Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Huyu unayemsifia mbona kasema mengi tu ya uongo
Tatizo kuna misukule ya fisiem. Kuna clip nimeipata nitairusha. Watu wamechoka na huu utawala bora wafungwe tu. Msukule wa fisiem hawez kukuelewa.
Km anasema ukweli na mpenz wa Mungu. Vip kuhus ajira za watu? Yy anakula na kunywa hiyo njaa ataiona wapi km ajira zenyew kaziweka kapun halaf anasem hapa kaz tu.
 
Siku zote binadam hana shukurani yule mlikuwa mnamwita Dhaifu sasa wasasa anawasafishia nchi ni mbaya pia what kind of Presidential material you want?
Suala la first lady kila kiongozi ana hulka yake kama Mheshimiwa hataki kumhusisha mambo ya siasa ni dhambi?
Rais Magufuli kama mwanadamu hakosi mapungufu lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpe


amesafisha hadi sembe na chumvi sukar ndo usiseme hatar tupu
 
Hivi ni lini watanzania tutajitegemea kwa akili na uwezo wetu sisi wenyewe? Kilimo cha umwagiliaji nacho unataka serikali ije ikwambie fanyeni? Namkumbuka jamaa mmoja anaitwa Yethro Tull alivyofanya mapinduzi ya kilimo uingereza na namna baadae serikali ilivyokuja kumsapoti
Umeandika vizuri. Watu wana mawazo mazuri lkn pesa. Unaongea utafikiri tupo ulaya vile wakati upo tz nchi yenye dhambi ya kila aina.
Ww umefanya nn kweny kilimo? Km serikali tu mpaka sasa haijahamia dodoma, mwananchi wa kawaida anayeishi chin ya dola 1 ataweza?
Usiongee tu km mfalme wenu
 
Ukisema ukweli gani ndio utapona? Njaa iko wapi? Mbona hakuna mtu aliyekufa kwa njaa? Tofautisha upungufu wa chakula na njaa, magufuli hana uwezo wa kuzuia au kukanusha njaa kama kweli ipo ni sawa na kuficha mimba changa sababu itakua tu.

OK kumbe njaa hadi watu wafeee nilikua silijui hili. Kwa hiyo maana ya njaa ni kifo asante sana ndio maana tunawapenda wasomi mnatuweka sawa sisi tusiosoma
 
Watu wafanye kazi mkuu, hivi unadhani hata serikali ikiamua kutoa misaada ya chakula kila kaya inapata kiasi gani? Hakitazidi debe tano, sasa hizo debe tano zikiisha wanaenda wapi?
Watanzania kwa bahati mbaya tulizoea vibaya sana akili za utegemezi na kulaumu laumu kila kitu.
Magufuli kaza Uzi tu, next time watu watalima chakula kitaozea kwenye maghala

Njaa ya familia yako sio hoja ya msingi sana kwa serikali, watu wanafanya uzembe kila kitu ili mwishoni walaumu serikali.

"Poor minded people will always blame politicians for their own problems "
Fanyeni kazi watanzania, acheni maneno ya wanasiasa, hata kama chakula kimepungua serikali haiwezi kuwalisha ninyi nyote, tuna uchumi gani wa kulisha nchi nzima hata kwa wiki mbili? Wanasiasa wanawadanganya oooh serikali haiwajali wananchi wake wakati wa njaa sasa hao wakiingia madarakani wataweza kuilisha nchi hii hata wiki mbili in case kuna njaa?
Ni kweli sisi bado ni maskini wa vipato, tusikubali kua maskini wa akili, kukaa tunalaumu laumu kila kitu, igeni mifano ya wachaga wao wanachakarika, wakati nyie wengine mnalialia wao magari yanaongozana kwenda Moshi kusheherekea Christmas sasa wao wako Tanzania gani? Au wote ni wapiga dili?

Fanyeni kazi bhana

Nikiangalia hekari zangu 4 mahindi yanakauka then ww unasema ni uvivu natamani hata nijitoe muhanga kwako. Najua upo town unapesa za kununua chakula sasa kisipofika sokoni utanunua nn
 
Mie binafsi nakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa hapa nchini hakuna njaa. Tanzania ni moja wapo za nchi ambazo mwenyezi Mungu ameipa kila aina ya neema lakini watu wake hawataki kuitumia ipasavyo kwa sababu ya kutotaka kufanya kazi haswa za kilimo.

