Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Huyu rais ni genius sana..na kubwa anawaelewa watanzania kuliko wanavyojielewa..anajua watanzania hawawezi kujiongoza wenyewe kwa utashi wao ndio maana akitokea hata mwanasiasa akasema huyu mtu ni mchafu mzomeeni, watu watamzomea na kesho akigeuka na kusema huyu ni msafi mlambeni miguu watu wanalamba..
Maana yangu ni hii rais alizuia uuzaji wa chakula Nje ya nchi..watu wenye akili ndogo yaani upinzani wakashauti sana..ooh mipaka ifunguliwe,.genius katika ubora wake akaaema haya ngoja tuone,uzeni..watu wakauza chote.. Haijapita hata miezi sita eti wakiongozwa na hao hao waliowashawishi wauze wanalia njaa..ajabu wanapaza sauti eti rais atangaze njaa..kweli magufuli aliona mbali..ndio maana huwa tunasema nchi hii hatujapata mwanasiasa ila tumempata Kiongozi na ndio maana tunaunga mkono jitihada za kupiga marufuku mikutano uchwara ya siasa..
mvua haijanyesha jibaba.jaribu kutumia akili kidogo
 
Mie binafsi nakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa hapa nchini hakuna njaa. Tanzania ni moja wapo za nchi ambazo mwenyezi Mungu ameipa kila aina ya neema lakini watu wake hawataki kuitumia ipasavyo kwa sababu ya kutotaka kufanya kazi haswa za kilimo.

Leo nchi kama Misri yenye idadi ya watu karibu Milioni 100 wanaishi kwa kutegemea kilimo cha umwagiliaji kutoka mto Nile inakuwaje hapa Tanzania tuna maziwa na mito mengi mbali mbali na mvua kunyesha mara kwa mara tunashindwa kuwa na chakula na kusingizia njaa?

Sasa hivi tuna kiongozi asiyekuwa mnafiki anachowaambia watanzania ni ukweli mtupu na inatakiwa mkubaliane na ushauri wake kwamba kuna wafanyabiashara na wanasiasa wanajaribu kutengeneza hili suala la njaa kwa manufaa ya kujipatia umaarufu wa kisiasa na faida ya kibiashara.
Kuna nafasi gani utenguzi umetokea ili uteuliwe kwa kuwa nakuona huna kazi. Kuwa na maziwa na mito mingi hakupelekei wananchi kutopatwa na njaa. Kule kwetu Mara tuko pembezoni mwa ziwa pia kuna MTO Mara lakini si maeneo yote ya Mara yako Karibu na ziwa au MTO kuwa wachote maji na waendeshe kilimo cha umwagiriaji. Inahitajika kuandaliwa mazingira kama vile kusambaza mambomba ya maji ili wananchi wajishughulishe na hicho kilimo unachodai. Pia siyo kila ardhi anastahili kwa kilimo cha umwagiriaji. Mkoa kama wa mara kuna ardhi kidogo sana kwa ajili ya kilimo. Emu chukulia familia yenye watu 10 kuwa na shamba lenye ukubwa wa ekari 5 na ardhi imechoka. Ndugu upumbavu huu unaoandika haukubaliki ni lazima serikali iwajibike kuwanusuru watu waliokumbwa na baa la njaa.
 
Watu wafanye kazi mkuu, hivi unadhani hata serikali ikiamua kutoa misaada ya chakula kila kaya inapata kiasi gani? Hakitazidi debe tano, sasa hizo debe tano zikiisha wanaenda wapi?
Watanzania kwa bahati mbaya tulizoea vibaya sana akili za utegemezi na kulaumu laumu kila kitu.
Magufuli kaza Uzi tu, next time watu watalima chakula kitaozea kwenye maghala

Njaa ya familia yako sio hoja ya msingi sana kwa serikali, watu wanafanya uzembe kila kitu ili mwishoni walaumu serikali.

"Poor minded people will always blame politicians for their own problems "
Fanyeni kazi watanzania, acheni maneno ya wanasiasa, hata kama chakula kimepungua serikali haiwezi kuwalisha ninyi nyote, tuna uchumi gani wa kulisha nchi nzima hata kwa wiki mbili? Wanasiasa wanawadanganya oooh serikali haiwajali wananchi wake wakati wa njaa sasa hao wakiingia madarakani wataweza kuilisha nchi hii hata wiki mbili in case kuna njaa?
Ni kweli sisi bado ni maskini wa vipato, tusikubali kua maskini wa akili, kukaa tunalaumu laumu kila kitu, igeni mifano ya wachaga wao wanachakarika, wakati nyie wengine mnalialia wao magari yanaongozana kwenda Moshi kusheherekea Christmas sasa wao wako Tanzania gani? Au wote ni wapiga dili?

Fanyeni kazi bhana
It's not about being fed by the government mkuu, what we have lost is hope, there are no medicines in hospitals, employment for the newly qualified young people is questionable. We never asked for draught neither Mr President but the little we expected from him is words of encouragement.
 
