jambo la kushangaza kwamba, Chadema waliosusia sherehe za kitaifa kwa miaka minne mfululizo ikiwemo ya Uhuru ambayo ni miongoni mwa tunu za kitaifa, leo ndiyo bila aibu wanasema wapo tayari kushirikiana na Rais? Haiwezekani.

Ni jambo ya kushitua kwamba, Chadema ambao wanapinga kila kitu yakiwemo maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa miaka minne mfululizo kama vile miradi mikubwa ya kiuchumi, ununuzi wa ndege, elimu bure, maji, afya, umeme vijijini, mikopo vyuo vikuu, barabara, fly over, mazao ya wakulima, eti leo ndiyo wanataka kuwa karibu na Rais? Haiwezekani.

Ni jambo la kufikirisha kwamba, Chadema waliodiriki hata kumzushia Rais wa nchi kifo kutokana na uadui walioujenga kwake, na hawajamwomba radhi kwa kitendo hicho, eti leo ndiyo wanataka wakakae jukwaa moja na Rais? Haiwezekani.

Ni jambo la kushangaza kwamba, Chadema wanaoshiriki ndani na nje ya nchi kulihujumu taifa dhidi ya vita vya uchumi ikiwemo kushirikiana na mabeberu kukamata rasilimali zetu (ndege) ili kudhoofisha jitihada za nchi kujikomboa kiuchumi, eti leo ndiyo wanataka wakakae jukwaa moja na Mzalendo wa nchi, mtetezi wa taifa, mtetezi wa wanyonge. Hii haikubaliki.

Ni jambo la kushangaza kwamba, Chadema kupitia Tundu Lissu walivyozunguka dunia nzima kuishitaki serikali, kuombea nchi mabaya ikiwemo kunyimwa misaada ya maendeleo kutoka nchi wahisani, mikopo pamoja na kuitangaza nchi vibaya kuhusu kukiuka haki za binadamu na utawala bora, eti leo ndiyo wanataka kukaa jukwaa moja na Rais wanayemwita dikiteta. Hilo haliwezekani.

Ni jambo la kushangaza kwamba, Chadema wanaokesha na kushinda mitandaoni wakimtukana Rais wa nchi kwa utovu wa nidhamu uliovuka kiwango cha maadili, ndiyo sasa wanataka kukaa jukwaa moja na Rais wanayemtukana kutwa mara tatu kama vile wanatoa dozi kwa mgonjwa wakati Mwenyekiti wao Mbowe yupo na jajawahi kukemea uovu huo. Hii haikubaliki.

Kwa maoni yangu ili tamko la Chadema kushiriki sherehe za uhuru liweze kueleweka kwa Watanzania kwamba lina nia njema, viongozi wa Chadema wangeanza kutekeleza masharti yafuatayo:-

Kwanza, wamtambuwe Rais Magufuli kwamba ni Rais halali aliyechaguliwa kidemokrasia na si vinginevyo.

Pili, watambuwe na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi hususani katika swala la kufufua uchumi wa nchi, kuwaletea wananchi maendeleo.

Washiriki kwa vitendo vita dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na kushiriki vita vya uchumi kwa kutoshirikiana na mabeberu wa nje.

Waache kumtukana Rais ikiwa ni pamoja na kumwomba msamaha, kuwaomba msamaha watanzania kutokana na uovu waliofanya kwa nchi hii.

Watamke hadharani kwamba, kuanzia sasa watafanya siasa za ushindani kwa njia ya kistaarabu, kwa kuheshimiana, kwa kushindanisha sera na hoja badala ya matusi na kwamba kiongozi wao au mwanachama wao atakayekwenda kinyume, Chama kitamchukulia hatua za kinidhamu mara moja.

#MUHIMU: Iwapo Chadema haitatimiza masharti haya, kwa unyenyekevu mkubwa, naviomba vyombo vya dola visiruhusu viongozi wa Chama hiki kumsogelea Rais wetu mahali popote atakapokuwa. Kama mbwai na iwe mbwai tu, hakuna namna.
 
Wanapinga ila wanakubali kiaina..

Na ukweli usio na shaka ni kuwa Mh. Raid amefanya na bado anatenda kwa vitendo ahadi zake.

Ni punguwani pekee atakae pinga juhudi hizo..

