Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178


Wanabodi,

Kama kawaida yangu, japo mimi ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, naomba kutoa ushauri huu wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba yetu, haki hiyo ilifutwa kwa tangazo la rais Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa, japo ni kinyume cha katiba!, lakini rais Magufuli ana mamlaka yote ya kuzuia jambo lolote kwa Maslahi ya taifa hata kama jambo hilo limeruhusiwa na katiba, hivyo zuio la rais Magufuli kwa mikutano ya kisiasa, japo ni zuio linalokwenda kinyume cha katiba, na ni zuio batili, maraisi wote duniani wanaruhusiwa kufanya ubatili wowote in the name of national security concerns, wana tap simu za watu, wana intercept letters na kuingilia mawasiliano, wa teams za ma snipers, sharp shooters, hivyo wale 'jamaa zetu', wa covert operation wana weza kumshoot yoyote anaye pose threats to national security, hivyo Magufuli ndio Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, kila atakalosema, automatically linakuwa ni sheria na linafuatiwa na utekelezwaji tuu hata kama ni kinyume cha Katiba, mpaka pale vyombo vyenye uwezo wa kumdhibiti rais, vitakapo mdhibiti. Vyombo hivyo ni Bunge na Mahakama!.

Hivyo alichokifanya rais Magufuli kizuia mikutano ya vyama, japo ni ni udikiteta of the highest nature na highest stages, lakini as long as amefanya kwa nia njema, then rais Magufuli is doing the right thing, although in a wrong way!.

Dawa pekee ya kuzuia udikiteta huu sio maandamano, bali ni kutumia legal redress kwa Chadema kufungua shauri Mahakama Kuu, kuomba rasmi tafsiri ya kisheria ya katazo la rais kwa kutumia kitu kinachoitwa prerogative orders kinachoombwa kupitia Judicial Review.
Hizi Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.

  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment.
Hivyo nawashauri kwa dhati kabisa Chadema, udikiteta haupingwi kwa maandamano, kama Chadema mnajipenda, tafadhalini sana msiandamane, sitisheni hayo maandamano, na badala yake undeni jopo la wanasheria nguli, mfungue shauri mahakamani, badala ya kuwasumbua wanachama na wafuasi wenu kuandamana for nothing, kwa sababu kwenye mazingira haya kama ya udikiteta fulani, kutumia maandamano kupinga kuvunjwa kwa katiba, ni nothing!, mtaachieve nothing, na sana sana mtaishia kuumizwa na kuwaumiza wanachama, wapenzi na wafuasi wenu kwa kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, utaumia!. Na sio tuu mtu huyo ana nguvu zaidi yako, bali tayari, umeishajua pia kuwa ana hulka ya udikiteta, na ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!. Tangu rais Magufuli ameingia madarakani, ameisha onyesha kwa kauli za maneno na matendo kuwa kwake katiba sio kipaumbele chake, hivyo sio kitu kivile!, it is nothing.

Dawa ya mtu wa aina hii ni kuitumia katiba kumfanyia checks and balance kwa kuomba tafsi rasmi mahakamani, akumbushwe kuwa nchi haindeshwi kwa matakwa binafsi ya mtu, bali inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni kama zilivyoainishwa kwenye katiba. Rais Magufuli atakumbushwa kuwa, kwa vile aliapishwa kuifuata, kuilinda, kuitetea na kuitekeleza katiba ya JMT, then ni lazima akiheshimu kiapo chake, kinyume cha hapo ni udikiteta tuu, japo udikiteta wake ni udikiteta Mzalendo, a benevolent dictatorship!.

The Doctrine of Separation of Powers With Checks and Balance.
Nchi yetu ina mihmili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii yote mitatu, ina nguvu za mamlaka sawa zinazojitegemea, bila kuingiliana, (powers), lakini nguvu hizo zinatenganishwa ili nguvu ya mamlaka moja isiingilie nguvu ya mamlaka nyingine, (separation of powers), huku kila mhimili ukiwa ni mwangalizi na mlinzi wa mhimili mwingine usivuke mipaka ya nguvu na mamlaka yake, kwa kufanya checks and balance, yaani ku act as a watchdog wa muhimili mingine.

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa The Executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlature, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote ina mamlaka na hakuna mhimili wowote unaopaswa kujiinua juu Zaidi na kuwa na mamlaka kuu kuliko mhimili mwingine in theory, lakini kiukweli in practical, mhimili wa The Executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa The Executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!. Rais anaingilia Bunge, Bunge lipo na linaingiliwa huku linatazama tuu na linanyamaza, hili ni Bunge gani kama sio Bunge Butu?!, rais anaingilia mhimili wa Mahakama, Mahakama ipo na ina meno, lakini haiwezi kung'ata, hii ni Mahakama gani kama sio Mahakama Kibogoyo?, ila yote ni tisa kumi ni sisi wananchi, ndio wenye katiba, ndio tuliomuajiri rais Magufuli awe rais wetu kwa kura zetu, hivyo sisi ndio mabosi wake!. Serikali ipo kwa ajili yetu, Bunge lipo kwa ajili yetu, na mahakama ipo kwa ajili yetu, ila nasi kwa sababu hatujui wajibu wetu, nasi tupo tuu tumenyamaza tunaangalia!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, na kinyume cha kanuni ya the separation of powers kwa kuiamumuru mihimili ya Bunge na Mahakama kufanya hiki au kile, wakati mihimili hiyo ilipaswa kuingilia kati kwa kuicheck serikali kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is eveything, the big boss and he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!". Njia pekee kuzuia uvunjwaji huu wa katiba ni kupitia mahakama.

