Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Mkuu mto Nile nimetolea mfano nina maana tunatakiwa tuanzishe kilimo cha umwagiliaji kutumia mito na maziwa tuliyonayo
Nahisi una tatizo kwenye mental faculty yako! Wewe ni Mmoja ya wanaoishi kwa nadharia za KIPUUZI! Hiyo mito Hali yake ikoje? Ipo mingapi na kijiografia inawagusa kina Nani na kina Nani hawaguswi? Umefikiria kuhusu irrigation schemes/ infrastructures namna zitakavyowafikia watu wote? Tembea, Tz Ni kubwa, acheni kukaa town/city centers na kuongelea Rural areas kwa nadharia za KIPUUZI!
 
Kwann mnachanganya Sasa? Ishu ni Kuna njaa au hakuna. Mnapokubali kuhusu watanzania wavivu sijui Kuna mito na maziwa hawataki kilimo cha kumwagilia Basi kubalini Kuna njaa maana hao watanzania wavivu hawakulima. Kubalini Kuna njaa alafu ndio mseme hampeleki chakula cha msaada sababu watu wavivu hawakulima kutumia kilimo cha umwagiliaji. Ila kubalini Kuna njaa
 
Uongozi wa TZ raha sana mwenye njaa anaambia tuna nunua Ndege hili utalii ukue ....
Something joking here
 
Nchi kama misri walijua wako jangwani hivo walitengeneza miundo mbinu ya umwagiliaji ili waepuke balaa la kukosa chakula

Sasa unapokuja na hoja ya kilimo cha umwagiliaji lazima ujue nchi yetu iko katika ukanda ambao hua tunategemea mvua ila hali ya hewa imebadilika sasa tunapata matatizo sasa wananvhi wajitemgenezee miundo mbinu ya umwagiliaji ?? Kama maji ya kutumia tu simiyu ni shida hayo ya kumwagilia wanapata wapi


Acha kuwa mnafki
Nawe nadhani inapaswa kuchange jinsi ya kushauri, why not sasa tusimpe rais hii changamoto kuwa serkali iboreshe miundo mbinu ya umawagiaji kwa kuwa kuna source za maji nyingi ili tulime? hii inaweza kumjulisha tu kuwa serkali ikiboresha kama walivyofanya maeneo mengi tunao uwezo na dhamira ya kufanya kazi,
 
Serikali ni muajiriwa wa wananchi.serikali ndo inatakiwa kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na kodi wanazotoa wananchi.magufuli analipwa mshahara kutokana na kodi zetu.kuna maeneo mvua zimekata mazao yamekufa chakula hamna.bhado unakataa kuwapelekea chakula.jua kuwa wale ndo mabosi wako.walioungua jua tarehe 25.kukuchagua wewe ili uingie madarakani.uwaongoze.watakapokwama uwasaidie.ila imekuwa vice versa.
 
Nawe nadhani inapaswa kuchange jinsi ya kushauri, why not sasa tusimpe rais hii changamoto kuwa serkali iboreshe miundo mbinu ya umawagiaji kwa kuwa kuna source za maji nyingi ili tulime? hii inaweza kumjulisha tu kuwa serkali ikiboresha kama walivyofanya maeneo mengi tunao uwezo na dhamira ya kufanya kazi,
Mkuu tahadhari ni bora kuliko tiba

Dalili zinaonyesha kabisa upungufu wa chakula swala ni kukubali kwanza unatafuta suluhisho then unaangalia jinsi yakukabiriana na tatizo baadae sasa unapokuja na hoja ya uzembe uvivu pigeni kazi ...sio sahihi kwa wananchi wako nchi ni watu serikali wanayoichangia mapato kupitia kodi inawajali vipi? Ina vision gani kwao baadae ina mikakati gani kuwanusuru?
 
Aliyenunua boti uozo la bilioni 8 ni nani? Magufuli
Aliyesema tuwachangie wahanga wa tetemeko kisha akazikwapua ni nani? Baadaye akaja na uongo mwingine eti zilikuwa ndogo!!! Nani alimwambia kuwasadia wahanga bilioni 16 ni pesa ndogo?
Aliyesema Serikalini kuna mishahara ya milioni 40 kwa kwezi ni nane? Mafuru akaweka ukweli hadharani akapoteza kazi.
Aliyesema ataiheshimu na kuilinda katiba ya Tanzania ni nani? Unaujua ukweli
Unadhani kwani mkewe aligoma kumfanyia kampeni? Kuna mtu Tanzania hii anayemjua Magufuli fika kama Janeth Magufuli? Tia akili kichwani cheza mbali na unafiki.
Kwanza kabisa meli sio mbovu ina kasoro za kitaalam inarekebishwa na supplier kwa gharama zake, pesa za tetemeko zimepigwa kwenda wapi zimeenda uswiss? Hapana zimechangia matibabu na mazishi ya wahathirika na huduma zingine ndogondogo lkn zinaendelea kujenga miundo mbinu mbali mbali. Mafuru aliondolewa kwa sab za kinidhamu sio kusema ukweli kwa sab huna kigezo chochote cha kuona ukweli ni wa mafuru tu lkn sio magufuli na kuhusu kampeni janeth ulitaka ampigie vipi na baadhi ya mikutano ya kampeni alishiriki na kumuombea kura mume wake? Na unataka kuimply nini kwenye maisha yao watu ambao wako pamoja ikulu na wana watoto wanalea?
 