Heko, VIVA Magufuli
 
Umepangilia vizuri na nakshi pointi zenu. Unaonaje kesho Mtafuteni Mbowe pale uwanjani au baada ya pale mummweke kati na hizi point, huku mkirusha Live hewani? Si live coverage itakuwepo na nyie mna uwezo wa kufanya hiyo kitu./.
 
Yote uliyoyataja sijaona uhusiano wake na sherehe za uhuru. Raisi hawezi kua mkubwa zaidi ya uhuru wa nchi, kitendo cha kutokumtambua raisi huwezi kihusianisha na sherehe za uhuru wa nchi hata siku moja, Raisi atakuja na kupita lakini hizo kumbukumbu zitaendelea kuwepo. Kama walikua hawashiriki huko nyuma hizo ni ratiba zao na matumizi ya uhuru wao like wise kama wameamua kushiriki kwa sasa.
 
Siku ya uhuru ina uhusiano gani na siasa😂 watu wajinga jinga mbona sana siku hizi kuna Mtanzania ambaye hapendi uhuru wa nchi yetu kwasababu ya vyama.viongozi , chaguzi na vyama vitapita lakini siku ya uhuru itakuwa palepale
 
Eti tutawazuia! Leteni shobo zenu za kuwa nyanyapaa mbele ya hao wanaowalisha na kuwapa mpaka vidoge vya ARV huku mnawaita mabeberu muone mtakavyo shukiwa kama mwewe!

Chadema wasipokuwepo kwenye sherehe mnalialia, wakija mnaogopa kama kundi la mabikira lionapo madume yanavua nguo.

Mlishaona Uhuru day kama ccm day? Shubamit! Nasikia nusu uwanja unajaa peoples, na mtu wenu akileta maneno yake ya shobo sijui vijembe ni full kuzomewa.
Tuheshimiane
 
Mimi ningependa kupatiwa uthibitisho kuwa huwa wanaalikwa na wanakataa mialiko. Kutokuwepo eneo la tukio, sio uthibitisho walikataa kuwepo.

Kwa jinsi ulivoandika ni kama ulipenda wasiwepo na sasa unapenda kuwe na masharti ya kuhalalisha kudhuria kwao. Unataka mambo mengi ambayo ukiyapindua huenda ndio yalifanya au wasihudhurie kwa mialiko au wasihudhurie kwa sababu hawakualikwa!
 
Yote uliyoyataja sijaona uhusiano wake na sherehe za uhuru. Raisi hawezi kua mkubwa zaidi ya uhuru wa nchi, kitendo cha kutokumtambua raisi huwezi kihusianisha na sherehe za uhuru wa nchi hata siku moja, Raisi atakuja na kupita lakini hizo kumbukumbu zitaendelea kuwepo. Kama walikua hawashiriki huko nyuma hizo ni ratiba zao na matumizi ya uhuru wao like wise kama wameamua kushiriki kwa sasa.
A County is not a Company
 
"Last kicks of the dyeing horse" CDM wanajua kua mwisho wao wa kuwa chama kikuu cha upinzani upo karibu, hivo wanataka poo na JPM RE:ruzuku.
Vise versa, mashariti ya wafadhili na watoa mikopo kwa serilkali lazima kwanza ccm na opposition waridhiane, LA sivyo sgr na sligler zitakwama.
 
Selikali za kiafrika zinaingia madarakani kwa figisu, Leo hii hata ulimuuliza Lubuva ni chama gani kilishinda uchaguzi 2015 hajui

Unashabikia ccm huenda unanufaika kwa namna moja au nyingine, sisi tusio na vyama tunaiona ccm inazidi kutudidimiza kiuchumi, kijamii na kisiasa

Miaka 4 sasa hakuna kitu mmefanya mnaweza tuonyesha story ni zile zile tu ndege, sgr, Stifler's, msichojua ni kuwa watu wanahitaji matokeo kwenye maisha ya mila Sikh

Ni kitu gani kitanishawisi Mimi mfanyabiashara niwaunge mkono ikiwa napambana na mlima wa kodi kandamizi?

Je makundi mengine kwenye jamii yananufaikaje na uwekezaji wenu ?
 
Binafsi nashangazwa Na uwezo mdogo Wa mtoa mada kuchambua vitu, hivi unahusishaje sherehe za Uhuru Wa taifa letu Na utendaji Wa rais jpm? Sherehe hizi Ni za watanzania wote.
Hata uchaguzi wa serikali za mitaa ni wa watanzania wote
 
Back
Top Bottom