Hakuna haja kuwapa maneno matamu, kawambia ukweli ulio mchungu, ukizungumzia ajira hilo ni tatizo la dunia nzima siyo Tanzania peke yake, serikali haina uwezo wa kumuajiri kila mhitimu.
Dawa hospital ni suala ambalo linafanyiwa kazi na serikali lakini pia hata sisi watanzania tulioajiriwa huko hospitali tunaiba dawa na kuziuza ili mwisho wa siku tuseme hakuna dawa, mkuu waafrika tuna akili za ajabu sana unaweza kua unatibiwa kwa Bima, ukienda hospital na Bima yako wahudumu wa Afya wanakuona kama unatibiwa bure kisa hutoi Pesa ambayo ingepitia mikononi kwao ingewapa ulaji, hapo lazima utajibiwa hakuna dawa ila mtu akija na Pesa cash anapewa dawa,
Mambo mengine sio rais anasababisha ni sisi wenyewe hatutaki kubadilika
 
Kwanini vitu kama hiyo Bima ya afya na wizi wa dawa mahospitalini visiwe highlighted na kila mtu kuwajibishwa. Ninauhakika wafanyakazi watakao shitakiwa kwa wizi wa dawa na habari kuwekwa kwenye luninga na magazeti vitawapa wengine fundisho na woga wa kuwa na work ethics. Hii ndiyo sababu kazi nyingi za wizara ya afya ni wito. Unapowaweka vijana wenye akili timamu na elimu wakiwa hawana cha kufanya huoni kuwa ni fuel ya mambo kama yaliyotokea Egypt?
 
Ivi mnaosema ukame wa mwaka huu ndio umeleta njaa ina maana mwaka jana watu hawakupata chakula? Na kama mvua ingewahi kunyesha toka mwez wa kumi na moja ina maana mahind,viaz au maharage vingekuwa vimeshaiva mwez huu wa kwanza? Chakula cha mwaka jana chote walichovuna kiliishia wapi kwa wakulima hawa?..tunalalamika kuna njaa kwa sababu hatujui kufanya bajeti ya mwaka ya chakula katika familia pamoja na kuweka akiba ya ziada....mwacheni aziweke sawa saikolojia zetu ili mwakani tujue nini maana ya kuweka akiba ya chakula kwa ajili ya dharula...kuna watu huwa wanapata sana mavuno mazur ila wakiona kuna bei nzur wanauza hadi akiba ya chakula wakitegemea mvua itawahi kunyesha na baadhi ya vyakula vitawahi kukomaa mashamban, mvua ikichelewa sasa vilio.........MAGUFULI ANACHEZA NA SAIKOLOJIA!
 
Uchaguzi uligharimu pesa kuliko ulivyopangwa na ilisababisha hazina kufagiliwa period.
 
Wanafki UvCCM na Eti hamna njaa wakati hata wazazi wao huko kijijini wakipiga simu kuomba hela wanasema hali ngumu,njaa mpaka mjini ila wao wanakanusha kwa wananchi wa kawaida.
Hili suala haliihitji kupigiwa kengele,kama mtu anasema hama chakula,ngombe wanakufa unatka nn zaidi,Shibe mwana malevya,Aliyeshiba na kufanya shoppong mlimani city huku akila kuku chips na Soda baridi hawezi jua kuna mtu kule msoga hajala siku ya tatu,wanaume ndoa zinavunjika maana hamna tena nguvu ya kugegeda(mjomba hasimami)
 
Jamani njaa ni matokeo,tuamue kuibadilisha kwa kukubali kufanya kazi kwa bidii na kujituma," Jembe halimtupi mkulima"- Hii ina maanisha kila mmoja akifuata anachosema Rais na kuamua kufanya kazi kwa bidii,mambo yatabadilika,na pia kila mtu apande mti hata mmoja basi mwaka huu ili kuivuta mvua,kumbuka sisi ndio tunahitaji miti na uoto asili,lakini uoto asili hautuhitaji sisi,kwa sababu tumekuwa waharibifu sana.Huyu Rais wetu anatutoa kwenye comfort zone ili tufanye kazi kwa weledi na bidii,kuna watu wanaishi jangwani na wanaendelea mbele hawalalamiki,hata serikali ikisema itoe chakula nani apewe na mpaka lini watoe,tumuombe Mungu atupe chakula na hakika hakuna atakayekufa kwa njaa.Mungu ibariki Tanzania na bariki viongozi wake wote na watu wake wote.Amen
 
Kiilimo Kwsnza na matokeo makubwa ( Big Results Now) vimeishinda serikali mkulima je mkulima mwenyewe atafiika wapi? Kokote kwenye miundombinu ya umwsgiliaji hakuwezi kuwa na njaa. Kwingine maji yanapita mito imechimbika kiasi cha hata kuyachoya kwa ndoo haiwezekani!
 
Kwanini vitu kama hiyo Bima ya afya na wizi wa dawa mahospitalini visiwe highlighted na kila mtu kuwajibishwa. Ninauhakika wafanyakazi watakao shitakiwa kwa wizi wa dawa na habari kuwekwa kwenye luninga na magazeti vitawapa wengine fundisho na woga wa kuwa na work ethics. Hii ndiyo sababu kazi nyingi za wizara ya afya ni wito. Unapowaweka vijana wenye akili timamu na elimu wakiwa hawana cha kufanya huoni kuwa ni fuel ya mambo kama yaliyotokea Egypt?
Hayo ndo mambo yanayoshughulikiwa sasa, hapo kwenye uadilifu kilikua kilio cha miaka mingi, kwa sasa Nuru inaanza kuonekana.
Ajira bado mkuu angalia wasomi wanaohitimu alafu angalia ajira za serikali ni kiasi gani, mengine hayawezekani hata aje nani hataweza kuajiri wahitimu wote
 
Penye miti hapana wajenzi.

Magufuli anachosema kuhusu chakula kinaingia akilini.

Watanzania watie akili.
Muogopeni Allah nyie watu
IMG_20170112_103811_435.jpg
 
Back
Top Bottom