Ni asili ya Uislaam kutii mamlaka ila sio uchawa

Ni asili ya Uislaam kutii mamlaka ila sio uchawa

Hii JF inaanza kuwa cha hatari wabaguzi wamehamia humu, na siku serikali ikifunga huu mtandao mmiliki wake asijeanza kulialia wana uwezo w kuchuja threads wakazuia hizi za kibaguzi
Unanijibu mimi au?

Maana kama ulinikusudia mimi sioni wapi nimembagua mtu labda unionyeshe wewe nilipoonyesha ubaguzi.
 
Hivi kiislamu mwanamke kuwa raisi,kiongozi mkuu juu ya jamii pana kama tunavyoona hapa nyumbani ni sahihi?
SI SAHIHI...NDIO KAWA SASA... SHERIA YETU YA KIISLAMU HAITUTAKI KUMUASI...KWA SABABU ATATUMIA MAPUNGUFU YAKE KUWAUMIZENI...CHA MSINGI KUWA NA SUBRA MPAKA PALE ALLAAH AKIAMUA VINGINEVYO...
 
Basi tusitumie uislaam wake kumhukumu...
Hakuna anartumia uislam kum hukumu mkuu,hata na mimi ni muslim kama wew au yeye but kwenye fact na ukweli she is not good enough kukaa hapo….analeta maafa makubwa mno .
 
Uislaam unatufundisha waumini wake kutii mamlaka hata kama aliyepata mamlaka hayo hakustahili...au ameyapata mamlaka hayo isivyostahili...madhali amekuwa KIONGOZI...NA MAMLAKA YAPO MIKONONI MWAKE...NI WAJIBU WETU SISI WAISLAAM KUTII MAMLAKA HAYO.

Hata kama kuna wakati utakuwa unaonewa...ila tumeamrishwa kutotoka nje ya utiifu wa kiongozi.

Pamoja na hayo, HATUJARUHUSIWA KUMTII KIONGOZI kwenye jambo linalohusu KUMUASI ALLAAH MUNGU WETU...

Vilevile dini yetu haitaki UNAFKI useme Nyeupe mdomoni, hali ya kuwa nyeusi MOYONI, au USIFIE MAASI YA KIONGOZI ILI KUTETEA MASLAHI YAKO BINAFSI(UISLAAM HAURUHUSU UCHAWA)...

YAANI TUMEAMBIWA NA MTUME WETU MUHAMMAD SWALALLAAHU ALAYHI WA SALLAM KUWA..."SEMA AU FANYA JAMBO ZURI LINALOHITAJIKA, UKIONA HUWEZI PIGA KIMYA."

Naamini wengi wetu tungepewa mamlaka haya haya waliopewa viongozi hawa...mngefanya hivi hivi au zaidi kwa yeyote anayehatarisha mamlaka yako.
Nadhani kuna pahala hujui.
Nchi nyingi za kasikazini mwa Afrika ni za waislamu asilimia kubwa,lakini hawatii mamlaka hadi mapinduzi wanafanya.
Kama unamaanisha waislam wa Bakwata sawa
Huko Saudia watu wananyongwa kila uchao kwa kuikosoa serikali,Iran ndiyo kabisaaa.
Waislamu wa Bakwata sawa!
 
Ungekuwa na akili kidogo japo ya kuvukia barabara, ungejua kuwa kuifungia JF hawawezi.
Hii JF inaanza kuwa cha hatari wabaguzi wamehamia humu, na siku serikali ikifunga huu mtandao mmiliki wake asijeanza kulialia wana uwezo w kuchuja threads wakazuia hizi za kibaguzi
 
Back
Top Bottom