Leo nchi kama Misri yenye idadi ya watu karibu Milioni 100 wanaishi kwa kutegemea kilimo cha umwagiliaji kutoka mto Nile inakuwaje hapa Tanzania tuna maziwa na mito mengi mbali mbali na mvua kunyesha mara kwa mara tunashindwa kuwa na chakula na kusingizia njaa?

Sasa hivi tuna kiongozi asiyekuwa mnafiki anachowaambia watanzania ni ukweli mtupu na inatakiwa mkubaliane na ushauri wake kwamba kuna wafanyabiashara na wanasiasa wanajaribu kutengeneza hili suala la njaa kwa manufaa ya kujipatia umaarufu wa kisiasa na faida ya kibiashara.
umeishia hapo tu!!???
 
Ukosefu wa virutubisho ktk vyakula naona unaathiri hata uwezo wa watu kufikiri, kusema Tanzania ina ardhi nzuri lkn inapata njaa ni sawa na kusema Tanzania ina chuma lkn haitengenezi gari au Tz inalima Pamba lkn inaimport jeans - poor argument.

What matters most is the policy, sera ya kilimo ikoje? je tuna sera ya kilimo inayowezesha kujitosheleza kwa chakula? Mliimba wimbo wa kilimo kwanza, what was the policy? mliishia kununua mashangingi wakulima wakabaki na jembe lao la mkono, waafrika tutabaki nyuma sana kwa kuwa tuna wishful thinking ambayo haifikirii mechanism of achieving the objective.
 
Mtoa post nadhan umekurupuka tu, Kwan nilini CCM imewekeza ktk kilimo cha umwagiliaji ? Ila mungu anawaona kwa unafiki wenu
 
OK kumbe njaa hadi watu wafeee nilikua silijui hili. Kwa hiyo maana ya njaa ni kifo asante sana ndio maana tunawapenda wasomi mnatuweka sawa sisi tusiosoma
Vifo ni matokeo ya njaa ambayo mnadai ipo lkn dalili za njaa sio kifo. Tanzania hakuna njaa wala dalili za njaa bali kuna upungufu wa chakula ulio sababishwa ukame uliozikumba baadhi ya wilaya lkn chakula kilichopo kwenye mikoa mingine ambayo haijakumbwa na ukame kinatosha kusustain nchi mpk mwakani halafu vile vile upungufu mkubwa upo kwenye mahindi pekee lkn nafaka zingine hazina upungufu kama mtama mchele uwele na mazao jamii ya kunde kwahiyo hakuna njaa na haitatokea besides mvua zimeanza kunyesha kwa mfano wilaya ya rufiji huwa wanapanda mpunga tar 20 mpk 25 ya kila dec ya mwaka lkn kutokana na kuchelewa kwa mvua wameanza kupanda tarehe 5 January baada ya kupata mvua kuanzia tar 1 jan sasa kuchelewa huko kutasababisha NJAAAA?
 
ww naona hujielewi hata kidogo kwa kumtete huyu jizi mwaaaafaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna watu Wa ajabu sana tatizo La Tanzania sio rasilimali Bali matumizi ya hizo rasilimali serikali ndio inayotakiwa kuweka mazingira mazuri mfano suala La irrigation schemes Nani anatakiwa kuzijenga? Kilimo kwanza ulikuwa Sera ya serikali walifanya nini kuboresha Kilimo kiwe cha kisasa? Leo mvua hakuna karibu nchi nzima unabishaje sasa kama hakuna njaaa bei ya unga na mchele vimepanda bado watu hawajiulizi kwa nn, so ukisema kuwa hakuna njaaa basi sema hakuna haja ya kukopa au kupewa Msaada na Morocco kwa kuwa ss na Morocco Nani ana rasilimali nyingi? Mbona bado tunaomba Msaada kwenye nchi jangwa? Naona tunakimbia kivuri chetu so mleta mada umepungukiwa kidogo akiri au huyajui mazingira ya Tanzania kwa maana hujatembea ndani ya nchi hii zaidi ya kukaa town mchele unaenda kununua kisutu. Kwa kifupi Kilimo cha umwagiliaji nchi hii ni kwa wachache yaani hata 2% hawafiki waliobaki ni Kilimo mvua au wanaolima mbogamboga pembezoni mwa mto napo serikali hairuhusu. Kilimo cha umwagiliaji kinahitaji uwekezaji Wa miundo mbinu ndugu zetu wengi ni maskini usichukulie poa.

