Serikali ndo kila kitu kuwawekea sawa miundombinu ya maji wananchi wake,hakuna mahali kwenye maji ya kutosha na wananchi wakawa hawalimi wakailalamikia serikali wana njaa.hakuna sehemu kama hiyo.sehem nyingi zenye njaa zina ukame na vyanzo vya maji kwa ajili ya umwagiliaji hakuna hili sasa ni jukum la serikal iangalie nini cha kufanya kwa wananchi wake wapate maji
Unajua Maelezo bila takwimu inakuwa vigumu hata kuchangia. Kiukweli nchi ina eneo la kekta milioni 40 linalofaa kwa Kilimo, asilimia 10.2 ya eneo hilo ndilo linalolimwa. Eneo linalofaa kuendelezwa miundombinu ya umwagiliaji ni hekta milioni 29.4. Eneo lenye miundombinu linakaribia hekta laki 5 tu. Maeneo haya yote kwa sasa yanategemea maji ya juu ya ardhi ambayo kama mvua isiponyesha maji hayo nayo hukauka. Kwahiyo, kinachotakiwa kwa sasa ni kuhifadhi maji kwa kukinga maji ya mvua ambayo hufurika kwenda baharini kunapokuwa na mvua nyingi.
Kwahiyo, Kilimo cha umwagiliaji kinatakiwa kuwa ni strategic ukizingatia mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa.
Hili ni jambo linalohitaji uwekezaji mkubwa kwa maana ya rasilimali. Nayazungumza haya ili mtu asidhani kuwa ujenzi huo ni jambo la kulala na kuamka ukakuta kuna miundombinu inayotakiwa kwa umwagiliaji. Hili ni jambo la kupangilia kwa muda mrefu.
Jambo jingine ni kwa wananchi ambao wamebahatika kuwa sehemu ya hizo hekta laki 5 zenye miundombinu ya umwagiliaji kujipanga vizuri kutumia ardhi hiyo kwa tija zaidi ili kupata manufaa zaidi kwa kuzalisha chakula hata mara mbili kwa eneo kwa mwaka.
Tija kwa eneo bado iko chini hata kwenye maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji. Hivyo, wakulima na wadau tunayo kazi ya kufanya ili tuweze kupiga hatua zaidi tutoke kwenye Kilimo cha kujikimu na kuwa na Kilimo cha kibiashara.
Serikali haina mashamba Bali inaweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo na wataalam. Wananchi tunatakiwa kujiongeza kwa kutumia fursa zilizopo kwa kulima kibiashara. Tunapokwama tunaiambia serikali nn tumekwama na tunahitaji msaada upi.
Suala la mvua kutonyesha au kuchelewa Serikali inalaumiwa kwa lipi? Kwakuwa mvua hunyesha kwa neema na rehema za mungu.
Nilitegemea wananchi waiombe Serikali kama kuna uhaba wa mbegu zinazovumilia ukame ama kuomba kupatiwa ruzuku ya aina fulani n.k.
Kwahiyo, tujenge hoja zinazoweza kutusaidia kama nchi kuondokana na tatizo, tutoe ushauri ambao utasaidia serikali na wananchi kujipanga vizuri zaidi katika Siku za usoni, kukabiliana na majanga.
Huo ndo mchango wangu kwa sasa, najua kuna wengine watakuwa na michango mizuri zaidi ya kutujenga.