uyo nae itakuwa kanunuliwa na watu wa chama fln ili aseme tz hakuna njaa
 
Mie binafsi nakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa hapa nchini hakuna njaa. Tanzania ni moja wapo za nchi ambazo mwenyezi Mungu ameipa kila aina ya neema lakini watu wake hawataki kuitumia ipasavyo kwa sababu ya kutotaka kufanya kazi haswa za kilimo.
Leo nchi kama Misri yenye idadi ya watu karibu Milioni 100 wanaishi kwa kutegemea kilimo cha umwagiliaji kutoka mto Nile inakuwaje hapa Tanzania tuna maziwa na mito mengi mbali mbali na mvua kunyesha mara kwa mara tunashindwa kuwa na chakula na kusingizia njaa?
Sasa hivi tuna kiongozi asiyekuwa mnafiki anachowaambia watanzania ni ukweli mtupu na inatakiwa mkubaliane na ushauri wake kwamba kuna wafanyabiashara na wanasiasa wanajaribu kutengeneza hili suala la njaa kwa manufaa ya kujipatia umaarufu wa kisiasa na faida ya kibiashara.
Wala hukumwelewa!!!
 
Kalime mazao yanayostahimili ukame uone kama utakuwa na njaa. Naona Mr. Vya bule yuko akilini mwako. Pigs kazi acha kulalama serikali haitakuletea chakula by unbani kwako.
Hapa JF hakuna anaetaka hicho chakula! Ila wale wanavijiji masikini, ambao kipindi cha kampeni mlikuwa wapole na kuwaambia Serikali hii itakuwa kwa ajili yao, wapelekeeni chakula! Mnawapa kazi ya kuwa miungu ili kujua mwakani mvua hazitanyesha! Mnawajua kabisa kwamba ni masikini, ila mnataka walime kilimo cha kumwagilia, mnawafahamu masikini nyie? Jiografia ya Nchi mnaifahamu, mmechukua hatua gani km Serikali kwa kutumia Kodi zetu kutufikishia miundombinu ya kuwezesha kilimo cha umwagiliaji? Mbona mnaishi nchi ya kufikirika? Ni Wanyonge/ masikini gani hao mnaojinasibu kuwa hii Serikali ni yao?
 
Tanzania kuna njaa kweli kweli. Huo ndio ukweli. Bora tuseme ukweli ili tupone, kuliko kuficha aibu huku tukiangamia.

Achana na porojo za yule 'Mfalme' asiyependa kuusikia ukweli unaomuumbua.
Ukisema ukweli gani ndio utapona? Njaa iko wapi? Mbona hakuna mtu aliyekufa kwa njaa? Tofautisha upungufu wa chakula na njaa, magufuli hana uwezo wa kuzuia au kukanusha njaa kama kweli ipo ni sawa na kuficha mimba changa sababu itakua tu.
 
Kilimo cha umwagiliaji ni lini kimewahi kuwa kipaumbele cha serikali za CCM?

Acha kujitoa akili.
Hivi ni lini watanzania tutajitegemea kwa akili na uwezo wetu sisi wenyewe? Kilimo cha umwagiliaji nacho unataka serikali ije ikwambie fanyeni? Namkumbuka jamaa mmoja anaitwa Yethro Tull alivyofanya mapinduzi ya kilimo uingereza na namna baadae serikali ilivyokuja kumsapoti
 
Hakuna mwenye njaa Tanzania.Kila mtanzania anakula kuku ,nyama na mayai kila siku.
Wanaolia njaa ni wapiga dili.
Tofautisha njaa na upungufu wa chakula mtu kama alikuwa anakula milo mitatu na sasa anakula miwili au mmoja hiyo sio njaa.
 
Huyu rais ni genius sana..na kubwa anawaelewa watanzania kuliko wanavyojielewa..anajua watanzania hawawezi kujiongoza wenyewe kwa utashi wao ndio maana akitokea hata mwanasiasa akasema huyu mtu ni mchafu mzomeeni, watu watamzomea na kesho akigeuka na kusema huyu ni msafi mlambeni miguu watu wanalamba..
Maana yangu ni hii rais alizuia uuzaji wa chakula Nje ya nchi..watu wenye akili ndogo yaani upinzani wakashauti sana..ooh mipaka ifunguliwe,.genius katika ubora wake akaaema haya ngoja tuone,uzeni..watu wakauza chote.. Haijapita hata miezi sita eti wakiongozwa na hao hao waliowashawishi wauze wanalia njaa..ajabu wanapaza sauti eti rais atangaze njaa..kweli magufuli aliona mbali..ndio maana huwa tunasema nchi hii hatujapata mwanasiasa ila tumempata Kiongozi na ndio maana tunaunga mkono jitihada za kupiga marufuku mikutano uchwara ya siasa..
 
Kwaio hakuna njaa sababu Mungu ameijalia Tanzania mito mingi na Misri inalisha watu 100 millioni kwa kutumia mto nile, unaweza kwenda shule na usielimike...
 
Back
Top Bottom