Ulifanya upembuzi na mchanganuo wa kufanya "Irrigation" ukanyimwa?
 
Binafsi nimechoka na matamshi yako yakukatisha tamaa, lakini nasema hivi njia ya muongo ni fupi sana tena sana ipo siku .......
 
Njaa ipo na itaendelea kama mvua za masika nazo hazitonyesha vizuri. Si kwamba watu ni wavivu, wamelima ila mvua haikunyesha ilivyopaswa. Mimea inakauka mashambani, hili si la kiunafiki.

Umwagiliaji ktk schemes kubwa kubwa ni jukumu la serikali, eidha kupitia wawekezaji au yenyewe, kivyovyote vile ustawi wa nchi uko mikononi mwa serikali, ndo watunga sera zote na kusimamia utekelezaji wake.

Tumejikwaa hapa, tumeliona kosa, tunyanyuke na tukimbie, tusichelewe zaidi.
 
Unafiki umekuzidi wewe. Kuwa na wananchi kama wewe nchini ni hasara kubwa sana kwa Taifa maana upumbavu wenu wa kupigia makofi udikteta uchwara, uongo, ubadhirifu, wizi, ufisadi, utoaji rushwa na upkeaji rushwa ndito unawapa kiburi hawa mafisadi.

MV Dar es Salaam kufa kabla ya kuanza kazi?

Kwanza kabisa meli sio mbovu ina kasoro za kitaalam inarekebishwa na supplier kwa gharama zake, pesa za tetemeko zimepigwa kwenda wapi zimeenda uswiss? Hapana zimechangia matibabu na mazishi ya wahathirika na huduma zingine ndogondogo lkn zinaendelea kujenga miundo mbinu mbali mbali. Mafuru aliondolewa kwa sab za kinidhamu sio kusema ukweli kwa sab huna kigezo chochote cha kuona ukweli ni wa mafuru tu lkn sio magufuli na kuhusu kampeni janeth ulitaka ampigie vipi na baadhi ya mikutano ya kampeni alishiriki na kumuombea kura mume wake? Na unataka kuimply nini kwenye maisha yao watu ambao wako pamoja ikulu na wana watoto wanalea?
 
Kivuko MV Dar es Salaam; Je, ni udanganyifu, ufisadi au utapeli wa serikali ya CCM?

Acha unafiki wewe! Bakhressa kanunua boti jioya kwa bilioni 5 tu na halina kasoro zozote za kitaalamu iweje boti la bei kubwa zaiidi karibu mara mbili ya bei liwe na kasoro za kitaalamu!? Boti ni uozo Magufuli kafanya ufisadi wa kununua boti uozo la mwaka 1978.

Kwanza kabisa meli sio mbovu ina kasoro za kitaalam inarekebishwa na supplier kwa gharama zake, pesa za tetemeko zimepigwa kwenda wapi zimeenda uswiss? Hapana zimechangia matibabu na mazishi ya wahathirika na huduma zingine ndogondogo lkn zinaendelea kujenga miundo mbinu mbali mbali. Mafuru aliondolewa kwa sab za kinidhamu sio kusema ukweli kwa sab huna kigezo chochote cha kuona ukweli ni wa mafuru tu lkn sio magufuli na kuhusu kampeni janeth ulitaka ampigie vipi na baadhi ya mikutano ya kampeni alishiriki na kumuombea kura mume wake? Na unataka kuimply nini kwenye maisha yao watu ambao wako pamoja ikulu na wana watoto wanalea?
 
Back
Top Bottom