Udikiteta wa Magufuli ni Dikiteta Mzalendo, A benevolent dictatorship
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana mswalie Mtume, ila dikiteta Mzalendo anayefanya udikiteta kwa nia njema, na tangu alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo wabunge na watumishi wa bunge, wakiwemo majaji na watumishi wa mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kibali cha kutimiza wajibu wao!, huu sui tuu ni udikiteta, pia ni udhalilishaji wa bunge na mahakama!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executive, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais kuwa ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!, na badala yake waitumie mahakama kutoa tafsiri ya katazo la rais na sio kushindana nae au kutaka kupimana naye kwa kutunishiana msuli!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...


Dawa ya Udikiteta

Dawa pekee dhidi ya Udikiteta ni kupitia a legal redress kwa kufungua shauri mahakama kuu itoe tafsiri rasmi ya kisheria kama rais anavunja katiba au laa, kama amevunja katiba, then mahakama kuu kupitia prerogative orders, inamuamuru rais kwa kumlazimisha lazima afuate katiba, hivyo analazimishwa kufuta tamko lake, apende asipende, atake asitake, katiba ndio iko juu ya kila kitu, hata rais wa JMT, yuko chini ya katiba!.

Kama Chadema wanavyojinasibu wana wanasheria manguli, huo unguli wao kwenye sheria ni unguli wa kwenye nini kama serious issues kama hizi za kukiukwa kwa katiba, wanazipinga kwa maandamano na mikutano?!. Sio kila kitu kinapingwa kwa maandamano, na mikutano ya hadhara. Kuna wakati CHADEMA mnahamasisha maandamano ya kijingajinga. Sometimes Chadema wawe wanachukua ushauri kwa wenye busara wao kabla hawajafanya maandamano. Sikumbuki ni lini Moshi wamewahi kuandamana. Hii maana yake Ndesamburo ni miongoni mwa wenye busara wachache ndani ya Chadema. Sikumbuki kuwahi kumuona Ndesamburo, Prof. Beregu, Prof. Safari na Mzee Victor Kimesera wakishiriki maandamano yeyote zaidi ya yale ya Arusha. Hivyo sio kila kitu ni maandamano tuu!.

Uzuri wa Magufuli na Udikteta Wake.
Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli, japo ni dikiteta kweli na amevunja katiba kuzuia mikutano ya hadhara, yeye sio mwanasheria, hivyo baada ya kuchaguliwa rais, anajua yeye ndio kila kitu!, wala hajui kuwa mamlaka yake yana mipaka, hajui kuna vitu anaweza kufanya na kuna vitu hawezi, yeye anajua maadam ameshinda urais, na yeye ndio rais, hivyo anajiamini kyeye ndio kila kitu na anaweza kufanya chochote!, hivyo amefanya hayo ya nia njema, na dhamira safi hivyo ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Paskali
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
 
Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.
Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"

Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.
He should be careful of what he wish for!
 
Naisikitikia serikali kwa kujiingiza katika confrontation zisizo za lazima, kwa sababu katiba na sheria za nchi zinaruhusu mikutano ya kisiasa ya chama chochote chenye usajili nchini kufanya mikutano ktk mikoa yote ya nchi!. Hili liko wazi na wala siyo hisani ya mtu yoyote kuguarantee haki hii

Sheria haijasema walioshinda peke yake ndo wafanye mikutano katika majimbo yao.

Kwa jinsi ninavyoona, iwapo Watu wataandamana na ikatokea nguvu kutumika hadi kupoteza maisha ya wananchi, basi kuna hatari watu kupelekwa katika vyombo vya kimataifa kama the Hague kujibu mashtaka, kwa maana wananchi hao wanadai kilicho haki kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa kuhusu haki ya kufanya mikutano!
 
Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.

Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"


Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.

He should be careful of what he wish for!
Acha mikwara Ben umeshaambiwa kaandamane na usisahau kukaa mbele kabisa ya maandamano ukione chamtemakuni
 
Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.

Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"


Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.

He should be careful of what he wish for!
Uzuri wa kitu ninachopenda kwa Magufuli....atafanya anachokisema,hana msalia mtume kwa vichwa maji na wenye viburi na alishasema ana mkataba wa miaka mitano na wananchi wake tu basi.....sasa nyie Warombo mnataka mkaandamane kahama huku majimbo yenu yako salama tu
 
Onyo la Jana linawatosha ila mwenye kuzalau mwiba mguu wake ukimharibikia ni shaur yake mwenyew.hata vitabu vya dini vimenena kabisa zieshimuni mamulaka za dunia sasa kama chadema wao siasa zao ni kupimana na dola haya sasa kazi kwenu nahis sasa mmempata wa saizi yenu.maana mnajifanya wajuaji sana
 
Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.

Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"


Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.

He should be careful of what he wish for!
Unadhani yule sawa na Zitto ? kijana umelewa sifa eeh, tarehe mosi kesho kutwa.
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom